Waziri
wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira
Barani Afrika akiipongeza Hoteli ya DoubleTree by Hilton kwa kuona
umuhimu wa elimu kwa kukabidhi taa mia mbili kwa Shule za Msingi
zilizopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma , Shule zilizopewa msaada huo
ni Shule ya msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula , Taa hizi
zinazotumia Nishati ya jua pia ni rafiki wa mazingira. " Taa hizi
zitawasaidia kuepeuka kutumia vibatari na mishumaa muda wa kujisomea kwa
sababu ni hatari kwani vimekuwa vikisababisha majanga ya kuungua kwa
watoto wengi nchini ".
Mkuu
wa wilaya ya Songea Bw. Joesph Joseph Mkirikiti alie kaa katikati na
kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli
za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman na alie kaa kushoto
ni mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso
Kirambata wakati wa hafula ya kukabidhi msaada wa taa zinazotumia
nishati ya jua.
Mkuu
wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiteta jambo na
mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata
(kushoto) juu ya matumizi ya taa zinazotumia nishati ya Jua ambazo pia
ni rafiki wa mazingira kwa Wanafunzi wa darasa la Saba. Kulia ni
Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by
Hilton Tanzania Bw. Judd Helman.
Toka
kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso
Kirambata akiwa ameshikilia taa na wakatikati ni mkuu wa wilaya ya
Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiwa ameshikilia taa na wa mwisho
ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by
Hilton Bw. Judd helman.
Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by
Hilton Bw. Judd helman akimkabidhi moja ya taa inayotumia nishati ya Jua
mwanafunzi wa Shule ya Msingi Liumbu iliyopo ndani ya manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma .
Waziri
wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira
Barani Afrika hapa ni umati wa wanafunzi (Viongozi wa leo) kila mmoja
akitaka ampe mkono wa pongezi baada ya kumalizikla hafla ya kukabidhi
taa za nishati ya jua kwa shule nne za manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Wanafunzi
toka katika shule nne za msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na
Namang'ula na wakifatilia kwa makini hutuba iliyokuwa ikitolewa kabla
ya kukabidhiwa taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na
Hoteli ya DoubleTree by Hilton.
Wanafunzi
hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea
hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao
kielimu na kupunguza matumizi ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya
kusomea
Naye Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata amesema
"tumeamua
kufanya kampeni hii ambayo ni endelevu tutakuwa tukigawa taa 200 za
mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa
shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi
juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira vile
vile tunaomba wahisani wengine nao wajitokeze".
Picha na habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment