Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya cha 'Town' mkoani Lindi, Assumpta
Mpiri, akimtoa damu mtoto mchanga kupitia kisigino, tayari kwa kuikausha
na kuipeleka maabara kuu ya Taifa ya Muhimbili kwa njia ya mashine 'sms
printer' ambayo pia katika kipindi kifupi inauwezo wa kupokea majibu ya
vipimo hivyo tayari kwa kumkabidhi mzazi wa mtoto huyo. Mashine hizo
takribani 8 zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 11,
zimetolewa mkoani humo kwa msaada wa Vodacom Foundation chini ya uratibu
wa Taasisi inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya
ya Uzazi ya EGPAF
Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya cha 'Town' mkoani Lindi, Faida
Ibrahim, kwa kushirikiana na Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon,
akimtoa damu mtoto mchanga kupitia kisigino, tayari kwa kuikausha na
kuipeleka maabara kuu ya Taifa ya Muhimbili kwa njia ya mashine ya
kisasa 'sms printer' ambayo pia katika kipindi kifupi inauwezo wa
kupokea majibu ya vipimo hivyo tayari kwa kumkabidhi mzazi. Mashine hizo
takribani 8 zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 11,
zimetolewa mkoani humo na Vodacom Foundation, chini ya uratibu wa
Taasisi inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya
Uzazi ya EGPAF
Mratibu wa Uchunguzi wa VVU kwa Watoto Wachanga kutoka Taasisi Tafiti
za maendeleo ya Afya ya Uzazi wa mtoto, baba na mama wa EGPAF, Georgiah
Kasori (katikati) akitoa maelekezo ya namna bora ya kutumia mashine za
kisasa 'sms printers' zinazowezesha upatikanaji wa haraka wa vipimo vya
VVU kwa watoto wa umri wa kati ya mwezi 1 hadi miezi 18 kwenye Zahanati
ya 'Town' katika ziara iliyofanywa na Maofisa wa Vodacom Foundation
kukagua ufanisi wa mashine hizo mkoani Lindi. Zahanati hiyo ni miongoni
mwa Vituo vya Afya vilivyonufaika na mashine hizo takribani 8
zilizotolewa kwa hisani ya Vodacom Foundation
Mtaalamu wa Maabara ya Hospitali ya Mkoa wa Lindi, Julius
Mwansimba, (kulia) akimuonesha Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon,
ufanisi wa mashine 'sms printers' zinazowezesha upatikanaji wa haraka
wa majibu ya vipimo vya VVU kwa watoto wachanga ndani ya maabara ya
hospitali hiyo jana. Vodacom Foundation chini ya uratibu wa Taasisi
inayojishughulisha na Tafiti za Afya ya Uzazi wa mtoto, baba na mama ya
EGPAF hivi karibuni ilitoa msaada wa mashine hizo zipatazo 8 mkoani
Lindi, zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 10
Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Lindi, Zainab Mathradas,
(kulia), akimkabidhi mmoja wa wadau wa huduma za afya, ambaye ni Meneja
wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, taarifa ya takwimu na matokeo ya
ufanisi wa huduma ya Afya ya Uzazi wa mtoto, baba na mama mkoani Lindi.
Wengine wanaoshuhudia ni Maafisa waandamizi kutoka Taasisi
inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya
EGPAF. Vodacom Foundation hivi karibuni ilichangia mashine 8 'sms
printers' zenye gharama ya zaidi ya Dola Marekani elfu 10 mkoani Lindi,
zinazowezesha upatikanaji wa haraka wa majibu ya vipimo vya VVU kwa
watoto wachanga.
Mkazi wa Matokeni mkoani Lindi, ambaye anaishi na Virusi vya Ukimwi,
Iman Bakari, akiwaeleza wanahabari, na maofisa kutoka Vodacom Foundation
na Taasisi inayojishughulisha na Afya ya uzazi wa mtoto, baba na mama
ya EGPAF, namna mashine za kisasa 'sms printers'zilivyomuwezesha kupata
majibu ya vipimo vya VVU vya watoto wake wawili kwa urahisi na haraka.
Mashine hizo takribani 8 zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu
10, zimetolewa mkoani humo na Vodacom Foundation, chini ya uratibu wa
Taasisi inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya
Uzazi ya EGPAF .
Mganga Mkuu wa mkoa wa Lindi, Dk Sonda Shaaban, akifafanua jambo
mbele ya maofisa wa Vodacom Foundation na Taasisi inayojishughulisha na
tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF, (hawapo pichani),
sanjari na kutoa tathmini ya jinsi mkoa huo ulivyojipanga kukabiliana na
changamoto ya afya ya Uzazi wa mtoto, baba, na mama kwenye eneo la
maambukizi mapya ya VVU toka kwa baba na mama kwenda kwa mtoto. Vodacom
Foundation hivi karibuni ilichangia mashine 8 za kisasa 'SMS PRINTER'
zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 10 ndani ya mkoa huo,
katika kuwezesha upatikanaji wa haraka wa majibu ya vipimo vya VVU kwa
watoto wachanga.
0 comments:
Post a Comment