SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, August 9, 2012

BENKI YA KIISLAM YA WATU WA ZANZIBAR PBZ WAFUTURU NA MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL JIJINI DAR ES SALAAM

  Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, akizungumza machache kuhusu kazi na utendaji wa kazi za Benki hiyo ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na malengo yake wakati wa hafla hiyo ya futari  iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa  hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu  pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, jana.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa  hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu  pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, jana.
Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakishiriki kuomba dua ya pamoja  wakati wa hafla hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongazana  na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana, kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo na kufutari pamoja na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh, Abdulla Tarib Abdulla  na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha na  Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments:

Post a Comment