Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu.
Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wakimwingiza katika gari muumini wa Kiislamu aliyekamatwa katika viunga vya maeneo ya Ikuu
Safari ya kuelekea Kituo Kikuu ilianza
Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea jana
Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo
Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo jana
Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo jana
Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo jana
Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara yaMsimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana.
Picha zote na Happiness Mnale.




0 comments:
Post a Comment