SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, October 12, 2012

WASANII DIAMOND NA LINAH WAWATAKA WATANZANIA HASA VIJANA KUPIGIA KURA TANZANIA KATIKA SHINDANO LA VIVUTIO VYA ASILI VYA AFRIKA.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdull Naseeb almaarufu Diamond akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro mwishoni mwa wiki na kutanabaisha kuwa watatumia nafasi yao kama wasanii kuwaomba vijana wenzao kuvipigia kura vivutio hivyo ikiwemo mbuga ya Serengeti, Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro. Kwa picha zaidi tembele mtandao wake 


Abdull Naseeb almaarufu (Diamond)
Mahmoud Ahmad Arusha.
Vijana nchini wameshauriwa kuvipigia kura vivutio vitatu vya utalii vilivoainishwa hapa Tanzania ili viweze kuingia kwenye shindano la vivutio vya asili vya afrika, kwani wao wana nafasi ya kufanya hivyo kwa kuwa wanatumia mtandao kwenye shughuli zao nyingi za kila siku.

Kauli hiyo imetolewa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Abdull Naseeb almaarufu Diamond na Linah Sanga kwa nyakati tofauti, wakati walipotembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro mwishoni mwa wiki na kutanabaisha kuwa watatumia nafasi yao kama wasanii kuwaomba vijana wenzao kuvipigia kura vivutio hivyo ikiwemo mbuga ya Serengeti, Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake Diamond amesema kuwa alikuwa akiwaona wanyama hao kupitia kwenye luninga lakini ameweza kuwaona kwa uhalisia, hivyo anakubaliana kuwa sasa tubebe uzalendo kuweza kuvitangaza vivutio vyetu mahali popote ulimwenguni na kuwataka vijana na watanzania kuanza kupenda utamaduni wa kutembelea mbuga zetu.

Diamond amesema kuwa Tanzania imejaaliwa kuwa na vivutio ambavyo ni nadra kukuta sehemu nyingine duniani lakini sisi tumekuwa nyuma kuvitangaza na kuvitembelea huku ni kuwa watumwa wa wenzetu na kuwataka vijana na watanzania kwa ujumla kuweza kuweka uzalendo na kuacha kutizama kupitia kwenye luniga vipindi vya wanyama na kwenda kutembela mbuga zetu popote zilipo hapa nchini.

Na kwa upande wake msanii Linah Sanga amesema kuwa yeye alikuwa hajawahi kuwaona kwa uhalisia Simba na wanyama wengine kwa ujumla lakini ameweza kuona wanyama hao na pia ameweza kuona Crater jinsi ilivyo akiacha alivyosoma shuleni kwa kweli ni mandhari ya kuvutia na inafaa kuipigia kura ili iweze kuwemo kwenye maajabu saba ya Afrika.

Linah amesema kuwa wao kama wasani watawaomba vijana wenzao popote hapa nchini kutumia muda wao wa ziada kutembelea mbuga zetu, ili kuweza kuvitangaza vivutio hivyo kwenye kaya zao ili nchi yetu iweze kupata pato kupitia utalii wa ndani na kuwataka watanzania kuvipigia kura vivutio vyetu ili kuweza kushinda na taifa kuweza kuingiza pato.

Nae Kaimu Mhifadhi wa mamlaka ya Ngorongoro Dkt. Fransic Mumba amesema kuwa ni bahati kwa watanzania kupata nafasi ya vivutio hivyo vitatu ikwemo Ngorongoro, Serengeti na Mlima Kilimanjaro kuweza kupigiwa kura ili viweze kuingia kwenye maajabu saba ya Afrika na kuwataka watanzania kuvipigia kura Vivutio hivyo.

Dkt. Mumba amesema kuwa anawaomba vijana wengi kuvipigia kura vivutio hivyo kwa kuwa wamekuwa mstari wa mbele kwenye matumizi ya mtandao hivyo wataweza kupiga kura kwa urahisi huku akitanabaisha jinsi ya upigaji wa kura hizo.

0 comments:

Post a Comment