SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, August 16, 2012

RAIS KIKWETE AZITAKA HALMASHAURI ZA BARA NA VISIWANI KUJIANDAA KUFANIKISHA MIRADI YA MAENDELEO.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye  mabanda ya maonyesho ya bidhaa zilizozalishwa kutokana na mradi wa Tasaf awamu ya Pili kabla ya kuzindua  mradi wa Tasaf awamu ya Tatu.  Kushoto kwake ni Skipa wa Bunge la Jamhuri Mh. Anne Makinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayesimamia Uratibu na Mahusiano Mh. Steven Wasira. 
 
Rais Kikwete akiangalia bidhaa za moja ya banda la miradi ya wajasiriamali iliyoanzishwa katika awamu ya pili ya mradi wa Tasaf nchini Tanzania katika uwanja wa michezo wa Jamuhuri Mjini Dodoma.  Kushoto kwake ni Spika wa Bunge Mh. Anne  Makinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi . 
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Tasaf mara baada ya kuzindua Mradi wa Tasaf awamu ya Tatu.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema wakati umefika kwa Halmashauri za Wilaya Tanzania Bara na Zanzibar lazima zilenge kujiandaa vyema katika kufanikisha miradi ya maendeleo iliyobuniwa na hatimae kuanzishwa na wananchi wenyewe katika maeneo yao.                                                                                                                    
Dkt. Kikwete ametoa agizo hilo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (Tasaf) awamu ya tatu zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Jamuhuri Mjini Dodoma.                                                                                          
Rais Kikwete amesema ipo miradi mingi iliyoanzishwa na wananchi na kukamilika akaitolea mfano ile ya Majengo ya Vituo vya Afya na shule lakini hadi sasa inashindwa kutoa huduma zinazostahiki kutokana na sababu ya ukosefu wa watendaji walioatayarishwa na Halmashauri husika.                                                                                                                                                   
Amesema utaratibu huo ukipuuzwa kwa kiasi kikubwa unaweza kupunguza ari ya Wananchi ya kubuni miradi itakayowaletea faida yao kiuchumi pamoja na  kijamii kwa nia ya kupunguza umaskini.                                                                                                                                                       
Akizungumzia Awamu ya Tatu ya Tasaf Rais Kikwete amesema maandalizi yanafanyika ili mpango huu wa awamu ya tatu uenee nchi nzima kwa kulenga kutolewa mafunzo kwa wananchi pamoja na kuelekezwa vizuri kwa nia ya kuondoa mapungufu yaliyojichomoza katika awamu mbili za mwanzo. Rais wa Jamhuri ya Muungano alieleza kwamba Serikali ina matumaini makubwa kwa awamu ya tatu.

0 comments:

Post a Comment