SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 30, 2011

Muungano Wa Afrika Waishutumu Ufaransa!!


Kamishna Jean Ping
Kamishna wa tume ya Muungano wa Afrika Jean Ping amesema kuwa uamuzi wa Ufaransa kuwarushia silaha waasi wa Libya kutoka angani ni hatari na kuwa mtindo huo unahatarisha eneo zima.
Ameiambia BBC kuwa hatua hii huenda ikaitumbukiza Libya katika matatizo sawa na yale yanayoonekana katika nchi ya Somalia ambayo imekabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi.
Ufaransa imekiri kuwa iliwapa silaha wapiganaji wa Berber kwa kuzirusha toka angani katika milima ya kusini-mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli.
Wadadisi wanasema kuwa hatua hiyo huenda inakiuka vikwazo vilivyowekwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupinga silaha kupelekwa Libya.
Bw Ping alikuwa anazungumza kutoka Equatorial Guinea ambako viongozi wa Afrika wanakutana katika kikao cha kikele cha Muungano wa Afrika.
    "Kuna matatizo kadhaa, hatari ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe, hatari ya kuigawa nchi, hatari ya kuwepo na somalia nyengine, hatari ya kusambaa silaha kila mahali na vile vile ugaidi. Hatari hizi zitazitia hofu pia nchi jirani."Kamishna Jean Ping
Suala la Libya inatarajiwa kupewa kipaumbele katika mkutano huo.
Bw Ping amesema kuwa mpango wa amani wa Muungano wa Afrika kwa Libya ulioafikiwa mwezi Marchi bado upo na unafaa. Mpango huu unahusu utaratibu wa amani unaonuiwa kufungua njia ya mazungumzo ya kisiasa.
Taarifa kuhusu Ufaransa kuwapa silaha waasi zilifichuliwa na gazeti la Le Figaro hapo jana.Gazeti hilo liliongeza kusema kuwa Ufaransa haikuwafahamisha wenzake katika kikosi cha kujihami cha Nato kuhusu hatua yake hiyo.
Hofu ya kuendelea kwa mapigano
Taarifa hiyo imesema silaha hizo ni pamoja na makombora ingawa maafisa wa Ufaransa wanasisitiza na kuthibitisha kuwa silaha zilizorushiwa waasi hao zilikuwa ndogo ndogo.
Uwamuzi huu inaarifiwa uliafikiwa baada ya mkutano wa mwezi Aprili kati ya Rais Sarkozy wa Ufaransa na kiongozi wa wapiganaji wa waasi Jenerali Abdel Ifatah Younis.
Ufaransa imekuwa ikionesha wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa mapigano haya ya Libya yalioanza mwezi February.
Waasi wameonekana kupiga hatua na wanatumai kuelekea Tripoli kutokea maeneo ya milimani ya Nafusa kilomita 65 kutoka mji mkuu huo.
Urusi na Uchina zimeshutumu mashambulio ya Nato, zikisema kuwa yamevuka mipaka ya azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1973 linaloruhusu hatua za kijeshi kuchukuliwa nchini Libya.
Hatahivyo Marekani inasema kuwa azimio la mwaka 1973 linaruhusu nchi kuwapa waasi silaha licha ya azimio la awali la mwaka 1970 ambalo liliiwekea Libya vikwazo vya silaha.

Mdau Nova Kambota Mwanaharakati Na Porojo Za Tatizo La Umeme Nchini

William Ngeleja waziri wa Nishati na Madini
---

Na Nova Kambota
Kama kuna jambo linalowaumiza vichwa watanznia basi ni swali kuwa kwanini kila wanalopanga halifanikiwi? au kwanini wananchi ni masikini licha ya maliasili zilizojaa kila kona yanchi hii? Wakiangalia elimu hoi watoto wanafeli, wakija kwenye afya hakuna kitu, wakienda kwenye kilimo na hata umeme tabu tu kwa kifupi hakuna jipya ni uduni na ubabaishaji mtupu.
 Katika lindi la mawazo ya namna hii au maswali mengi yasiyojibika tunawatazama viongozi wetu na uwajibikaji wao usiokidhi viwango kiasi kwamba wamepwaya mno , wajuzi wa kuzungumza bila kutenda, ni watu wa blah blah na porojo tu.
   Kwakweli Tanzania imetawaliwa na wapiga porojo hebu angalia kwenye hiyo kaulimbiu ya “kilimo kwanza”inavyotangazwa na kupigiwa chapuo na viongozi wetu kasha nenda huko vijijini kwenye mashamba utaona hata mabwana shamba hakuna na hizo pembejeo zenyewe za kilimo hakuna, sasa utasema hapo kuna kilimo kwanza au porojo tu?
    Geukia elimu nddio utashangaa kabisa kulivyooza huko lakini cha ajabu ni kuwa viongozi wetu bado wna ujasiri wa kusimama kwenye majukwaa na kudai kuwa serikali imeboresha elimu, elimu gani? Shule za kata? Si ndio hizi zinatoa sifuri? Nasikia siku hizi zinaitwa mtambo wa sifuri, ajabu sana! Yaani serikali inajenga majengo tupu bila walimu,madawati wala maabara kasha wanaita sekondari halafu wanazidi kuboronga wanafuta mitihani, tuziiteje hizi? Hizi ni porojo za watawala wetu, porojo porojo kila mtu anapiga porojo tu.
   Njoo kwenye hizo huduma za afya , tunaambiwa kuwa Tanzania bila maralia inawezekana tena kwa mbwembwe kwa matamasha makubwa lakini hivi mtu wa kule kijijini analala chini hana hata hiko kitanda je hiyo neti atachomeka wapi? Au motto wa mtaani analala kwenye vichochoro huyu neti atachomeka wapi? Sasa hizo Zahanati za vijijini kama kweli zinaviwango mbona vifo vya akina mama wajawazito bado vinaendelea? Hakika hizi ni porojo za viongozi wetu!
   Halafu anaibuka kiongozi mkubwa wa nchi anadai msongamano wa magari jijini Dar es salaam ni ushahidi wa kukua kwa uchumi wetu, hizi sasa porojo, uchumi wetu na nani? Mafisadi? Au Brigedia Al Adawy na Dowans? Uchumi umekua na ombaomba wameongozeka ndiyo magari yameongezeka na umasikini umekithiri , sasa huo uchumi uliokua umemnufaisha nani? Mawaziri na wabunge? Au rais na waziri mkuu? Hizi ni porojo tupu.
   Serikali nayo imeshindwa kuweka huduma za nishati ya umeme wa uhakika, sasa naona ina mchoko naam! Huu ni mchoko ndio maana kila kwenye hotuba tunapigwa kalenda mpaka mwaka huu au ule tatizo la umeme litakuwa historia halafu mda huohuo umeme ni wa mgao, waziri wa nishati nay eye hana jipya bado watu tunateseka kwa sababu ya kukosa ubunifu na uzalendo , mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati anataka tuwashe mitambo ya Dowans, watu wanahoji anataka turudi tulipotoka? Hizi kama sio porojo nini basi? Nchi ipo gizani viongozi wanapiga porojo inasikitisha sana.
    Tabia ya kupiga porojo inaendelea kudidimiza nchi , hata kwenye michezo tunapiga porojo halafu tunataka kucheza kombe la Dunia,bungeni kuna porojo kiasi kwamba bunge linafanywa sehemu ya kupigana vijembe na mipasho halafu na sisi tunaamini iko siku tutakuwa kama wenzetu wa Ulaya na Marekani ambao tayari wamefuta blah blah na porojo kwenye kamusi za vichwa vyao wanafanya mambo kizalendo na kwa kujituma, haiwezekani!
    Matokeo ya porojo yanapoonekana viongozi wetu hawachelewi kusikitika na kuhidi kujirekebisha, ona matokeo ya kidato cha nne yalivyowaumbua viongozi sasa wanajifanya wamejifunza hakuna kitu porojo tu , mabasi yanakimbia yanavyotaka wenye jukumu la kulinda usalama barabarani wanapiga porojo watu wanakufa utadhani ni msimu wa ajali.
   Siku hizi hadi viongozi wa dini wamekumbwa na tabia ya kupiga porojo , badala ya kutetea wanyonge wao wanagombana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kujigeuza miungu watu wanadanganya masikini na kuwakamua hata kidogo walichonacho na wengine wamejigeuza watabiri wanatabiria watu kufa? Hizi ni porojo tupu.
    Sasa katika muktadha huu ndio maana najiuliza kuwa nchi hii iliyolewa kwa wingi wa porojo itaendelea vipi?  Badala ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma kwasababu ya porojo zisizokwisha na hazina mipaka hata kwenye mambo ya msingi tunapiga porojo au ndio tunategemea  kuendelea kwa miujiza ya Mussa?  Tafakari!

Nova Kambota Mwanaharakati,
0717 709618 au +255717 709618
Tanzania, East Africa,
June 30, 2011
CHANZO: H@ki Ngowi

Taswira Zaidi Za Ziara Ya Mama Salma Kikwete Huko Comoro

Mke wa Rais wa Mama Salma Kikwete(aliesimama kushoto)akiongea katika haffa ya chakula cha usiku Juni 28, 2011 huko Comoro.(wa pili kutoka kwake) ni Mke wa Rais wa Comoro Mama Hadidja Aboubacar Ikililoi .
Baadhi ya wageni waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha usiku Juni 28,2011 katika Ikulu ya Comoro, kilichoandaliwa na Mke wa Rais wa Comoro Mama Hadidja Aboubacar Ikililoi Dhoinine(hayupo pichani) kwa heshima ya Mke wa Rais mama Salma Kikwete
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(kushoto)akipokea zawadi kutoka kwa Mke wa Rais wa Comoro Mama Hadidja Aboubacar Ikililoi Dhoinine wakati alipomtembelea nyumbani kwake mjini Comoro na kubadilishana mawazo.(juni 28.2011)
Mke wa Rais mama Salma Kikwete(kushoto)akiagana na Rais wa Comoro Dr.Ikililoi Dhoinine alipomtembelae Ikulu Comoro na kuzungumza nae. Juni 28,2011.
Kikundi cha ngoma ya asili ya Comoro kikitumbuiza wakati wa hafla ya Chakula cha usiku alichoandaliwa mke wa rais mama Salma Kikwete na mwenyeji wake mama Hadidja Aboubacar Ikililoi Dhoinine Ikulu. June 28, 2011- 
(Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO)

Snoop Dogg: 'MC Hammer Was Great For Rap'

 Snoop Dogg
MC Hammer
Snoop Dogg has risked damaging his street cred by praising MC Hammer, insisting the U Can't Touch This hit-maker was "great" for rap music.
Hammer is often derided by his peers for his baggy trousers and flamboyant dance moves, but he achieved huge fame in the early 1990s, selling more than 50 million records worldwide.
And Gin and Juice star Snoop has now spoken out to praise the mocked hip-hop star, insisting his global success paved the way for other young rappers to achieve international fame.
He tells Britain's Q magazine, "MC Hammer was great for rap. That was a growth and development stage where rap was taken outside the street corners of the hardcore scene and put in the realm of being international and making money."

Connor Wickham kujiunga na Sunderland


 Connor Wickham
Wickham, mwenye umri wa miaka 18, anaweza kuwa mchezaji wa Sunderland katika muda wa saa 24, iwapo watakubaliana juu ya masuala binafsi pamoja na kukamilisha uchunguzi wa kiafya.
Kandarasi hiyo ya mchezaji wa timu ya taifa ya England ya vijana wasiozidi miaka 21, ambaye alianza kuchezea Ipswich akiwa na miaka 16, huenda ikafika kiwango cha pauni za Uingereza milioni £12.5m.
Awali ilidhaniwa angejiunga na timu ya Tottenham au Liverpool.
Haikufahamika mustakabali wake kwenye timu hiyo ungekuwaje, licha ya kuongeza kandarasi yake na Ipswich hadi mwezi Aprili 2014.

Historia fupi

Wickham alijumuishwa kwenye timu ya England ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 kwa michuano ya bara Ulaya lakini hakucheza mechi hata moja.
Tangu kujiunga na Ipswich mwezi Julai 2008 amechezea kikosi cha kwanza mara 37 na kuingia kama mchezaji wa akiba mara 35,kwa jumla akifunga magoli 15.
Mwezi wa Mei 2010 Wickham alisaidia England kupata ushindi kwenye michuano ya bara Ulaya ya vijana wasiozidi miaka 17, baada ya kufunga bao la ushindi. Katika fainali hiyo England iliifunga Uhispania 2-1.
Kocha wa Ipswich Paul Jewell alisema wiki iliopita kwamba alitarajia timu nyingi kuonyesha nia ya kumsajili Wickham lakini wao hawakuwa na haraka ya kumuuza mshambulizi huyo.
Bunge Lapitisha Mswada Muhimu Ugiriki
Makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji wanaopinga mpango wa kuunusuru uchumi wa Ugiriki yameendelea mjini Athens kutwa nzima.
Raia wanapinga mpango huo ambapo kodi itaongezeka maradufu
Mabomu yaliotengenezwa na petroli yamekua yakilipukua jioni nzima, huku polisi wakutuliza ghasia wakiwarushia watu hao waliokusanyika nje ya jengo la bunge gesi za kutoa machozi.
Lakini licha ya vurugu hizo, mswada wa serikali uliochochea machungu haya yote ulipitishwa japo katika mazingira ya ushindani mkali.
Wabunge 155 waliunga mkono pendekezo hilo huku wengine 138 wakipinga. Leo wabunge watapiga kura tena kubadilisha sheria ili mpango huo utekelezwe.
Waziri mkuu George Papandreou amelenga kubana matumizi ya serikali ili ifikiapo mwaka wa 2015 watakuwa na hazina ya pauni bilioni 25.
Pamoja na hilo, amependekeza kupandisha kodi ili kuongezea kipato cha serikali, hatua iliochochea maandamano hayo nchini humo.
Lakini waziri mkuu Papandreou anasema mpango huo ukitibuka ni sawa na kuangamiza nchi hiyo.
Umoja wa ulaya umepongeza bunge kupitisha pendekezo hilo ambapo liki zingatiwa serikali ya Ugiri huenda ikafaulu kulipa malimbikizi ya madeni yake.
Hata hivyo bado kuna wale ambao hawaamini kuwa mpango huo utafaulu.
Serikali ya Ugiriki sasa inatarajia kupata mkopo wa euro billioni 110 kutoka kwa shirika la fedha duniani na umoja wa ulaya kutatua matatizo yake ya kiuchumi.

BALOZI WA IRELAND NCHINI ATEMBELEA BANDA LA SHIRIKA LA MAENDELEO YA TAIFA (NDC)

Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akiwasili katika Banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa ajili ya kuangalia na kujifunza shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na shirika hilo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(kulia) akikaribishwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Neema Mbuja (kushoto) jana jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda la Shirika hilo  kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere ili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi kuhusu mradi wa uzalishaji wa chuma ghafi eneo la Maganga Matiti , Ludewa mkoani Njombe jijini Dar es salaam kutoka kwa Meneja wa Mradi huo Abdallah Mandwanga(kulia) wakati Balozi  huyo alipotembelea Banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Meneja Mawasiliano Neema Mbuja. Mradi huo unasimamiwa na Maganga Matitu Resources Development Limited.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mtaalamu wa Miamba(Geologist) wa Kampuni ya TANCOAL Alex Sosteness(kulia) kuhusu mradi wa machimbo ya makaa ya mawe wa Mbalawala wilayani Mbinga unaotarajiwa kuanza uchimbaji hivi karibuni.Mtaalamu huyo alitoa maelezo hayo wakati Balozi huyo alipotembelea NDC kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa Neema Mbuja.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NDC jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere.
(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO).

RAIS JAKAYA ALIPOKUTANA NA BILL GATES


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9jtg6UNB4XPgRc2BfZtBcbsnH0r6hpwsCH3CklL1_ETQum731tl8M9MRiMlv4uOAWDunU1r-HJG7f9KvRCPjpr4rj2x95K_g0846TKYOuIoITi4uX3XgCgSq4B5xGyaSXooG7SvLKl90Q/s1600/JK_Bill+Gate1.jpg
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Bill na Melina Gates, Bw. Bill Gates wakati wa mazungumzo yao Ikulu, jana jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.

Sunday, June 26, 2011


VOTE FOR THIS BLOG IN TANZANIA BLOGS AWARDS 2011/

IPIGIE KURA BLOG HII INDE KATIKA TANZANIA SHIBLOGS AWARDS 2011
HABARI ZENU WADAU

NATUMAINI NI WAZIMA WA AFYA.
KWANZA KABISA NINGEPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA SAPOTI YENU MNAYONIPA  KWA KUITEMBELEA BLOG HII NA KUNISHAURI KATIKA KUENDELEZA HARAKATI HIZI MBELE.
PILI OMBI LANGU KWENU NAOMBA MUIPIGIE KURA BLOG HII ISHINDE KATIKA TANZANIA BLOGS AWARDS 2011 KATIKA  VIPENGELE VIFUATAVYO:




IT’S TWO YEARS WE REMEMBER OUR BELOVED THE KING OF POP




The World marks the two year anniversary of Michael Jackson’s passing. From growing up as a spell-binding child star to becoming the most prolific and celebrated pop artist to date, Michael’s legacy is showing no signs of fading, nor is controversial news about the icon.
WE REMEMBER YOU ALL TIME…. THE ICON OF POP MUSIC (KING OF POP MUSIC).
R.I.P.

Friday, June 24, 2011

ZIFF KUMUONA SHAGGY LAKI MOJA NA KIWANGO CHA CHINI 15,000!!

Shaggy.
Na Andrew Chale, Zanzibar.
 KUTUA NA BOTI MAALUM VISIWANI ZANZIBAR.
Mwanamuziki wa kimataifa wa ragga na mshindi wa tuzo za Grammy 2011, Orville Richard   ‘Shaggy’  usiku wa leo anatarajia kupanda jukwaani ndani ya Ngome kongwe ukumbi wa Mambo kutumbuiza shoo kali huku akisindizwa na wanamuziki nyota wa hapa nchini sambamba na kundi la THT Dancers.
Kwa mujibu wa  Meneja masoko  na mmoja wa waratibu wa Tamasha la Filamu za Nchi za majahazi maarufu  ZIFF,  Laurian Kipeja  alisema kuwa, mwanamuziki huyo wa kimataifa atapanda jukwaani  hiyo  majira ya usiku na kupiga shoo kali na  ya aina yake huku akisindikizwa na wasanii mahiri wa hapa nchini.
Kipeja alisema kuwa, tayari tiketi za shoo hiyo zimeanza kutolewa katika  ofisi zilizopo makao makuu ya ZIFF ndani ya Ngome Kongwe huku bei zikiwa nafuu kwa kila mmoja.
“Shoo hii itakuwa ni ya pekee na ya aina yake kwa wakazi wa Zanzibar na wageni mbalimbali huku kima cha juu kwa V.I.P. wa juu ni  laki moja (100000) na V.I.P wa kawaida   (50,000)  na vya kawaida kwa wageni ni 30,000 huku  wazawa ama wakazi ni 15,000” alisema Laurian.
Aidha, inadaiwa Shaggy  atatua visiwani hapa na boti maalum mapema leo na kisha saa sita mchana atafanya mkutano na vyombo vya habari  sambamba na kufunga vyombo kwenye hoteli ya Zanzibar Resort.
Kwa upande wake,meneja wa ZIFF, Danny Nyalusi alisema wasanii watakao msindikiza Shaggy ni pamoja na Sultan King, na kundi la THT ambapo watapiga shoo kali ambayo haijawai kutokea visiwani humo.
Pia alisema kuwa kwa mwaka huu, kaulimbiu ya ZIFF imebeba ujumbe wa ‘A SEASON OF VISIONS’  na kwa mara ya kwanza, tamasha hilo limedhaminiwa na  mdhamini mkuu Kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kinywaji chake cha Tusker Malt, Prime Time promotion, Coconut FM, Azam Marine Co ltd, TTB, Common Wealth Foundation, Coca-Cola, GIZ (TZ), na Ujerumani, Smole, Movenpick, Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa.

TANZANIA YAPATA TUZO YA UN KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII!!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stephen Wassira  Tuzo  ya UN  ya mshindi wa pili ya Tanzania katika kutoa huduma bora kwa Jamii (Mkurabita) wakati Makamu alipofika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Juni 23, 2011 kufunga maadhimisho ya siku ya Utumishi ya Umoja wa Mataifa na Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kuadhimishwa Barani Afrika na kufanyika nchini Tanzania.
Walipata tuzo hawa ni kutoka Ubalozi wa Afrika ya Kusini, wakifurahia tuzo yao kwa pamoja baada ya kukabidhiwa.
Balozi wa canada nchini, akipokea tuzo kwa niaba ya nchi yake.
Zoezi la kukabidhi tuzo linaendelea kwa wawakilishi wa nchi mbalimbali.
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Afrika ya Kusini nchini, wakifurahia tuzo yao baada ya kukabidhiwa.
Baadhi ya watu kutoka mataifa mbalimbali walioshiriki wakati wa hafla hiyo ya kutoa tuzo na kufunga maadhimisho hayo katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
(Picha na Muhidin Sufiani-OMR).

MICHORO YA RAZA MOHAMMED NA MWANAE EDDY YASTAWISHA JINA LA TANZANIA LONDON

 
Mzee Raza (kushoto) katika pozi na mwanae Eddy kwenye baadhi ya kazi zake.
 
Mdau (kulia) akimuuliza Mzee Raza maswali kuhusiana na kazi zake.
Salaam,
UTAMADUNI na sanaa ya Mtanzania vimewasisimua watazamaji waliohudhuria maonyesho ya mchoraji Raza Mohammed mjini London siku chache zilizopita. Mzee Raza ameanza kazi ya kuchora picha tokea kipindi cha uhuru mojawapo ya kazi zake ni pamoja na "TINGATINGA", JUMA NA ROZA. Pia amewahi kuwachora baadhi ya viongozi wetu kama Rais Mstaafu Mwinyi, Jakaya Kikwete  na wengineo wengi.

Akifungua maonyesho hayo yatakayoendelea kwa mwezi mzima kwa niaba ya serikali, Kaimu Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Chibaka Kilumanga alilishukuru shirika la Global Fusion Music and Arts (GFMA) chini ya uongozi wa Louisa Le Marchand kusaidia kutayarisha shughuli hii.

Bwana Kilumanga alisema Raza alialikwa Uingereza awali kusaidia sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Bongo.
Soma zaidi Habari http://www.kitoto.wordpress.com
Habari hii imeandaliwa na Freddy Macha akishirikiana na URBAN PULSE CREATIVE
Zifuatazo ni picha za tukio hilo:

Eddy mwenye kofia akiwa na baba yake Mzee Raza wakiweka picha ukutani.
Kutoka kushoto: Freddy Macha akifurahia Jambo na Baraka wakiwa na wadau wengine.
Freddy Macha (kushoto) akiwa kazini na bendi ya Global Fusion wakiwatumbuiza wadau waliojitokeza kwenye onyesho hilo.

Baaadhi ya kazi za Eddy.

Baadhi ya kazi za Mzee Raza.
Wadau mbalimbali walijitokeza kuangalia kazi za Mzee Raza na mwanae Eddy.
Wadau wakifurahia burudani.
Wadau wakijadiliana jambo.
Wadau wakipata misosi.

Wednesday, June 22, 2011

WAKE WA VIONGOZI WA AFRIKA WATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUHAKIKISHA KUWA MATATIZO YANAYOWAKABILI KINAMAMA NA WATOTO YANAPATA UFUMBUZI

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea katika hafla ya chai ya jioni iliyoandaliwa na Mke wa Waziri Mkuu wa Malaysia Datin Paduka Seri Rosmah Mansor maaulum kwa wake wa viongozi nyumbani kwake Putrajaya Malaysia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto ) akiongea na baadhi ya wake wa viongozi wa kitaifa kutoka nchi za Afrika wakati walipokaribishwa kwenye hafla ya chai ya jioni na mke wa Waziri Mkuu wa Malaysia Datin Paduka Seri Rosmah Mansor (kulia) nyumbani kwake Putrajaya Malaysia. (.Pichani akifuatiwa wa pili kulia) ni Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya Mama Pailine Kalonzo pamoja na mke wa Waziri Mkuu wa Lesotho Mama Mathato Mosisili (wa tatu kutoka kulia).
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete pia Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA (kushoto) wakibadilishana mawazo Juni 22,2011 na mke wa Waziri Mkuu wa Lesotho Mama Mathato Mosisili (nguo ya mistari) pamoja na mwenyeji wao Mke wa Waziri Mkuu wa Malaysia Datin Paduka Seri Rosmah Mansor (kulia) nyumbani kwake Putrajaya Malaysia. alipowaalika kwenye chai ya jioni.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
*****************************
Na Anna Nkinda – Putrajaya, Malaysia.
Wake wa viongozi wa Afrika wameshauriwa kutunza mahusiano yaliyopo baina yao ili waweze kushirikiana kwa pamoja kutatua matatizo yanayowakabili wanawake na watoto katika nchi zao kwani kundi hili limesahaulika kwa kiasi kikubwa katika jamii.
Ushauri huo umetolewa jana na Mke wa Waziri Mkuu wa Malaysia  Mama Datin Paduka Seri Rosmah Mansor alipokuwa akiongea na wake wa viongozi kutoka nchi za Tanzania, Lesotho, Kenya na Zambia wakati walipomtembelea nyumbani kwake Putrajaya kwa ajili hafla ya chai ya jioni.
Alisema kuwa moja ya malengo ya kazi zao ni kuhakikisha kuwa kina mama na watoto wanaishi katika mazingira salama hivyo basi kama wanataka kufanikiwa zaidi jambo la muhimu ni kufanya kazi kwa pamoja na kubadilishana  mawazo waliyonayo kwani Afrika ni moja na changamoto zinazowakabili wanawake na watoto zinafanana.
“Kazi mnazozifanya zinafanana na kuna malengo ambayo mmejiwekea ili muweze kufanikisha kazi zenu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kina mama na watoto wanaishi katika mazingira salama hivyo basi ni lazima muungane na kuwa kitu kimoja hakika kwa kufanya hivi mtaweza kumkomboa mwanamke na mtoto wa kiafrika”, alisema Mama Mansor.
Mama Mansor aliendelea kusema kuwa kutokana na uhalisia ni rahisi kwa wanaume kujiangalia wao wenyewe na kutatua matatizo yao lakini kwa wanawake na watoto wanatakiwa kupewa uangalizi wa ziada na msaada wa lazima hasa kwa wale wanatoka katika familia maskini.
Akiongea kwa niaba ya wenzake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alisema kuwa wao kama wake wa viongozi wanakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa kinamama na watoto wanapata huduma muhimu katika jamii ikiwa ni pamoja na elimu na afya.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa kwa upande wa Tanzania amekuwa akijitahidi kuhakikisha kuwa watoto wa kike ambao ni yatima wanapata elimu na vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinapungua.
“Taasisi yangu ya WAMA imesaidia katika jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinapungua kwa kuchangia  vifaa vya afya katika Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati na kutoa elimu kwa jamii kupitia kampeni mbalimbali za uhamasishaji”, alisema Mama Kikwete.

Monday, June 20, 2011

Alyssa Campanella Crowned Miss USA

Miss USA Alyssa Campanella
Miss California Alyssa Campanella took home the title of Miss USA at last night's pageant. Alyssa, 21, is a self-confessed "science geek."
Contestants from the 50 states and the District of Columbia were judged in three categories: swimsuit, evening gown and interview.
Alyssa will represent the United States in this year's Miss Universe pageant in September in Brazil.
Miss USA travels the nation as an advocate for breast and ovarian cancer awareness, education, research, and legislation.
Miss USA

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR!!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifungua kongamano la siku nne wa kimataifa wa utumishi wa umma leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Mawaziri wa Utumishi wa Afrika ambaye pia ni Waziri wa Utumishi wa Kenya Dalmas Otieno Anyango akitoa ufafanuzi juu ya viongozi wa Afrika kuacha tabia ya kurithishana uongozi kutoka mzazi hadi mtoto. Waziri huyo alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam katika kongamano la kimataifa la utumishi wa umma.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia wakati wa kongamano la kimataifa la utumishi wa umma liloanza leo jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu alikuwa ngeni rasmi katika ufunguaji wa kongamano hilo.
Washiriki  wa Kongamano la Kimataifa la utumishi wa umma wakimsilikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (hayupo) pichani wakati wa ufunguaji wa kongamano hilo jijini Dar es  Salaam.
(Picha na Tiganya Vicent-MAELEZO Dar).