Hoyce Temu akitoa Msaada kwa mtoto Sesilia Edward
Ndugu Watanzania,
Jumapili tarehe 11 Septemba, kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Chanel Ten, kilifanya Mahojiano na Mtoto Sesilia Edward mwenye matatizo ya moyo na anahitaji upasuaji wa haraka kuokoa maisha yake. Upasuaji huo unatakiwa kufanyika nchini India.
Jumla ya dola 15 sawa na shilingi milioni 24 za kitanzania zinahitajika kuokoa maisha yake. Kama asipofanyiwa upasuaji wa haraka la sivyo atapoteza maisha ndani ya Mwezi Mmoja.
Watanzania wameanza kuchanga kumsaidia motto huyu apate matibabu. Kupitia katika simu za mlezi wake anaeishi naye huko Mbagala Bwana Nyarugembe Peter Kambaliko katika nambari zifuatazo:
Tigo Pesa:- 0715 095797
MPESA: – 0762 962467
NMB Account: 2072517079
*Hadi sasa zaidi ya shilingi milioni mbili zimekwisha changwa na bado Watanzania wanaendelea.
Chonde chonde Watanzania, hata mia tano ni mchango.
Usiache kutizama marudio ya kipindi Jumamosi saa 12:30 jioni, Chanel Ten ambapo mtasomewa kiasi cha fedha zilizokusanywa. Account ya NMB imefunguliwa kwa ajili ya hitaji hilo na namba za simu pia.
0 comments:
Post a Comment