Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akipandisha bendera ya chama nje ya ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula
Pichani ni Mwenyekiti Freeman Mbowe akikata utepe wa kufungua Ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula. Ilikuwa ni baada ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa kutoa hotuba ya ufunguzi na John Mnyika kupandisha bendera ya chama nje ya ofisi hiyo, ikiwa ni ishara ya kupiga hatua katika mapambano ya awamu ya pili.
Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika akitoa 'somo' kwa wanakijiji wa vijiji vya Kata ya Lumesule. Mapema Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika alikaribishwa na kuzungumza na Katibu wa Tawi wa CUF, Bi. Zaituni. Wananchi walimwelewa vyema. Kadi zikauzwa vizuri. Akaacha uongozi wa muda wa tawi lenye wanachama wa 34. Katika Kijiji hicho cha Lumesule,
Mwananchi mmoja kwa jina la Yasin Mohamed alihoji Ya Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika (Kulia)ilikuwaje CHADEMA wakaachia Dkt. Slaa ashindwe urais, wakati alichaguliwa kwa kura nyingi na wananchi na wao wanajua alishinda uchaguzi huo wa mwaka 2010.
Unaweza kuona pia wanawake wakiitikia PEOPLES POWER, nao wakaipiga ya nguvu kweli kweli kuonesha umoja na mshikamano katika Falsafa ya Nguvu ya Umma ya CHADEMA, katika kudai uwajibikaji, kupigania haki, uhuru na mabadiliko ya kweli ya mfumo na utawala nchini. 

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa akizongwa na wananchi wa Kijiji cha Namahinga, Masasi aliokuwa akisalimiana nao.
Opresheni Okoa Kusini katika picha, hapa ilikuwa Masasi Mjini. Waweza kuona katika baadhi ya picha watu walivyopanga mstari kupigania kadi.
Picha na Habari na Kurugenzi ya Habari- CHADEMA




0 comments:
Post a Comment