Mwenyekiti
wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm akitoa mada kuhusu
haki za binadamu jinsia na mitazamo ya Mataifa Mbalimbali ulimwenguni
kuhusu Uhuru wa Habari na Haki za Binadamu siku ya mwisho ya Kongamano
la maadhimisho ya Uhuru wa Habari duniani kwenye Hoteli ya Naura Springs
jijini Arusha. (Picha na Dewji Blog).
Mkurugenzi
wa Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akitoa maoni yake katika
kuchangia Azimio la Arusha la kupaza sauti za waandishi wa habari kudai
uhuru wa habari kwenye siku ya pili ya kongamano la kuadhimisha Siku ya
Uhuru wa Habari Duniani lililomalizika leo jijini Arusha.
Pichani
juu na chini ni washiriki wa kongamano la siku mbili la kuadhimisha
siku ya uhuru wa habari duniani hapa wakiwa wanafuatilia mjadala na mada
mbali mbali zilizopelekea kutoka na azimio la Arusha la waandishi wa
habari katika kudai mambo mbali mbali zikiwemo changamoto na sheria za
tasnia hiyo zinazotumika hapa nchini.
Mwakilishi
wa COMNETU ya nchini Uganda Jimmy Okello akitoa mada kwenye kongamano
hilo juu ya Usalama na Ulinzi wa waandishi wa habari wa Kenya na Uganda
na kueleza kuwa hali Usalama na Ulinzi kwa waandishi wa habari kwenye
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinalingana hazitofautiani japo
zingine zimepiga hatua kwa sheria ya uandishi wa habari kuingizwa kwenye
Katiba.
Kutoka
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Nyirembe Munasa,
Mwenyekiti wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm
na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO wakifuatilia mada
mbali mbali zilizokuwa zikijadiliwa ambapo leo waandishi wa habari
wametoka na Azimio la Arusha linalohusu mazingira ya usalama wao wawapo
kazini na mazingira ya vyombo vya habari ikiwemo pia Serikali.
Mwalimu Ayubu Rioba akifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano hilo.
Mama Rose Haji wa UNESCO wakifurahia jambo Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige.
Mwakilishi
wa Mo Blog jijini Arusha Mahmoud Ahmed (kushoto) akiwa na mhariri wa
Sibuka Fm Felix Kaombwe wakifuatilia majadiliano mbali mbali yaliyozua
Azimio la Arusha la Uhuru wa Habari ikiwemo kupitishwa kwa sheria ya
Uhuru wa Habari kwenye Katiba yetu na masuala ya Usalama wa mazingira
katika kazi zao za kila siku.
Usia
Nkhoma Ledama wa UNIC akiteta jambo na Mwenyekiti wa UN Tanzania Human
Rights Group Bw. Tobias Rahm wakati wa Kongamano la siku mbili
lillilomalizika leo jijini Arusha.
Mkuu
wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo wakati wa kufunga kongamano la Uhuru wa
Habari Duniani lililomalizika leo jioni jijini Arusha.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akizungumza kwa niaba ya
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
ambapo amewaasa wanahabari kutimiza majukuma yao na kutoiyona Serikali
kuwa inayafumbia macho madai yao na kuwa Azimio waliolotoka nalo
litafanyiwa kazi ili kuboresha muhimili wa tasnia hiyo.
Mwenyekiti
wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO akiongea kwa niaba ya Mashirika ya
Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi hapa nchini na kutoa shukrani kwa
kuona ushiriki na kufana kwa hafla nzima ya Kongamano la Uhuru wa Habari
Duniani na kuwa na imani kwamba Azimio la Arusha la Wanahabari
litafanikiwa. Kongamano hilo limemalizika leo jioni kwenye Hoteli ya
Naura Springs jijini Arusha.
Mkongwe
wa Habari Mama Eda Sanga (mwenye sweta jeupe) akiwa na wanafunzi wake
wakibadilishana mawazo mwishoni mwa Kongamano la Uhuru wa Habari
Duniani. Kulia kwake ni Gladness Munuo na Wa pili kulia Cecilia
Mng’ong’o na Aliyekaa ni Dominica Haule wote ni wafanyakazi wa GEMSAT.
Mmoja
wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni
Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akiwa na
Mhariri wa Sibuka Fm Felix Kaombwe na Meneja wa Program za Vipindi wa
Mpanda Fm Bw. Revocutus Andrew nje ya ukumbi wa mikutano.
NA DEWJI BLOG
0 comments:
Post a Comment