SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, August 17, 2012

SERIKALI KUVIPATIA UMEME VIJIJI 21 MKOANI SINGIDA KUHARAKISHA MAENDELEO ENDELEVU.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini George Simbachawene (Mb)akizungumza na wananchi wa kata ya Kaselya jimbo la Iramba Magharibi. 
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini George Simbachawene (wa kwanza kulia) akisaini kitabu cha wageni cha ofisi ya kata ya Kaselya.
Na.Nathaniel Limu.
Serikali imeahidi kuvipatia umeme wa grid vijiji 21 vya jimbo la Iramba Magharibi na Iramba Mashariki ili pamoja na mambo mengine kuharakisha upatikaji wa maendeleo endelevu.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kaselya jimbo la Iramba Magharibi  Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene, amesema kati ya vijiji hivyo, kijiji cha Msingi na Milade, ni vya jimbo la Iramba Mashariki na vilivyobaki 19 ni vya jimbo la Iramba Magharibi.
Simbachawene ametaja baadhi ya vijiji vya jimbo la Iramba Magharibi vitakavyonufaika na mradi huo kuwa ni Kaselya, Mbelekese, Ndulungu, Malendi, Kitusha, Lugwala, Moto moto, Kizaga, Kitukuntu, Kibigiri, New Kiomboi, Makunda na Maluga.
Naibu Waziri huyo amesema vijiji hivyo vitapata umeme kwa awamu tofauti, lakini vijiji vya Mbelekese, Kaselya na Ndulungu, vitapata umeme katika mwaka huu wa fedha utakaoishia juni mwakani.
Amesema kutokana na hatua hiyo, hivi sasa hakuna haja ya vijana kukimbilia mijini ambako hakuna kazi za kufanya.
Kwa hali hiyo, amewataka wakazi wa vijijini, wasidhani kuwa umeme ni kwa ajili ya kuwasha wakati wa kulala tu, umeme pia ni kwa ajili ya maendeleo yao.
Naye mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Lameck Nchemba, amewataka wakazi wa maeneo yatakayopatiwa umeme, kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makandarasi watakaopewa kazi ya kusambaza umeme vijijini ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa haraka. 

0 comments:

Post a Comment