SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 23, 2013

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akutana na Waziri wa Ushirika wa Kimataifa wa Canada Mhe. Julian Fantino kujadili vipaumbele vya maendeleo ambavyo ni Elimu, Nishati, Rasilimali Fedha, Kilimo, Maji na Usafirishaji.

 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada Bw. Julian kabla ya kikao kuanza Fantino
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Wiliam Mgimwa pamoja na ujumbe wa Tanzania katika majadiliano ya pamoja na  Mhe. Julian Fantino ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa katikati mbele.  Aliyekaa kushoto kwake ni Bi. Margaret Biggs ambaye ni Rais wa Taasisi ya maendeleo ya  kimaifa(CIDA).
 Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada Mhe. Julian Fantino akisikiliza kwa makini ujumbe wa Tanzania kuhusu masuala ya Nishati, Elimu, Maji, Usafirishaji, Rasilimali Fedha na Kilimo.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar, Bw. Khamis Mussa.
 Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada Mhe. Julian Fantino aliyesimama, akisoma hotuba yake mbele ya ujumbe wa Tanzania. Aliyekaa kushoto kwake ni Bi Margaret Biggs ambaye ni Rais wa shirika la maendeleo la kimataifa (CIDA).
Kamishna wa Fedha za Nje Zanzibar Bi. Bihindi Nassor akisalimiana na Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada Mhe. Julian Fantino.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akisisitiza jambo kwa Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa Bw. Julian Fantino mara baada ya kikao kumalizika.

Habari Imetolewa Na, 
Msemaji Mkuu, 
Wizara Ya Fedha,
Ingiahedi Mduma,
23/April/2013.

0 comments:

Post a Comment