SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, January 28, 2011

Mandela aruhusiwa kutoka hospitali
 Bw. Nelson Mandela
Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela ametolewa hospitali ambapo alikaa kwa siku mbili.
Daktari General Vejaynand Ramlakan alisema Bw Mandela, mwenye umri wa miaka 92, ambaye alikuwa na maradhi mbalimbali yaliyo ya kawaida kwa watu wa umri yake anaendelea uzuri.
Makamu wa Rais Kgalema Motlanthe- akitumia jina lake la ukoo la Bw Mandela-alisema "Madiba anaendelea vizuri."
Siku ya Ijumaa Bw Ramlakan alisema Bw Mandela alipata matatizo ya kupumua, lakini alikuwa akiendelea vizuri na atakuwa anapata matibabu akiwa nyumbani.
Alisafiri kutoka Cape Town hadi Johannesburg siku ya Jumatano kwa kile serikali kilichoita uchunguzi wa "kitaalamu".
Hatua hiyo ilichochea wasiwasi upya juu ya afya dhaifu ya kiongozi huyo.
Marafiki na familia walimtembelea licha ya kuwepo kwa usalama wa hali ya juu siku ya Alhamis.
Afisa mwandamizi wa polisi alisema mfululizo wa magari ulikuwepo nyuma ya eneo la kuingilia katika hospitali ya Milpark mjini Johannesburg, yakijiandaa kumchukua Bw Mandela nyumbani kwake Houghton.
Shujaa huyo wa ukombozi wa Afrika Kusini-anayejulikana miongoni mwa Waafrika Kusini kwa jina lake la ukoo, Madiba- tangu ajiuzulu na masuala ya umma mwaka 2004 ameonekana kuwa dhaifu katika mara chache anazoonekana hadharani.

Wednesday, January 26, 2011

Arsenal kucheza fainali Carling Cup
Arsene Wenger anaamini kukua kwa ukomavu wa wachezaji wake, kumewasaidia kugeuza matokeo baada ya kupoteza mchezo wa awali wa nusu fainali ya kombe la Carling Cup na kufainikiwa kuingia fainali kwa kuiondoa Ipswich kwa jumla ya mabao 3-1.
 Arsene Wenger
Katika mchezo wa siku ya Jumanne, Arsenal iliilaza Ipswich mabao 3-0.
Nicklas Bendtner na Laurent Koscielny walifunga mabao mawili ya kwanza katika muda wa dakika tatu kipindi cha pili, kabla nahodha Cesc Fabregas kushindilia msumari wa mwisho kwa bao la tatu na kuihakikishia Arsenal ushindi wa mabao 3-0 nyumbani.
"Mwaka mmoja au miwili iliyopita, tungekuwa na wasiwasi wakati mechi ilivyokuwa ikienda mrama kwa upande wetu," Meneja wa Gunners, Wenger ameiambia BBC.
"Lakini tuliendelea kudhibiti mpira na kucheza mchezo wetu. Tumekomaa katika mechi ngumu kama hiyo."
Arsenal, ambao watakabiliana na ama West Ham au Birmingham katika fainali tarehe 27 mwezi wa Februari, haijashinda kombe tangu mwaka 2005 waliponyakua kombe la FA.
Wenger amebainisha kwamba muelekeo wa kupata kombe ulikuwa mawazoni mwake kila "anaposali" na amekiri kushinda Kombe la Carling itakuwa ni mafanikio makubwa kwao.
Masikini Ghailani afungwa maisha

Mfungwa wa kwanza katika jela ya Guantanamo kushtakiwa kwenye mahakama ya kiraia, Ahmed Ghailani kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya jimbo la Manhattan.
Ghailani alipatikana bila hatia mwaka jana, katika kesi ambayo alishtakiwa kwa mauaji pamoja na mashtaka mengine kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 katika balozi za Marekani mjini Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania.
Jopo la majaji hata hivyo limempata na hatia ya kufanya njama ya kuharibu majengo ya serikali.
Upande wa mashtaka ulijaribu kumshawishi jaji kwamba Ghailani alipaswa kuonewa huruma kwa sababu hakujua kuhusu njama hiyo.
Vile vile walisema kuwa Ghailani aliteswa na CIA baada ya kukamatwa.
Hata hivyo waendesha mashtaka walitaka apewe kifungo cha maisha gerezani huku wakisisitiza kuwa alijua kuhusu njama hiyo.
Akijiandaa kutoa hukumu yake, Lewis A. Kaplan alisema ilikuwa siku ya haki kwa jamii za watu 224 waliofariki kwenye mashambulizi ya bomu ya mwaka wa 1998 pamoja na wale wote waliojeruhiwa.
Kaplan alisema aliridhishwa na ushahidi aliopata kwamba Ghailani alijua kwamba watu wangekufa kutokana na vitendo vyake.
Ghailani alikamatwa nchini Pakistan mwaka 2004.
Alipelekwa kwenye kambi ya siri inayosimamiwa na shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kabla ya kupelekwa Guantanamo Bay, Cuba, mwaka 2006.
Baadaye alihamishwa hadi New York alikoshtakiwa.
Tunisia issues intl arrest warrant for ousted President Ben Ali, says he fled with state money:
President Zine al-Abidine Ben Ali
Protestors stand in front of the Prime Minister's office in Tunis, Tuesday, Jan. 25. 2011 to demand the removal of members of the ousted president's regime still in the government. Many people, bundled up in blankets, slept outside the prime minister's office overnight, in defiance of a curfew initiated in response to unrest that forced President Zine El Abidine Ben Ali to flee Tunisia on Jan. 14
Tunisia - Tunisia has issued an international arrest warrant for ousted autocratic President Zine El Abidine Ben Ali, who fled to Saudi Arabia earlier this month amid violent protests.
Charges against Ben Ali include taking money out of the country illegally, Justice Minister Lazhar Karoui Chebbi said Wednesday. The country is also seeking the arrest of Ben Ali's wife, Leila, as well as other family members.
Ben Ali fled the North African country Jan. 14 after 23 years in power, pushed out by weeks of deadly protests driven by anger over joblessness, corruption and repression.
On Wednesday, the justice minister released figures that underlined the massive scope of the unrest: More than 11,000 prisoners — about a third of the country's prison population — were able to escape amid the chaos, he said.
Chebbi spoke as Tunisian police fired tear gas at hundreds of protesters in Tunis, the capital, who have been pressuring the interim government to get rid of old guard ministers who served under Ben Ali.
The clashes broke out Wednesday in front of the prime minister's office. Acrid clouds of tear gas engulfed hundreds of people, and some demonstrators responded by throwing stones at police.
The state news agency TAP said officials are to announce changes to the interim government later Wednesday. The acting premier must replace five ministers who quit their posts, echoing protesters' concerns.
TAP reported there will be other changes too, but it is unclear whether they will satisfy the crowds who have been protesting every day in Tunis.
The caretaker government includes some former opposition leaders, but many top posts — including prime minister and the ministers of defence, foreign affairs and the interior — were retained by the old guard.
Prime Minister Mohamed Ghannouchi, who took that post in 1999 under Ben Ali and has kept it through the upheaval, has vowed to quit politics after elections in the coming months. But he has insisted that he needs to stay on for now to guide Tunisia through a transition to democracy.
Tunisia's so-called "Jasmine Revolution" has sparked scattered protests and civil disobedience in the Middle East and North Africa.
In Egypt on Tuesday, thousands of anti-government protesters, some hurling rocks, clashed with riot police in Cairo in a Tunisia-inspired demonstration to demand the end of President Hosni Mubarak's nearly 30 years in power.

Saturday, January 22, 2011

Waziri Mkuu wa Tunisia kustaafu Siasa
Waziri Mkuu wa Tunisia, Mohammed Ghannouchi
Waziri Mkuu wa Tunisia, Mohammed Ghannouchi, amesema atastaafu shughuli za kisiasa haraka iwezekanavyo baada ya mhula wa mpito kumalizika na Tunisia kurejea katika mfumo rasmi wa kidemokrasia.
Katika mahojiano na televisheni ya Tunisia siku ya Ijumaa, Bw Ghannouchi pia aliahidi sheria zote zisizoambatana na demokrasia nchini humo, zitafutwa katika kipindi hiki cha mpito.
Siku chache zilizopita, waandamanaji nchini Tunisia wamekuwa wakidai kuondoka kwa viongozi wote wa serikali ya zamani waliobaki madarakani.
Nayo serikali ya mpito nchini humo imesema imewaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa waliotiwa mbaroni wakati wa utawala wa Rais aliyetimuliwa, Zine El-Abidine Ben Ali.
Wakati huo huo vikosi vya usalama nchini Tunisia, vimejiunga na waandamanaji, katika mji mkuu Tunis.
Wamesema wao ni sehemu ya watu kama walivyo wengine, na ni waathirika wa madhila kutoka kwa utawala wa zamani wa Rais ben Ali kama walivyo Watunisia wa kawaida.
Hatua hii inaonekana ni maendeleo makubwa kufuatia wiki tano za harakati zilizomng'oa Rais Zine el-Abidine Ben Ali aliyeikimbia nchi wiki moja iliyopita.
Maafisa wa polisi binafsi, wameiambia BBC, wanataka serikali ya mpito ijiuzulu kwa sababu imetawaliwa na viongozi waliokuwa katika utawala uliopita.
Duvalier asema amerejea kuijenga Haiti
Jean Claude "Baby Doc" Duvalier
Aliyewahi kuwa Rais wa Haiti, Jean Claude "Baby Doc" Duvalier, amesema kurejea kwake ghafla nchini humo baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka 25, ni kwa sababu anataka kusaidia kuijenga upya nchi yake.
Katika taarifa yake kamili tangu arejee siku ya Jumapili, pia alionyesha masikitiko yake na huzuni kwa wale ambao wanajiona waliathirika enzi za utawala wake.
Matamsnhi yake yanajitokeza wakati kukiwa na msukosuko wa kisiasa nchini humo, ambao ulisababisha kufutiliwa mbali kwa awamu ya pili ya uchaguzi wa Rais.
Siku ya Ijumaa, Marekani iliwanyang'anya hati za kuingilia nchini mwake maafisa kadhaa wa Haiti, ikiwa ni sehemu ya kuichagiza serikali kumtupa nje ya kinyag'anyiro mgombea inayempendelea katika uchaguzi huo wa marudio.
ASALAM ALAIKUM:
 Inshaallah siku ya Jumapili tarehe 23/01/2011 kutakuwa na DA'AWA baada ya salat maghrib TOLICHOWKI HYDERABAD-INDIA. 
Nyumbani anapoishi ABDILLAH NKYA M/Kiti mtsaafu wa TSAH. Kwa wale ambao hawakujui wafike MOGHAL RESIDENCE halafu wapige Simu namba hii +919963702460
Tunaombwa kuwahi kufika mapema ili tuwahi kumaliza shughuli yetu na pia tuhudhurie sote bila kukosa. Upatapo ujumbe huu wafikishie na wengine ili wapate kuhudhuria.
Kufika kwako ndio mafanikio ya shughuli hii. 
WABILAH TAWFIQ.

Thursday, January 20, 2011

Obama, Hu spar over human rights, hail economic ties:
Chinese President Hu Jintao & President Barack Obama
WASHINGTON 
Chinese President Hu Jintao declared Wednesday that “a lot still needs to be done” to improve his country’s record on human rights, a rare concession that came after President Barack Obama asserted that such rights are “core views” among Americans.
The exchange over human rights was balanced by U.S. delight over newly announced Chinese business deals expected to generate about $45 billion in new export sales for the U.S.
Those agreements were cemented during Wednesday’s summit meeting between the leaders of the world’s two largest economies. Obama said the deals would help create 235,000 U.S. jobs.
“I absolutely believe China’s peaceful rise is good for the world, and it’s good for America,” Obama said, addressing a major concern in Beijing that the United States wants to see China’s growth constrained.
“We just want to make sure that (its) rise occurs in a way that reinforces international norms, international rules, and enhances security and peace as opposed to it being a source of conflict either in the region or around the world,” Obama said.
The two leaders, standing side by side at a joint news conference in the White House, vowed closer cooperation on critical issues ranging from increasing trade to fighting terrorism. But they also stood fast on differences, especially over human rights.
Obama noted that China’s human rights policies were a source of tension between the two governments. The U.S. has called for expanded religious freedoms and for China to release jailed dissidents, including Nobel Peace Prize winner Liu Xiaobo, who was prevented from attending the Dec 10 prize ceremony in the Norwegian capital.
“We have some core views as Americans about the universality of certain rights: freedom of speech, freedom of religion, freedom of assembly,” Obama said.
He said he drove that home forcefully in his discussions with the Chinese leader, but “that doesn’t prevent us from cooperating in these other critical areas.”
Hu at first didn’t respond to an American reporter’s question on human rights differences between the two countries. Pressed about it in a later question, he said technical difficulties in translation had prevented him from hearing the question.
He argued that human rights should be viewed in the context of different national circumstances.
“China is a developing country with a huge population and also a developing country in a crucial stage of reform,” Hu said. China “faces many challenges in social and economic development. A lot still needs to be done in China on human rights.”
Hu said that while China “is willing to engage in dialogue” with the U.S. and other nations on human rights issues, countries must exercise “the principle of noninterference in each other’s internal affairs.”
On another contentious issue, Obama said that the United States continues to believe that China’s currency is undervalued, making Chinese imports cheaper in the United States and other countries and U.S. goods more expensive in China.
“I told President Hu that we welcomed China’s increasing the flexibility of its currency,” Obama said. But, he added, the yuan, also called the renminbi, “remains undervalued, that there needs to be further adjustment in the exchange rate, and that this can be a powerful tool for China boosting domestic demand and lessening the inflationary pressures in their economy.”
In a sign of the growing economic bonds between the two superpowers, Obama also said China was taking significant steps to curtail the theft of intellectual property and expand U.S. investment.
Obama said China had become “one of the top markets for American exports” and that these exports have helped to support a half million U.S. jobs.
U.S. companies have also bristled at China’s “indigenous innovation” policy, which limits Beijing’s purchase of foreign products to those designed in China. The White House said Wednesday that China took steps to ease that policy.
As both countries continue to recover from the global economic crisis — a recovery that began in China well before it did in the U.S. and other developed nations — the United States increasingly sees China as a market for its goods.
“We want to sell you all kinds of stuff,” Obama told Hu. “We want to sell you planes, we want to sell you cars, we want to sell you software.”
Obama welcomed Hu to the White House with full honors and a red-carpet greeting, marking the start of daylong meetings to address trade, security and human rights issues that have been the cause of strains between the two powers.
For all the pomp and ceremony, tensions between the nations were boldly evident. Senate Majority Leader Harry Reid of Nevada, a member of Obama’s party, called Hu “a dictator.”
In the House of Representatives, several members of the Republican-led Foreign Affairs Committee assailed the Chinese government’s record on human rights, military expansion, financial strategy and weapons sales. Several witnesses testifying at a committee hearing Wednesday, among them retired military officers and diplomats, echoed the lawmakers’ harsh take on China.
“When the Cold War ended over two decades ago, many in the West assumed that the threat from communism had been buried with the rubble of the Berlin Wall. However, while America slept, an authoritarian China was on the rise,” Rep Ilena Ros-Lehtinen, R-Fla, chairwoman of the committee, said.
The state visit marked Hu’s first trip to the U.S. since 2006, when his arrival ceremony was marred by protocol blunders and an outburst from a protester from the Falun Gong spiritual sect. No such missteps occurred Wednesday.
The day ended with jazz on the stage and prominent Chinese-Americans in the audience as the Obamas threw a “quintessentially American” state dinner for Hu. What is for dinner at the hottest event in town? Meat and potatoes, washed down with apple pie and ice cream for dessert, of course.
Action film star Jackie Chan was supplying some of the celebrity star power for the A-list guest list. Singer Barbra Streisand turned up at a State Department luncheon for the Chinese president and for the dinner, too.
The dinner’s all-star jazz lineup includes trumpeter Chris Botti, two-time Grammy Award-winning vocalist Dee Dee Bridgewater, jazz icon Herbie Hancock, rising star Lang Lang and four-time Grammy-winning vocalist Dianne Reeves.
Jazz pianist Peter Martin, part of the entertainment lineup, prepped for his appearance by buying formal wear.
“I’m finally a grown-up, graduated from renting to owning,” Martin tweeted, adding that he was “super-excited” about the White House gig.
Regular people who find themselves in a last-minute frenzy before guests arrive can take comfort in knowing that it is the same at the White House: Just hours before the dinner, chair cushions were stacked in the front foyer, and harried staff were shuttling flower arrangements to and fro.
New this state dinner: The 225 guests were spread out among three rooms: the State Dining Room, Blue Room and Red Room, then all shuttled to the East Room for the entertainment. There were big video monitors for the outcasts in the Blue and Red rooms to catch the dinner toasts.
Also new: This is the Obamas’ first state dinner where they’ve opted against bringing in a high-profile guest chef, instead putting White House Executive Chef Cristeta Comerford in charge.
The White House said the all-American theme was selected at the request of the Chinese delegation.
On the menu: d’anjou pear salad with farmstead goat cheese, poached Maine lobster, orange glazed carrots and black trumpet mushrooms, dry aged rib eye with buttermilk crisp onions, double-stuffed potatoes and creamed spinach. Dessert was old-fashioned apple pie with vanilla ice cream.
Obama is known to be an avid eater of pastry chef Bill Yosses’ pies.

Members of Obama’s cabinet with seats at the table include Energy Secretary Steven Chu, Commerce Secretary Gary Locke and Education Secretary Arne Duncan.

There were some high-profile no-shows, including three of the top four leaders from Congress: Republican House Speaker John Boehner, who declined Obama’s past state dinner invitations, Senate Majority Leader Harry Reid, a Democrat, and Sen Mitch McConnell, the Republican leader.

With the Senate out of session, Reid was home in the state of Nevada and McConnell just wrapped up a congressional trip to Afghanistan and Pakistan and had not planned to be in Washington this week, aides said.

House Democratic leader Nancy Pelosi, a Democrat, was the only top congressional leader to accept an invitation. Many in Congress see China as an economic threat to the U.S. Pelosi also has been an outspoken critic of China’s human rights record throughout her career.
At a White House news conference with Obama, Hu dodged the question when asked to comment on the congressional leaders’ absence.
“I think President Obama is certainly in a better position to answer that question,” he said, drawing laughter from journalists and the U.S. and China officials seated in the East Room.
Obama also avoided answering too.
Others on the guest list: Jon Huntsman, the U.S. ambassador to China, state dinner veteran Henry Kissinger, the former secretary of state. Kissinger also was at the State Department for a lunch in Hu’s honor, the same one where Streisand turned up.
ZANZIBAR’S PRESIDENT OFFICIAL POTRAIT
This is the official picture of Dr.Mohamed Ali Shein, the recently elected President of Zanzibar.
TALKING ABOUT BROTHERHOOD… 
Mara kwa mara tumeshawahi kuongelea jinsi ambavyo watoto kutoka familia moja wanavyoweza kuchagua kufanya kazi au ajira zinazoshabihiana.Tumewahi kuongelea wanamuziki kupata watoto ambao nao huja kuwa wanamuziki. Familia ya Mzee Zorro na wanae Banana na Maunda ni mfano mzuri.Tumeshawahi kuongelea wanasiasa kupata watoto ambao huja kurithi “uanasiasa”. Mifano ni mingi ukiwemo wa Rais wetu,JK kuwa na mtoto mwanasiasa(Ridhiwani).
Mara chache tumeongelea watoto wa familia moja,kujishughulisha na jambo moja au mambo yanayokwenda sambamba bila kufuata moja kwa moja walichokuwa wakikifanya wazazi wao.Kwa bahati nzuri,nchini kwetu tunayo mifano kadhaa.Leo ninazo familia mbili au brothers kutoka familia mbili. Vijana wa Mzee Kilosa na kutoka kwa Mzee Michuzi.Nadhani utakubaliana na mimi nikisema kwamba hii ni mifano miwili mizuri ya “brotherhood”.Kupendana na kupeana support ya kila hali.Unayo mifano mingine ya brotherhood au sisterhood ambayo tunaweza kusema ni mifano ya kuigwa? Tutumie nasi tutaiweka hewani. Kwa leo,lemme say Big Up to Kilosa Brothers and Michuzi Brothers!
Kutoka kushoto ni DJ Bon Luv,DJ Mackay na DJ Venture. Hawa ni brothers kutoka familia moja ambao wote ni DJs.They are very good at what they do.
Kutoka kushoto; Muhidin Issa Michuzi, Othman Michuzi na Ahmad Michuzi(MichuziJr). Wakiongozwa na M.Issa Michuzi, hawa wote ni wapiga picha wazuri na pia Bloggers. Mfano mzuri wa picha ni hiyo ya juu ya kina Kilosa ambayo imepigwa na Othman Michuzi.
www.bongocelebrity.com
Zombe kuishitaki serikali:
Bw. Abdallah Mohamed Zombe
HATIMAYE aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Mohamed Zombe, ametangaza rasmi nia yake ya kuishitaki serikali kwa hoja kuwa ilikiuka sheria na Katiba ya nchi wakati ilipomkamata na kumfungulia kesi ya mauaji.
Zombe alikamatwa mwaka 2006 na kufunguliwa kesi ya mauaji ya watu wanne lakini aliishinda serikali katika kesi hiyo.
Uamuzi huo ameutangaza baada ya siku 90 alizotoa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumwomba radhi na kumlipa fidia ya sh bilioni tano kumalizika.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, kamishina huyo wa zamani kupitia kwa wakili wake, Richard Rweyongeza, alikabidhi notisi hiyo ya siku 90 kwa IGP Mwema Septemba 27 mwaka jana, akisisitiza atakwenda mahakamani iwapo masharti hayo ya kuombwa radhi na kulipwa fidia hayatatekelezwa.
Alisema siku tisini hizo zilimalizika rasmi Desemba 25 mwaka jana huku IGP Mwema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiwa hawajamjibu chochote mpaka sasa.
Kwa mujibu wa hati hiyo ambayo gazeti hili linayo nakala yake, Jeshi la Polisi lilikiuka sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 inayotaka kabla ya mtu kukamatwa ni lazima aelezwe anakamatwa kwa sababu gani na akifikishwa kituo cha polisi ni lazima ahojiwe na kuchukuliwa maelezo yake ambayo baadaye hutumika mahakamani kama kielelezo.
Mbali na hilo, Jeshi la Polisi lilikiuka pia haki za msingi za binadamu na Ibara ya 15(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayosomeka kama ifuatavyo:
“Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang’anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-
“(a) Katika hali na kwakufuata utaratibu uliowekwa na sheria.”
Akiongea kwa kujiamini huku akilionyesha gazeti hili hukumu mbalimbali ambazo Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali rufaa zilizokuwa zimekatwa na serikali dhidi ya wananchi walioshinda kesi za mauaji katika mazingira kama aliyoshinda yeye, Zombe alisema serikali kama serikali ni nzuri ila kuna baadhi ya watendaji wana hulka za kinyang’au na hawatimizi wajibu wao kama inavyotakiwa.
“Nafahamu kwamba DPP amekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Massati, ambayo ilituachilia huru mimi na wenzangu tisa….hilo halinitishi.
“Nimewasilisha hati hiyo ya nia ya kutaka kuwashitaki na hawajanijibu, hivyo imeonyesha wazi wapo tayari kwenda mahakamani, na mimi na wakili tupo tayari na muda wowote kuanzia leo tunakwenda Mahakama Kuu kufungua kesi ya kudai sh bilioni tano ikiwa ni fidia ya usumbufu na kunyanyaswa kipindi kile nilipokuwa nakabiliwa na kesi ile ya mauaji.
“Sasa kitendo cha Jeshi la Polisi kunikamata na kunifikisha mahakamani na kwenda kuishi gerezani kwa miaka minne bila kuhojiwa na polisi, je, si ndiyo lilikiuka sheria na Katiba zilizotungwa na Bunge, ambapo na huyu huyu IGP aliapa kuilinda Katiba hiyo?” alihoji huku akionyesha kukerwa na jambo hilo.
Zombe ambaye kwa sasa anafanya shughuli zake zinazomuingizia kipato huko mkoani Morogoro, alisema anataka hilo liwe fundisho kwa Jeshi la Polisi ambalo baadhi ya askari wake wamekuwa wakikiuka taratibu kwa makusudi na kuonea wananchi wasio na hatia.
Agosti 17, mwaka 2009, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitoa hukumu ya kushtusha baada ya kumwachilia huru Zombe na wenzake wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja.
Serikali ilikata rufaa Oktoba 7 mwaka 2009 katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachilia Zombe na wenzake.
Akisoma hukumu, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati, alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, alibaini kuwa serikali ilishindwa kuthibitisha mashitaka na kuwa kamwe mahakama haiwezi kumhukumu mshitakiwa kwa ushahidi dhaifu na wa kusikia kama uliowasilishwa mahakamani hapo, kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria.
Kwamba washitakiwa hao si wauaji na aliliagiza Jeshi la Polisi liwatafute wauaji halisi wa marehemu wale.
Jeshi la Congo 'liliongoza ubakaji'
Wanajeshi wa Congo
Kamanda wa jeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameshutumiwa kwa kuongoza ubakaji wa wanawake takriban 50 uliofanyika hivi karibuni.
Mmoja wa waliobakwa, pamoja na vyanzo vilivyonukuliwa katika ripoti ya umoja wa mataifa, wote wanamshutumu Lt Col Kibibi Mutware kwa kuhusika na ubakaji huo uliofanyika mwaka mpya mjini Fizi.
Kumekuwa na ripoti nyingi za ubakaji huko Congo lakini tukio hili linaaminiwa kuwa la kwanza kwa idadi kubwa ya wanawake kubakwa likihusishwa jeshi.
Lt Col Kibibi amekana tuhuma hizo.
Alisema wanajeshi waliovamia eneo hilo walikiuka amri.
Kutokana na ugomvi baina ya wanaume wawili waliokuwa wakimgombea mwanamke, ghasia hizo zikazidi ambapo jeshi la serikali likaanza kuwaadhibu watu wa Fizi.
'Aibu'
Dr Faise Chacha, mkuu wa hospitali ya Fizi ameeleza, " Askari mmoja aliuawa hapa karibu kabisa na hospitali hii."
"Hiyo ilisababisha wasiwasi na wagonjwa wetu wote wakakimbia. Tulirudi siku ya pili asubuhi na tukaanza kuwapokea watu waliokuwa wamepigwa kisu na wengine- wanawake- waliobakwa."
Dr Chacha na shirika la kitabibu la kutoa msaada Medecins Sans Frontieres wamewatibu waathirika 51 waliobakwa mpaka sasa.
Kama ilivyo kwa matukio ya awali huko Congo, wengi wanatarajiwa kuficha yaliyowasibu kuepuka kuachwa na waume na familia zao.
Wawili miongoni mwa wanawake hao walikubali kuzungumza na BBC ilimradi tu wasitajwe majina yao.
Mmoja aliiambia BBC, " Nilibakwa mbele ya watoto wangu wanne."
"Ninaona aibu, ninaona aibu sana. Nikikutana na watu wawili au watatu ambao wanajadili jambo, naanza kuhisi tu kuwa wananizungumzia mimi, hata kama si kuhusu mie."
Mwanamke huyo mwengine alifanikiwa kumtambua aliyembaka.
"Ilikuwa jioni na walionibaka walikuwa wanajeshi," alisema kwa sauti ndogo, mwili wake ukiwa umefunikwa na khanga yenye rangi za kuvutia.
" Walikuwa wanne- Kibibi na walinzi wake. Wameiba vitu vyetu vyote pamoja na pesa."
SITTA: HAKUNA WA KUNIFUNGA MDOMO:
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (pichani), amekoleza moto wa sakata la kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans, akisema kamwe hawezi kufungwa mdomo kupinga malipo ya Sh94 bilioni kwa kampuni hiyo.
Kauli ya Sitta imekuwa wakati kukiwa na taarifa kwamba waziri huyo pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe wamebanwa na Ikulu wakitakiwa wasizungumzie tena suala hilo.
Hata hivyo, akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana Sitta alisema, "Naomba wananchi wafahamu, siwezi kufungwa mdomo kuhusu kupinga malipo kwa kampuni ya kitapeli ya Dowans."
Sitta ambaye msimamo wake umeibua mjadala mzito nchini na hata ndani ya baraza la mawaziri, alisema hajawahi kutishwa wala kufungwa mdomo kuhusu msimamo wake.
Kauli hiyo ya Sitta imekuja siku moja tangu gazeti moja la kila siku (siyo Mwananchi) kuripoti kwamba Rais Jakaya Kikwete amemfunga mdomo, uamuzi uliodaiwa kufikiwa juzi katika kikao cha Baraza la Mawaziri, kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Habari hizo zilidai kuwa Sitta na Dk Mwakyembe walikuwa na wakati mgumu kutetea hoja ya kutaka Serikali isiilipe Dowans na kwamba hata Rais alisema hafurahishwi na hukumu ya malipo hayo, hivyo kikao hicho kuwaamuru mawaziri hao kutozungumzia tena suala hilo hadharani.
Lakini jana Sitta alisema: "Nitaendelea kupinga malipo ya Dowans. Sijawahi kuitwa popote wala na mtu yeyote na kuambiwa nisizungumze suala hilo, hivyo wananchi wasifikiri nimebadili msimamo".
Aliongeza: "Taarifa zinazosambaa ni za kupikwa tu, zisije zikawapotosha wananchi wakidhani nimewasaliti katika hili, narudia tena sijafungwa mdomo."
Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye aliliongoza Bunge la Tisa katika vita dhidi ya ufisadi, alifafanua kwamba si suala la Dowans tu bali ataendelea kupinga mambo yote machafu kuhusu nchi.
Aliweka bayana kwamba nchi inahitaji viongozi wenye uwezo wa kusimamia vema maslahi ya taifa bila hofu ili kulinda haki za wananchi na kuboresha maisha yao.
Sitta alinukuliwa akihoji kile kinachoitwa kukiuka dhana ya uwajibakaji wa pamoja na kuweka bayana, kama dhana hiyo ingekuwa inaheshimika basi uamuzi wa kuilipa au kutoilipa Dowans ungefanywa kwa pamoja.
Alisema haiwezekani dhana ya uwajibikaji wa pamoja ifanyike bila kushirikisha wengine halafu mwisho itolewe taarifa ya uwajibakaji wa pamoja.
"Halafu kuna watu wanazungumzia nimekiuka dhana ya uwajibikaji wa pamoja, uwajibikaji wa pamoja ni lazima uamuzi ushirikishe wengine si mmoja kuamua halafu ifahamike ni uwajibakaji wa pamoja," aliongeza.
Sitta pia amekuwa akihoji kasi ya malipo hayo kwa kampuni ya Dowans wakati nchi ina madeni mengine kama ya Benki ya Dunia na IMF, lakini bado hayajalipwa kwa kasi kama hiyo.
"Lakini, hii haraka ya kuilipa Dowans ni ya nini?  Nchi hii ina madeni ya muda mrefu kama yale ya Benki ya Dunia na IMF, lakini hakuna uharaka wa kulipa kama huu sasa kasi hii inatoka wapi?" alihoji.
Alisema nchi ina matatizo mengi ikiwemo ya kiuchumi, hivyo haingii akilini kuona Watanzania wanalipa kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kampuni ya kitapeli.
Tayari msimamo wa Sitta ulimfanya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, kutoa vitisho kwa mawaziri wenzake akiwataka wakae kimya na kuacha kuzungumzia sakata hilo vinginevyo wajiondoe kwenye Serikali.
Hata hivyo, wakosoaji wamemwelezea Chikawe kama ambaye pia amekiuka taratibu kutokana na kuzungumza suala hilo kwenye vyombo vya habari, badala ya taratibu za kiserikali.
Tangu Mahakama ya Usuluhishi ya Biashara ya kimataifa (ICC Court) kutoa hukumu ya mwezi Novemba, ikitaka Tanesco ilipe Dowans, Sitta alikuwa waziri wa kwanza kupinga malipo hayo hadharani.
Hata hivyo, pamoja na Sitta kupinga, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alikwisha kusema bayana kwamba Serikali haiwezi kukata rufani katika sakata hilo, lazima ilipe faini hiyo.
      CHANZO: MWANANCHI

Saturday, January 15, 2011

Rais wa Tunisia ajiuzulu
Waziri mkuu wa Tunisia Mohammed Ghannouchi ameonekana kwenye televisheni ya taifa kutangaza kuwa Rais Ben Ali amemkabidhi madaraka kwa muda.
Bw Ghannouchi alisema Rais Ben Ali hakuweza kutimiza wajibu wake kwa muda.
Kwa sasa haijulikani Rais Ben Ali alipo.
Hali ya hatari imetangazwa nchini Tunisia huku maandamano yakiendelea kuhusu ukosefu wa ajira na mfumko wa bei.
Kwa sasa hairuhusiwi zaidi ya watu watatu kukutana hadharani.
Wakati huo huo Rais Zine al-Abidine Ben Ali amevunja serikali yake na kutangaza uchaguzi kufanyika katika kipindi cha miezi sita.
Maelfu ya watu wamekusanyika kwenye mji mkuu wa Tunis wakimtaka rais kujiuzulu.
Alhamisi usiku, Ben Ali, ambaye ameiongoza Tunisia tangu 1987, alitangaza kuondoka madarakani mwaka wa 2014 - lakini waandamanaji wanataka aondoke sasa.
Polisi waliwafyatulia mabomu ya machozi waandamanaji nje ya wizara ya mambo ya ndani.
Madaktari wamethibitisha kuwa watu 13 waliuawa wakati wa makabiliano usiku kwenye mji mkuu na kuna taarifa zinazosema kuwa watu watano wameuawa katika maandamano ya siku ya Ijumaa.
Makundi ya kutetea haki za binadamu wanasema zaidi ya watu 60 wameuawa kwenye ghasia tangu zianze.

Friday, January 14, 2011

Rais Jakaya Kikwete Apokea Ujumbe Maalum Kutoka Kwa Rais Mwai Kibaki
Mjumbe maalum wa Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Mhe.Robinson Njeru Githae akimkabidhi RaisDr.Jakaya Mrisho Kikwete ujumbe kutoka kwa Rais Kibaki ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Bwana Githae ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya jiji la Nairobi aliambatana na maofisa waandamizi kutoka ubalozi wa Kenya nchini Tanzania. Picha na Freddy Maro-Ikulu

WASANII WAFURAHIA TUZO ZA FC
WASANII mahiri katika tasnia ya filamu hapa nchini Tanzania leo hii asubuhi wameonyesha furaha kubwa baada ya kupokea tuzo hizo za Bora za 2010 zilizofanyika katika ukumbi wa Tamal Hotel uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam, wakiongea kwa nyakati tofauti wasanii hao wameupongeza mtanda huu kwa kuwajali na kuwapa moyo kwa kazi wanazofanya na kupokelewa na jamii.

“Napenda sana kuwapongeza sana filamucentral.co.tz kwa kuonyesha moyo wa kuwajali wasanii, lakini kwangu ni deni kwa mwaka huu wa 2011, mara nyingi watu wakipata tuzo huwa ndiyo wakati wa kubweteka, kwangu nisingependa iwe hivyo nahitaji kufanya kazi zaidi ili niwe mshindi tena kwangu ni heshima kubwa sana, nasema asante” Amesema Ali Yakuti mshindi wa uandishi wa mswaada.

“Tunawashukru waandaaji wa tuzo hizi kwa kweli mwaka huu umekuwa mzuri kwangu pamoja na kampuni yangu, tunawashukru sana tena na tena mtandao huu wa filamucentral.co.tz kwa kutukumbuka na kutujali”
Kanumba akiwa na tuzo zake alizoshinda.


Kiongozi wa Nigeria apata changamoto
Rais Goodluck Jonathan
 Atiku Abubakar.
Chama tawala Nigeria kinatarajiwa kuchagua mgombea wake katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Aprili.
Changamoto kubwa anayotarajiwa kukabiliana nayo Rais Goodluck Jonathan ni kutoka kwa aliyekuwa makamu wa Rais Atiku Abubakar.
Mgombea wa PDP ameshinda kila uchaguzi tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999, kwahiyo mgombea wake anatarajiwa kuungwa mkono zaidi.
Lakini baadhi ya wachambuzi wanasema PDP kinaweza kugawanyika kutokana na kura za watu wa kusini zinazomwuunga mkono Bw Jonathan na Bw Abubakar anayeungwa mkono na upande wa kaskazini.
PDP kina desturi ya kubadilishana uongozi baina ya kaskazini na kusini baada ya kukaa madarakani kwa mihula miwili lakini hii ilivurugwa baada ya Bw Jonathan, kutoka kusini, kumrithi Umaru Yar'Adua alipofariki mwaka jana.
Kuna ulinzi wa hali ya juu katika mji mkuu, Abuja, ambapo upigaji wa kura hizo unapofanyika, kufuatia mashambulio ya mabomu ya hivi karibuni.

Thursday, January 13, 2011

Child mauled to death, police ‘arrests’ dog
Bangalore: An 18-month-old child was killed by street dogs in the wee hours of Wednesday.
Around 5am, a snarling pack of 15 stray dogs dragged the sleeping 18-month-old S Prashanto out of his hut and mauled him to death near Bagalur off the Bangalore International Airport road, TOI reported.
    Police arrested Gonti Yadav alias Chandrasen, around whom the stray dogs live, and charged him under IPC sections 289 and 304 (A), which deal with negligence towards animals. Police also caught one of the stray dogs which mauled the baby. “We’ll hand it over to BBMP officials” said inspector Babu Anjinappa.
And I wonder what the officials will ‘officially’ do with the canine — banish it to a lifeterm in prison or hang it till death?
Although the authorities are keen to terminate the menace of canines and clear the streets of them, animal rights groups oppose any such move. I wonder why.
I don’t know how to avoid such incidents or induce social responsibility, but after reading such a story for the umpteenth time, I just wanted to ask one question to those animal lovers who stop the government from taking any measure — Whose life is more important for you? A street dog’s or your child’s?
PS: A billboard near Chinnaswami Stadium reads: “Save your children from stray dogs”. Is that all we can expect from the authorities? 
***HAPPY BIRTHDAY *** 
MOHAMAD FATH ALRAHMAN
LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA KAKA MOHAMAD FAH ALRAHMAN(aka FATH 7) HYDERABAD (MEHDI-PATNAM) INDIA.
BLOG HII INAUNGANA NA FAMILIA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KUKUTAKIA KILA LA HERI KATIKA SIKU YAKO HII YA KUZALIWA.
ALLAH AKUJAALIE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU,BUSARA NA HEKIMA  KATIKA MAISHA YAKO.

ballon poem
HAPPY BIRTHDAY TO YOU.
************
Wachezaji wawili wa Man City kuondoka
Roque Santa Cruz
Shaun Wright-Phillips
 Meneja wa Manchester City Roberto Mancini, amethibitisha Roque Santa Cruzna Shaun Wright-Phillips huenda wakaondoka katika klabu hiyo siku chache zijazo.

Santa Cruz mshambuliaji wa kimataifa wa Paraguay, kuna kila dalili akajiunga na klabu yake ya zamani ya Blackburn.

Nae Wright-Phillips, mshambuliaji wa pembeni, amehusishwa kujiunga na klabu za Fulham, Birmingham na West Ham.

Mancini amesema kwa sasa anasita kumruhusu Emmanuel Adebayor, kuondoka katika klabu hiyo hadi atakapofahamu iwapo Mario Balotelli atahitaji kufanyiwa upasuaji wa goti.Santa Cruz na Wright-Phillips wote walisajiliwa na meneja wa zamani wa Manchester City, Mark Hughes, lakini hawakuwa na bahati ya kucheza wakati alipoingia Mancini.Wright-Phillips huenda anaunganishwa tena na Hughes katika klabu ya Fulham, lakini Santa Cruz anataka kubakia maeneo ya kaskazini magharibi, ambako familia yake inaishi.

Mshambuliaji huyo wa Paraguay wakati akiichezea klabu ya Blackburn msimu wa mwaka 2007-08, alifunga mabao 23, kabla hajajiunga na Manchester City mwaka 2009 kwa kitita cha paundi milioni 17.5.Akiwa amekabiliwa na maumivu, alianza kucheza mechi nane na City, huku menchi nyingine 16 akiwa mchezaji wa akiba.
TAMKO LA CHADEMA WAKATI WA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU UWANJA WA NMC ARUSHA
UTANGULIZI
Tumekutana hapa leo hii kwa huzuni kubwa. Tumekutana hapa leo hii kwa sababu watoto wa familia mbili wamepoteza baba zao na mama wa familia hizo wamepoteza waume na wenzi wao wa maisha.
Tumekutana hapa leo kwa sababu wazazi wa familia mbili wamepotelewa na watoto wao wa kiume. Tumekutana hapa leo kwa sababu kuna familia nyingine – kwa sababu taarifa zetu za awali zinaonyesha watu wengine zaidi wameuawa – zimepotelewa na wapendwa wao vile vile.
Tumekutana hapa leo kwa sababu mamia ya wananchi wa Jiji hili wameumizwa kwa kupigwa risasi za moto, kupigwa mabomu ya machozi na/au kupigwa kwa virungu na mabuti ya Jeshi la Polisi la Tanzania.
Tumekutana hapa leo kwa sababu wote waliokufa na tunaowaomboleza leo nawote walioumizwa na/au kuharibiwa mali zao hawakufikwa na mauti na/au majanga hayo kwa ajali ya barabarani au tetemeko la ardhi. Tumekutana hapa kwa sababu wote waliofikwa na mauti wameuawa na wote walioumia wameumizwa na Jeshi la Polisi la Tanzania.
Tumekutana hapa leo kwa sababu Jeshi la Polisi la Tanzania halipaswi, na halikupaswa, kuua wananchi wasiokuwa na hatia yoyote na ambao walikuwa wanatumia haki yao ya kufanya maandamano ya amani inayotambuliwa na Katiba na sheria za nchi yetu. Na tumekutana hapa leo ili kulinda na kutetea haki hiyo na kuzuia nchi yetu kuwa dola ya kipolisi inayoendeshwa kwa amri za kijeshi na za watawala na sio kwa matakwa ya wananchi.
Lakini, ndugu wananchi wa Arusha, tumekutana hapa ili kuomboleza kwa pamojana tunahitaji kuomboleza kwa amani. Kwenye msiba watu hawapigani na tunawaomba tusipigane kwenye msiba huu. Kwenye msiba watu hawafanyi fujo na tunawaomba tusifanye fujo kwenye msiba huu. Tunawaomba tuomboleze kwa amani ili tusiwape wale walioua ndugu zetu sababu ya kusema kwamba sisi tunapenda fujo na uvunjifu wa amani.
SIKU YA KIHISTORIA
Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo haitasahaulika katika historia ya Jiji la Arusha. Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo haitasahaulika katika historia ya Tanzania.
Ni siku ambayo Jeshi la Polisi la Tanzania – ambalo limepewa wajibu wa kisheria wa ‘kulinda amani, sheria na utulivu, kugundua na kuzuia uhalifu, kukamata na kudhibiti wahalifu na kulinda mali za wananchi – liliamua kwa makusudi kuacha kutimiza wajibu wake kisheria na kujipa wajibu mwingine wa kuwa ni Jeshi la kuvunja amani, kukiuka sheria, kuvuruga utulivu, kufanya uhalifu na kuharibu mali za wananchi.
Ni siku ambayo Jeshi la Polisi la Tanzania – ambalo limejipachika kauli mbiu ya ‘Ulinzi wa Raia na Mali Zao’ – liliamua kwa makusudi kubadili kauli mbiu yake kuwa ni ‘Mauaji ya Raia na uharibifu wa mali zao’!
Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo wananchi wa Jiji la Arusha walivamiwa kwa
makusudi, waliuawa kikatili na kupigwa na kuumizwa bila kosa au sababu yoyoteya msingi.
Ni siku ambayo Jeshi la Polisi la Tanzania lilitumia silaha kubwa kubwa – risasi za moto, mabomu ya machozi na magari ya maji ya kuwasha – dhidi ya raia waliokuwa na vitambaa vyeupe vyenye kuashiria amani.
Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo – kama ilivyokuwa tarehe 26 na 27 Januari 2001 – Jeshi la Polisi la Tanzania lilitukumbusha tena kwamba liko tayari kumwaga damu ya Watanzania wasiokuwa na hatia ili kulinda wizi wa kura na unyongaji wa demokrasia unaofanywa na watawala wa Chama cha Mapinduzi.
Kama ilivyokuwa Zanzibar miaka kumi iliyopita ndivyo ambavyo imekuwa Arusha mwaka huu: tumeanza Mwaka Mpya kwa umwagaji wa damu na maombolezo badala ya sherehe na kutakiana heri! Hata hivyo, tofauti na ilivyokuwa Zanzibar baada ya mauaji ya Januari 2001, CHADEMA haitakubali kununuliwa au kunyamazishwa kwa kuvikwa vilemba vya ukoka na/au kupewa vipande thelathini vya fedha ili kunyamazia mauaji ya wananchi wetu: Mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia hayatazuia jitihada za kujikomboa kutoka kwenye makucha ya utawala wa CCM.
Mti wa haki uliorutubishwa kwa damu isiyokuwa na hatia ya wananchi wa Arusha utaendelea kukua na kuenea Tanzania nzima. Tarehe 5 Januari 2011 itakuwa siku itakayokumbukwa katika historia ya nchi yetu kama ni siku ambayo jitihada za ukombozi wa nchi yetu zilipata msukumo mkubwa.
MAANDAMANO HALALI
Jeshi la Polisi lilijua kwamba kutakuwa na maandamano ya amani ambayo yangefuatiwa na mkutano wa hadhara. Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linafahamu njia na/au barabara za Jiji la Arusha ambazo maandano hayo ya amani yangepitia hadi kufika kwenye eneo la Viwanja vya NMC ambako mkutano wa hadhara ungefanyika. Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linafahamu muda wa kuanza maandamano hayo ya amani na muda wa kumalizika kwa mkutano wa hadhara.
Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linafahamu yote hayo sio kwa sababu ya ‘taarifa za kiintelijensia’ ambayo ndio imekuwa kisingizio cha Jeshi la Polisi la Tanzania kukanyaga haki za kikatiba za wananchi wa Tanzania kupinga serikali ya CCM kwa njia za amani kwa kufanya maandamano na mikutano ya hadhara.
Jeshi la Polisi la Tanzania lilifahamu yote hayo kwa sababu Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilifuata taratibu zote za kisheria za kufanya maandamano na mikutano ya hadhara.
Tarehe 3 Januari 2011 CHADEMA ilitoa taarifa ya maandishi kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha kuhusu nia yake ya kufanya maandano ya amani yatakayofuatiwa na mkutano wa hadhara ili kupinga kitendo cha watawala wa CCM kuwalazimishia wananchi wa Jiji la Arusha Meya ya Jiji kwa njia za kiharamia.
Tarehe hiyo hiyo Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha alifanya kikao na viongozi wa CHADEMA kwa lengo la kukubaliana njia na/au barabara zitakazotumiwa na waandamanaji hadi kufikia Viwanja vya NMC.
Baada ya hapo, pamoja na kwamba hakuwa na haja ya kisheria ya kufanya hivyo, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha aliifahamisha CHADEMA kwa maandishi kwamba maandamano yetu ya amani na mkutano wa hadhara yalikuwa yameruhusiwa na Jeshi la Polisi la Tanzania.
Hatua zote tulizozichukua na ambazo tumezitaja hapa zilifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi na vile vile kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Lakini hata kabla ya hapo, Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linajua kwamba CHADEMA ingefanya maandamano ya amani kushinikiza utekelezaji wa madai yetu tuliyoyatoa kwa maandishi kwa serikali na nakala yake kupatiwa Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema mnamo tarehe 23 Desemba 2010.
Katika barua yake, CHADEMA ilidai kwamba uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ufutwe na kurudiwa; Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Jiji afukuzwe kazi kwa kushiriki katika ukiukwaji wa sheria za uchaguzi wa viongozi wa halmashauri za serikali za mitaa; na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha avuliwe madaraka yake kwa kushiriki kumpiga Mbunge wetu wa Jimbo la Arusha Mjini aliyekuwa anajaribu kutetea sheria za nchi yetu za uchaguzi wa viongozi wa halmashauri za serikali za mitaa.
CHADEMA ilitoa nafasi ya wiki mbili kwa serikali kutekeleza madai hayo la sivyo ingeandaa maandamano ya amani ya wananchi wa Arusha. Ni wazi, kwa hiyo, kwamba CHADEMA haikukimbilia kuandaa maandamano hata kama haikuwa kosa dhidi ya sheria za Tanzania kufanya hivyo.
Kabla ya matukio ya maandamano ya tarehe 5 Januari, CHADEMA ilishaweka wazi utayari wake wa kumaliza mgogoro wa Arusha kwa njia za mazungumzo. Barua yetu ya tarehe 23 Desemba 2010 kwa serikali na kwa Jeshi la Polisi la Tanzania haijajibiwa hadi leo hii!
JESHI LA WAHALIFU!
Baada ya taarifa ya maandamano na mkutano wa hadhara wa CHADEMA kutolewa kwa mujibu wa sheria zilizotajwa, njia pekee halali ya kusitisha maandamano na mkutano uliopangwa ilikuwa ni kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha kutoa amri ya kusitisha maandamano na mkutano huo.
Na Sheria ya Jeshi la Polisi inasema wazi kwamba Ofisa wa Polisi aliyepewa taarifa ya maandamano au mkutano hatatoa amri ya kuzuia au kusitisha maandamano au mkutano huo ‘isipokuwa tu kama amejiridhisha kwamba maandamano au mkutano huo unaweza kusababisha uvunjifu wa amani au kuhatarisha usalama na/au utulivu wa umma au kutumiwa kwa malengo haramu.’
Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, chama cha siasa kikishatoa taarifa ya mkutano kinaruhusiwa kufanya mkutano huo isipokuwa tu na kama kitapokea amri kutoka kwa ofisa wa polisi mwenye mamlaka ya eneo husika ikielekeza kwamba mkutano huo usifanyike kama ilivyopangwa.
Na chini ya sheria hii vile vile, ofisa wa polisi aliyepewa taarifa ya mkutano haruhusiwi kutoa amri ya kuzuia au kusitisha maandamano au mkutano huo mpaka atakapojiridhisha kwamba mkutano au maandamano hayo yana lengo la kutekeleza au kutumiwa kwa malengo haramu; au kama maandamano au mkutano huo unaweza au umelenga kusababisha uvunjifu wa amani au kuhatarisha usalama na/au utulivu wa umma katika eneo husika. Kwa vyovyote vile kwa mujibu wa sheria hizi mbili, amri ya kuzuia na/au kusitisha maandamano au mkutano wa hadhara uliotolewa taarifa ni lazima iwe ni ya maandishi.
Na hata kama ‘taarifa za kiintelijensia’ alizozisema Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema zilikuwa na ukweli
kwamba kulikuwa na uwezekano wa uvunjifu wa amani iwapo maandamano na mkutano wa hadhara wa CHADEMA ungeendelea kama ilivyokuwa imepangwa – bado Jeshi la Polisi la Tanzania lisingepaswa kutoa amri ya kuzuia na/au kusitisha maandamano na mkutano wa hadhara wa CHADEMA.
Hii ni kwa sababu, kuzuia na/au kusitisha maandamano sio hatua pekee inayoweza kuchukuliwa na Jeshi la Polisi la Tanzania. Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, kila chama ambacho kimesajiliwa ‘kina haki ya kupatiwa ulinzi na msaada wa vyombo vya ulinzi kwa malengo ya kuwezesha mikutano yenye amani na utulivu.’
Jeshi la Polisi la Tanzania lilikiuka kwa makusudi masharti haya ya sheria. Kwanza, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha ambaye ndiye ofisa anayetakiwa kupatiwa taarifa ya maandamano na mkutano wa hadhara hakuwahi kuipa CHADEMA taarifa yoyote ya maandishi ya kuzuia na/au kusitisha maandamano na mkutano wa hadhara uliotolewa taarifa rasmi kwake kwa mujibu wa sheria.
Taarifa na/au amri pekee tunayoisikia ya kuzuia na/au kusitisha maandamano ni ile inayosemekana ilitolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha jioni ya tarehe 4 Januari 2011.
Taarifa na/au amri hiyo – kama kweli ilikuwepo – ilikuwa ni haramu kwa sababu Kamanda wa Polisi wa Mkoa hana mamlaka yoyote ya kuruhusu au kukataza maandamano na/au mikutano ya vyama vya siasa. Mtu pekee mwenye mamlaka hayo chini ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa ni ‘ofisa polisi mwenye mamlaka ya eneo’ la mkutano, kwa maana nyingine, Mkuu wa Polisi wa Wilaya!
Aidha, tuna taarifa kwamba Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema alitangaza kwenye vyombo vya habari
kwamba maandamano na mkutano wa hadhara wa CHADEMA yamepigwa marufuku kutokana na kuwepo kwa ‘taarifa za kiintelijensia’ kwamba kutakuwa na uvunjifu wa amani wakati wa maandamano na/au mkutano huo wa hadhara.
Tangazo hilo la Inspekta Jenerali wa Polisi lilikuwa haramu na ni ukiukaji wa makusudi wa Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa kwa sababu Inspekta Jenerali wa Polisi hana mamlaka yoyote kisheria ya kuzuia au kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Vile vile utaratibu wa kutoa amri za kuzuia ama kusitisha maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa kwa kutumia matangazo ya televisheni na/au waandishi wa habari ni utaratibu mgeni katika nchi ya Tanzania na hautambuliwi kabisa na sheria hizo!
Lakini hata kama maandamano na mkutano wetu wa hadhara yangekuwa yamepigwa marufuku kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa – kitu ambacho hakikufanyika – bado CHADEMA ilikuwa na uhalali wa kuendelea na maandamano hayo na kufanya mkutano kama ilivyopangwa.
Hii ni kwa sababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kulinda uhuru wa wananchi ‘kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani….’
Hii ina maana kwamba uhuru wa kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara umepanuliwa sana na hauwezi kupokonywa kihalali kwa visingizio vya ‘taarifa za kiintelijensia’ vya Jeshi la Polisi la Tanzania.
Kwa hiyo wananchi wa Arusha walivamiwa na kupigwa risasi zilizowaua au kuwajeruhi sio kwa sababu walikuwa wamevunja sheria yoyote ya Tanzania. Walivamiwa na kuuawa au kujeruhiwa na mali zao kuharibiwa sio kwa sababu walifanya kosa lolote linalotambuliwa na sheria za nchi yetu.
Viongozi wa CHADEMA kuanzia ngazi za juu za kitaifa hadi ngazi za chini na wanachama wetu wa kawaida walishambuliwa kwa risasi na mabomu na baadaye kujazwa kwenye mahabusu za polisi sio kwa sababu walikiuka sheria yoyote. Wananchi wa Arusha walifanyiwa uhalifu wote huo licha ya kwamba Katiba ya nchi yetu inatambua na kulinda uhuru wa wananchi wa kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara.
MAUAJI YA KUPANGWA
Mauaji ya Arusha yalifanywa kwa makusudi na kwa kupangwa. Jeshi la Polisi la Tanzania lilipanga na kutekeleza mauaji hayo. Lakini sio Jeshi la Polisi la Tanzania pekee lenye kuhusika na mauaji ya wananchi wetu. Rais Kikwete na serikali yake na chama chake cha CCM wanahusika moja kwa moja na damu iliyomwagwa kwa makusudi Arusha. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.
Aidha, chini ya Sheria ya Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi – ambaye ni mteuliwa wa Rais – anawajibika kufuata amri na maelekezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani – mteuliwa mwingine wa Rais – kuhusiana na udhibiti wa shughuli za Jeshi la Polisi. Kwa hiyo, kikatiba na kisheria, Jeshi la Polisi liko chini ya mamlaka ya Rais na wateuliwa wake kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Inspekta Jenerali wa Polisi.
Pamoja na mamlaka ya Rais juu ya Jeshi la Polisi, Kikwete mwenyewe alikwishatoa kauli na matamko hadharani ambayo yaliashiria kwamba Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linajiandaa kumwaga damu ya Watanzania ili kulinda utawala wake na wa chama chake.
Kwa mfano, katika hotuba yake ya Mwaka Mpya aliyoitoa usiku wa tarehe 31 Desemba 2010, Kikwete alidai kwamba ‘… wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa … wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara…. Wao hasa wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya dola kuingilia ati waiambie jumuiya ya kimataifa jinsi Serikali yetu ilivyo katili.’
Katiba hotuba hiyo, Kikwete alizungumzia kile alichokiita wananchi ‘kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara’! Rais aliyasema hayo wiki moja baada ya barua yetu kwa serikali yake juu ya nia ya CHADEMA kufanya maandamano ya amani iwapo serikali yake isingechukua hatua tulizodai zichukuliwe katika barua yetu ya tarehe 23 Desemba 2010. Haikupita hata wiki moja tangu Kikwete atoe kauli yake hiyo na Jeshi la Polisi la Tanzania limemwaga damu ya Watanzania Arusha.
Jeshi la Polisi la Tanzania limetekeleza maagizo ya Amiri Jeshi wake mkuu, ndio maana Amiri Jeshi Mkuu huyo hajatoa kauli yoyote kwa Watanzania kuhusiana na matukio haya ya kusikitisha na wala kuchukua hatua kuwawajibisha wale waliotoa amri za kuua na kuumiza Watanzania na/au waliozitekeleza.
KISASI CHA UCHAGUZI MKUU!
Mauaji ya wananchi wetu, matumizi ya nguvu ya kutisha dhidi ya wanawake, watoto na wazee na kukamatwa kwa mamia ya viongozi, wanachama na wananchi wa kawaida wa Jiji la Arusha ilikuwa ni kulipa kisasi kwa viongozi wa CHADEMA wa ngazi zote na kwa wananchi wa Arusha kwa kudiriki kuisambaratisha CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Ndio maana Jeshi la Polisi la Tanzania lilidiriki kumvamia na kumpiga Mbunge wetu wa Arusha Mjini hadi akapoteza fahamu wakati alipojaribu kulinda haki ya wananchi wa Arusha kuwa na Meya wa Jiji wanayemtaka na sio anayetakiwa na mafisadi wa nchi hii na chama chao.
Jeshi la Polisi la Tanzania limelipa kisasi kwa niaba ya CCM kwa sababu wananchi wa Arusha wamediriki kutumia haki zao za kisheria kupinga mipango ya mafisadi kuingiza Meya wa Jiji la Arusha atakayelinda maslahi ya mafisadi na chama chao. Wananchi wa Arusha wamelipiziwa kisasi na Jeshi la Polisi la Tanzania kwa sababu mafisadi wanajua wangeruhusu haki itendeke katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha CCM ingesambaratishwa kama ilivyosambaratishwa katika Uchaguzi Mkuu.
Mauaji ya Arusha sio kisasi cha CCM dhidi wananchi wa Arusha tu. Ni kisasi pia dhidi ya wananchi wa Tanzania na dhidi ya CHADEMA. Ni kisasi dhidi ya Watanzania wote kwa sababu, kwa mara kwanza tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa urudishwe mwaka 1992, Uchaguzi Mkuu wa 2010 ulionyesha wazi kwamba CCM imeanza safari yake ya mwisho kuelekea kwenye jaa la taka taka la historia.
Kwa mara ya kwanza, CCM ilipoteza miji mikubwa karibu yote ya Tanzania. Licha ya uchakachuaji wa kura, rushwa na uharamia wa kutisha, CCM imepoteza Jiji la Dar es Salaam, Jiji la Mwanza, Jiji la Arusha, Jiji la Mbeya na miji mikubwa kama vile Moshi, Iringa na Musoma.
Lakini CCM na mafisadi hawakupoteza miji tu, wamepoteza pia majimbo ya vijijini. CCM imepoteza nusu ya Shinyanga, zaidi ya nusu ya Kigoma, sehemu kubwa za Manyara, Singida, Mbeya, Iringa na mikoa mingine ambayo kihistoria imekuwa inaonekana kama ngome za CCM.
Na licha ya nguvu nyingi za dola na za fedha za ufisadi, Jakaya Kikwete amepunguza idadi ya kura zake kutoka kura zaidi ya milioni nane alizopata wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 hadi kura milioni tano za mwaka jana, ikiwa ni pungufu ya zaidi ya kura milioni tatu na anguko la asilimia 20!

Kuporomoka kwa CCM kumeenda sambamba na kukua na kuongezeka kwa nguvu ya CHADEMA. Licha ya uchakachuaji wa kura wa kutisha, matumizi ya vyombo vya dola na rushwa ya kutisha, nguvu na ushawishi wa CHADEMA imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Ndio chama cha upinzani chenye Wabunge wengi kuliko vyama vingine vyote vya upinzani kwa pamoja.

Ndio chama pekee cha upinzani kilichowahi kupata Wabunge kutoka kanda zote za Tanzania Bara na Visiwani. Ndio chama cha upinzani pekee kilichowahi kupata zaidi ya robo ya kura zote za Rais na Wabunge. Na ndio chama pekee chenye kubeba matumaini ya wananchi wa Tanzania kwamba Tanzania bila ufisadi wa CCM inawezekana. Ndio maana Jeshi la Polisi la Tanzania limelipizia kisasi cha CCM kwa wananchi wa Arusha na viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA.
HAKI LAZIMA ITENDEKE ARUSHA!
Damu iliyomwagwa Arusha inalilia haki. Roho za wote waliotolewa muhanga na Jeshi la Polisi la Tanzania zinahitaji haki ili ziweze kutulia na mizimu yao ipumzike.
Wote walioumizwa na ujambazi wa Jeshi la Polisi la Tanzania wanalilia fidia ili waweze kuuguza maumivu yao ya kimwili, ya kiroho na ya mali zao zilizoharibiwa. Sheria za nchi yetu zilizokanyagwa chini kana kwamba hazipo zinahitaji kulindwa, kutetewa na kuheshimiwa ili iwe fundisho kwa wahalifu wengine wa aina hii.

Kwa hiyo, sisi wote tuliokusanyika hapa leo, na wale wote wanaotusikiliza mahali popote nchini na hata nje ya nchi yetu, tuna jukumu la kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa wale
ambao tunaomboleza vifo vyao hapaleo. Tuna jukumu la kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa wale wote walioumizwa kwa risasi na

mabomu na virungu na mabuti ya Jeshi la Polisi la Tanzania. Tuna jukumu la kuhakikisha wale wote ambao waliharibiwa mali zao kwa sababu ya uhalifu huu wa Jeshi la Polisi la Tanzania wanafidiwa kwa kiasi chote cha hasara waliyoipata.
Tuna jukumu la kuhakikisha kwamba Jeshi la Polisi la Tanzania halirudii tena ujambazi wa aina hii dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia yoyote kwa kuwawajibisha wale wote walioshiriki katika ujambazi huu kwa kutoa amri za kuua au kuumiza wananchi na/au kwa kuzitekeleza.
Ili tutimize majukumu yote haya, tunahitaji kuhakikisha kwamba mambo yafuatayo yanafanyika:
   1. Serikali hii iwajibike kwa wananchi kama ilivyotamkwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Waziri wa Mambo ya Nchi Shamsa Vuai Nahodha na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema wajiuzulu mara moja ili kuwawajibisha kama viongozi na wasimamizi wa juu kabisa wa Jeshi la Polisi la Tanzania. Aidha, kujiuzulu kwao kutapisha uchunguzi huru na wa kina wa matukio yote yaliyosababisha wananchi wetu kuuawa, mamia kujeruhiwa na mamia mengine kukamatwa bila sababu yoyote na kuwekwa rumande na baadaye kufunguliwa mashtaka ya uongo ya jinai;
   2. Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Andengenye na wale wote walioamuru au kutekeleza amri ya kuvunja maandamano na mkutano halali wafunguliwe mashtaka ya jinai kwa matumizi mabaya ya madaraka na kwa kusababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia;
   3. Fidia stahili ilipwe kwa mujibu wa sheria husika za nchi kwa ndugu na/au jamaa wa wale wote waliouawa kutokana na vitendo vya Jeshi la Polisi la Tanzania na kwa wale wote walioumizwa kwa namna yoyote ile na/au kuharibiwa mali zao kutokana na vitendo hivyo;
   4. Mashtaka ya uongo ya jinai yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA, wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote waliokumbwa na kumba kumba ya Jeshi la Polisi la Tanzania yafutwe bila masharti yoyote kwa sababu maandamano na mkutano wa hadhara uliozuiliwa yalikuwa halali kwa mujibu wa sheria husika za nchi yetu. Tunasisitiza katika jambo hili kwamba viongozi, wanachama na wafuasi wetu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka haya hawatahudhuria mahakamani tena kuhusiana kesi iliyofunguliwa dhidi yao hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani;
   5. Kwa vile uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ndio chanzo cha mauaji ya wananchi na kwa kufahamu utaratibu haramu uliotumika kumpata Meya wa Jiji hilo, matokeo ya uchaguzi huo yafutiliwe mbali na uchaguzi mpya uitishwe haraka iwezekanavyo kwa kufuata sheria husika za nchi yetu;
   6. Haki ya vyama vya siasa na wananchi kufanya maandamano ya amani kama inavyotambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iheshimiwe na kutiliwa nguvu zaidi kwa kufuta vifungu vya Sheria ya Jeshi la Polisi nay a Vyama vya Siasa vinavyoruhusu Jeshi la Polisi la Tanzania kuzuia na/au kusitisha maandamano ya amani. Badala yake, sheria ziweke wazi wajibu wa Jeshi la Polisi la Tanzania kulinda maandamano ya amani na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na/au ya wananchi;
  7. Tume huru ya uchunguzi ya kimahakama (Judicial Commission of Inquiry) itakayoundwa na majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania iundwe ili kufanya uchunguzi huru, wa kina na wa wazi wa matukio yote yaliyopelekea Inspekta Jenerali wa Polisi na/au Jeshi la Polisi la Tanzania kupiga marufuku maandamano ya amani na mkutano wa hadhara na baadaye Jeshi la Polisi la Tanzania kufanya vurugu zilizosababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia.
Tunapenda kusisitiza kuundwa kwa tume huru ya kimahakama kwa sababu historia ya tume nyingine ambazo zimeundwa kwa utaratibu wa Rais kuteua watu anaowataka inaonyesha kwamba zimefanya kazi zao za uchunguzi mafichoni bila kushirikisha wadau wengine na bila wananchi kufahamu kitu kinachoendelea.
Matokeo ya tume nyingi za namna hiyo ni kwamba ripoti zake mara nyingi zimepuuzwa na/au kufichwa na watawala. Tume ya uchunguzi ya kimahakama hufanya kazi zake kwa uwazi na huruhusu wananchi kuhudhuria na/au kushiriki moja kwa moja katika kazi za tume kama mashahidi na/au kwa kuhoji mashahidi wengine wanaotoa taarifa kwenye tume hiyo;
Katika kuhakikisha kwamba madai yetu yanatekelezwa, CHADEMA inaelekeza viongozi, wanachama na wafuasi wetu mikoani na Wilayani kuandaa maandamano ya amani nchi nzima ili kulaani mauaji ya wananchi wa Arusha na kudai utekelezaji wa madai haya. CHADEMA Makao Makuu itatuma maafisa wa ngazi za juu wa chama, wakiwemo Wabunge na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kushiriki katika maandamano hayo kwa ngazi za mikoa na wilaya ili kuyaongezea nguvu na hamasa.

MAUAJI YA ARUSHA NA UMUHIMU WA KATIBA MPYA
Mauaji ya wananchi wa Arusha yanadhihirisha wazi umuhimu wa kuwa na Katiba mpya kwa ajili ya nchi yetu. Hii ni kwa sababu, Katiba viraka inayotumika sasa hivi haiheshimiwi hasa na watawala wenyewe kama tulivyoonyesha kuhusiana na uhuru wa kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara.
Aidha, Katiba yetu na sheria nyingine kama vile Sheria ya Jeshi la Polisi na ya Vyama vya Siasa zimetoa mamlaka makubwa mno kwa watendaji kama vile mapolisi kuingilia na kuvuruga haki za wananchi. Mamlaka haya ya kisheria hayana udhibiti wowote wa maana ndio maana Jeshi la Polisi la Tanzania linajiona kama liko juu ya sheria na haliwajibiki kwa makosa yoyote yanayofanywa na Jeshi hilo dhidi ya wananchi.
Aidha, matukio yaliyopelekea Mauaji ya Arusha yanaonyesha kwamba mfumo mzima wa kisheria na kitaasisi
wa kuendesha chaguzi katika nchi yetu unahitaji mabadiliko makubwa.
Matokeo ya uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini – kama ilivyokuwa kwa majimbo mengine walikoshinda wagombea wa upinzani – yalitolewa baada ya shinikizo kubwa la nguvu ya umma na sio kwa sababu ya utashi na/au uadilifu wa wasimamizi wa uchaguzi. Na kilichotuleta hapa leo ni matokeo ya uchakachuaji wa uchaguzi wa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na viongozi wengine wa Halmashauri hiyo.
Sasa ni muda muafaka wa kuhakikisha kwamba tunapata Katiba mpya itakayohakikisha kwamba vyombo vya ulinzi wa wananchi vinakuwa chini ya udhibiti halisi wa wananchi na/au vyombo vyao vya uwakilishi.
Sasa ni muda muafaka kuhakikisha kwamba tunapata Katiba mpya itakayohakikisha kwamba mfumo wetu wa uchaguzi ni huru na wa haki kwa watu na vyama vyote. Sasa ni muda muafaka kuhakikisha tunakuwa na Katiba mpya itakayohakikisha kwamba siku za huzuni kama ya leo zinabaki katika kumbu kumbu za kihistoria tu.

Na kwenye suala hili la Katiba mpya tunaujulisha umma wa Watanzania kwamba hatukubaliani hata kidogo na utaratibu uliopendekezwa na Rais Kikwete wa kuunda Tume ya Kupitia Katiba. Utaratibu uliopendekezwa ni ule ule uliotufikisha hapa tulipo. Ni utaratibu wa kubadili Katiba wa watu wale wale unaoendeshwa na/au kusimamiwa na watu wale wale kwa manufaa ya watu wale wale.
Utaratibu ambao CHADEMA itauunga mkono na kushiriki kikamilifu ni ule utakaowezesha kufanyika kwa Mkutano wa Kitaifa wa Katiba ambao utawakilisha makundi yote ya kijamii katika uundaji wa Katiba mpya.
Utaratibu wa kusubiri fadhila za Kikwete za kuteua wajumbe wa Tume ya Katiba haukubaliki tena na CHADEMA haitaubariki kwa kushiriki. Aidha, CHADEMA itatumia uwezo wake wote kuhamasisha wananchi nchi nzima ili kupinga utaratibu unaopendekezwa na Kikwete na kuunga mkono utaratibu wa kidemokrasia wa kupata Katiba mpya kwa kupitia Mkutano wa Kitaifa wa Katiba.
Tamko limetolewa Kwa niaba ya Chama na Mwenyekiti Taifa, Mh. Freeman Mbowe (Mb) wakati wa heshima za mwisho za marehemu katika Uwanja wa NMC Arusha.