SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, September 30, 2012

BONDIA FRANCIS CHEKA AMCHAKAZA KALAMA KWA K.O

Bondia Francis Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Kalama Nyilawila. Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya Kalama kusalimu amri, kushoto ni Rais wa PST Emmanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Bondia Francis Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Kalama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika jana usiku. Cheka alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa.
Bondia Cheka (kushoto) akimshambulia Kalama Nyilawila kwa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika jana usiku. Cheka alishinda raundi ya sita baada ya Kalama kashindwa kuendelea.
Bondia Kalama Nyilawila (kulia) akijitahidi kukwepa makonde ya mpinzani wake Francis Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika jana usiku.
Mabondia Kalama na Francis Cheka wakizidi kutupiana masumbwi.

0 comments:

Post a Comment