Saudi King Abdullah Bin Abdul Aziz
Katika hatua ya
karibuni kutoka jamii ya kimataifa dhidi ya Syria, Utawala wa Saudi Arabia
umetaka serikali hiyo kukoma kuwalenga waandamanaji ambapo pia imetangaza
kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Damascus.
Taarifa ya Mfalme
Abdullah wa Saudi Arabia imesomwa kupitia runinga maarufu ya kiarabu ya Al
Arabiya ambapo balozi wa Saudia ameitwa nyumbani kutoka Syria.
Katika kile
kimeonekama kama hatua ya pamoja, muungano wa nchi za kiarabu umetoa taarifa
yake rasmi iliyolaani machafuko nchini Syria.
Muda mfupi baadaye
ikatolewa taarifa kali kutoka kwa mfalme Abdullah wa Saudi Arabia kupitia
runinga ya kiarabu Al Arabiya.
Wadadisi wamesema
taarifa hiyo ilinuia kuwafikia raia wengi wa Syria kupitia runginga hiyo, na
milki nzima ya kiarabu ikiwa ni kilele cha mwezi wa Ramadhani.
Mfalme Abdullah
ameitaka Syria kusitisha mauaji ya raia kiholela mara moja kabla hali kuzorota
zaidi.Taarifa iliendelea kusema kinachoendelea Syria hakikubaliki popote hasa
na Saudi arabia.
Mfalme ameonya Syria
kutafakari vitendo vyake au ikumbwe na hasara kubwa.Taarifa hii imetokea wakati
jeshi la Syria limeripotiwa kuwaua raia wengine hamsini.
Lalama dhidi ya
mauaji ya raia huko Syria pia zilitolewa na papa pamoja na balozi wa Marekani
mjini Damascus.Taarifa ya sasa imetajwa kama msimamo mpya wa Saudi Arabia
ambayo imekuwa ikitetea uhuru wa nchi kutoingiliwa na dola za nje.
Na hii ni ishara ya shinikizo
zaidi dhidi ya rais Bashar Al Asaad kutoka kwa jamii ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment