Siku Chache BaadaYa Chama Cha Wananchi(CUF)Kumtimua Kwenye Chama Mbunge Wake wa Jimbo la Wawi, Pemba, Hamad Rashid Baadhi Ya Wanachama Waanza Kurudisha Kadi.
Mbunge wa Jimbo la Wawi, Pemba, Hamad Rashid Mohamed, akionesha baadhi ya kadi alizodai zimekuwa zikirudishwa na baadhi ya wanachama wanaomuunga mkono kutokana na hatua zake alizozichukua na pia kutokana na kufukuzwa kwenye Chama.
Mbunge wa Jimbo la Wawi, kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohamed, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu kufukuzwa kwao kwenye Chama cha Wananchi (CUF) na hatua wanazozichukua katika suala hilo. Kulia ni mmoja wa wanachama aliofukuzwa nao, Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Doyo Hassan.
Mbunge wa Jimbo la Wawi, kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohamed, akionesha kitabu alichokiandika, kutokana na kile alichodai kuwa ni baadhi ya mambo yaliyokuwa yakikirudisha nyuma Chama chao cha CUF, ambacho baadaye alishutumiwa na uongozi wa juu wa chama chake kwa kukitoa na kukisambaza kwa wanachama. Kulia ni mmoja wa wanachama aliofukuzwa nao, Doyo Hassan.
Picha na Kassim Mbarouk
Credit to H@ki Ngowi.
Picha na Kassim Mbarouk
Credit to H@ki Ngowi.
0 comments:
Post a Comment