
Mwanae huyo Charles Sirleaf ni miongoni mwa maafisa 46 waliosimamishwa kazi kwa kushindwa kuweka wazi mali zao mbele ya maafisa wa tume dhidi ya rushwa.
Charles ni mmoja kati ya watoto wake watatu walioteuliwa kushika nyadhfa za juu baada ya rais huyo kushinda tena katika uchaguzi mwaka uliopita, ambapo wachambuzi wa mambo wamekuwa wakimtuhumu kwa endekeza undugu.
Rais Ellen Johnson Sirleaf alimteua motto wake mwingine Fumba kuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa, mwingine Robert ameuliwa kuwa Mshauri Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mafuta inayomilikiwa na serikali National Oil Company of Liberia (NOCAL).




0 comments:
Post a Comment