Mlezi wa Hospitali ya CCBRT, Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akifurahia jambo na mtoto aliyefanyiwa upasuaji na kuwekewa jicho bandia katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam.
Dk Luijisyo Mwakalukwa Mtaalam wa maswala ya viungo katika Hospitali ya CCBRT akimonesha Mhe. Spika aliyekuwa mgeni rasmi katika kuadhimisha miaka 10 ya CCBRT mmoja wapo wa watoto waliofanyiwa ukarabati wa viungo. Mtoto huyo amefanyiwa ukarabati wa sura na mkono baada ya kuungua kwa ajali ya moto iliyopelekea kupoteza baadhi ya viungo vyake vya mw
Meneja Miradi ya Jamii wa CCBRT Bi. Brenda Msangi akimuonesha Mlezi wa Hospitali ya CCBR, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) baadhi ya vifaa vya watu wenye ulemavu vinavyotolewa na Hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa wataalam wa Tiba toka CCBRT Ndg. Tom Boures akimweleza Mlezi wa Hospitali hiyo, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) kuhusu ramani ya majengo mapya yatakayojengwa katika Hospitali hiyo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na waanzilishi wa Hospitali ya CCBRT mara baada ya kuwatunukia tuzo ya heshima katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Hospitali hiyo hapa nchini. Kutoka kushoto ni Ndg. Erwin Telemans Mkurugenzi Mkuu wa CCBRT, ndg. Eliyuko Mnyone, Mkurugenzi Mkuu wa chama cha wasioona nchini, Ndg. BK Tanna Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi CCBR, Mhe. Dr. Wilbroad Slaa, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi CCBR na Ndg. Geert Vanneste aliyekuwa Mkurugenzi wa CCBRT.
Na Mpigapicha Maalumu
0 comments:
Post a Comment