SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 31, 2011

Rais Jacob Zuma Na Kanali Gaddafi Wakiagana Baada Ya Mazungumzo

Rais Jacob Zuma na Kanali Gaddafi wakiagana baada ya mazungumzo.
Mazungumzo kati ya rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi yaliyofanyika mjini Tripoli yamemalizika bila ya kuwa na mwafaka wa maendeleo juu ya kusitishwa kwa vita nchini Libya.
Rais Zuma amesema Kanali Gaddafi anakubali kusitishwa kwa mashambulizi lakini hayuko tayari kuachia madaraka, kama inavyodaiwa na majeshi ya NATO na waasi wa Libya.
Pendekezo la kusitishwa kwa mashambulizi lilikataliwa mwezi uliopita wakati wa mpango wa upatanishi ulioendeshwa na rais Zuma kwa niaba ya umoja wa Afrika.
Msemaji wa waasi wa Libya amekataa wito wa kusitisha mapigano na kusema kuwa wao wataendelea na mashambulizi.

MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI UGANDA AKABILIWA NA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA OFISI!!

Bw. Gilbert Bukenya
 Mahakama ya kudhibiti rushwa nchini Uganda imetoa hati ya uhalifu ya kumuita mahakamani aliyekuwa Makamu wa rais Gilbert Bukenya.
Hakimu Ngazi ya Kwanza Sarah Langa amewaita Bukenya pamoja na kampuni ya Motor Care Uganda Ltd kufika mahakamani mnamo Juni 6, 2011.
Bukenya anatakabiliwa na mashitaka katika sehemu mbili, ikiwemo la matumizi mabaya ya ofisi na tuhuma za kugushi zinazohusiana na kutolewa kwa mkataba wa kununua magari 80 aina ya BMW yaliyotumika wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM)uliofanyika nchini humo Novemba 2007.
Mkaguzi wa serikali aliyechunguza matumizi ya mkutano wa CHOGM amemtuhumu Bukenya kwa kushawishi kutolewa kwa tenda yenye thamani ya shilingi bilioni 9 kwa kampuni ya Motor Care Uganda Ltd kinyume na sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia manunuzi ya serikali nchini Uganda.
Mashitaka yanadai kuwa kati ya mwezi Mei na Novemba 2007, katika wilaya ya Kampala, Bukenya kinyume cha sheria aliagiza kufanyika manunuzi ya gari hizo.
Magari hayo 80 ya kifahari yalitumika kuwabeba wakuu wa nchi.
WAKATI HUO HUO
Chama cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda kimeunda baraza kivuli la mawaziri litakalokuwa na jukumu la kuunda sera mbadala dhidi ya serikali.
Hata hivyo orodha ya mawaziri na wajumbe wa kamati za bunge za kambi hiyo ya upinzani, bado imebaki kuwa siri yao mpaka hapo kesho Juni Mosi.

WAANDAMANAJI 15 WAUAWA YEMEN!!

Watu 15 wameuawa nchini Yemen baada ya wanajeshi wanaomtii Rais Ali Abdullah Saleh kuwafyatulia risasi waandamanaji katika mji wa kusini wa Taiz.Taarifa kutoka katika hospitali zimesema huenda idadi hiyo ikaongezeka, na kwamba mamia ya watu hao wamejeruhiwa.
Vikosi vya polisi viliwafyatulia risasi, kupiga mabomu ya kutoa machozi na kutumia mabomba ya maji kuwatawanya waandamanaji nje ya jengo la halmashauri ya jiji.
Waandamanaji hao walikuwa wakidai mwenzao mmoja aliyekamatwa aachiwe huru.

Monday, May 30, 2011

FIFA YAWASIMAMISHA BIN HAMMAN NA WARNER!!

 
Mohamed Bin Hammam na Jack Warner.
 Rais Wa Fifa Blatter.  
Shirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa, limewasimamisha kwa muda wajumbe wawili wa kamati kuu,
Mohamed Bin Hammam na Jack Warner baada ya kikao cha kamati yake ya maadili siku ya Jumapili.
Shirikisho hilo sasa litaanzisha uchunguzi kamili juu ya madai kwamba wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean walipewa rushwa.
Maafisa wawili wa shirikisho hilo Debbie Minguell na Jason Sylvester pia wamesimamishwa.
Lakini rais wa Fifa Sepp Blatter hakupatikana na hatia yoyote.
Petrus Damaseb,makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili, alisema haya juu ya Bin Hammam na Warner: "tumeridhika kwamba kuna majibu tunayohitaji kuhusu suala hili."
Hata hivyo, Fifa imesisitiza kuwa hawana hatia kwa sasa hadi itakapothibitishwa kuwa walihusika katika sakata hilo.
Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufukuzwa kutoka shirikisho hilo na kupigwa marufuku kushiriki shughuli zozote za mpira wa miguu.
Bin Hammam alikuwa mpinzani pekee wa Blatter katika uchaguzi ujao wa urais wa Fifa lakini alijiondoa mapema siku ya Jumapili.
MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA NIGERIA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Zakia Bilal, kuelekea Uwanja wa Igol Square, kuhudhuria Sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Nigeria, Dkt. Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan, aliyeapishwa jana Mei 29 jijini Abuja Nigeria. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakia Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma Maalim kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanaza wa Rais Zanzibar, Fatuma Fereji, kabla ya kuelekea Uwanja wa Igol Square, kuhudhuria Sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Nigeria, Dkt. Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan, aliyeapishwa leo Mei 29 jijini Abuja Nigeria.
 Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Sunday, May 29, 2011

STELLA MBUGE ATWAA TAJI LA MISS VODACOM DAR INDIAN OCEAN 2011

Miss Vodacom Dar Indian Ocean 2011 Stella Mbuge katika pozi.
Washiriki wakiwa jukwaani na Vazi la Jioni.
Prakatatumba tumba Prakata tumba tumba…… Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Diamond a.k.a Rais wa Wasafi akitoa burudani ya aina yake katika shindano hilo.
Wadau wakifuatilia shindano hilo kwa umakini.
Walimbwende waliofanikiwa kuingia TOP 5.
Tano bora wakiwa katika pozi na Mlimbwende wa Miss Dar Indian Ocean 2010 Alice Lushiku aliyekabidhi taji lake usiku wa kuamkia leo.
Kipindi cha Maswali na Majibu kwa walimbwende waliotinga TOP 5.
Panel ya majaji wakiwa kazini akiwamo Brother Benny Kisaka ( wa kwanza kulia).
Mshindi wa tatu Renalda Apolei baada ya kutangazwa.
Jamani looh…..hata siamini kama nimeshinda taji hili…. Ndivyo anavyosema Stella Mbuge baada ya kutangazwa kuwa mshindi namba moja wa Taji la Miss Vodacom Dar Indian Ocean 2011 huku machozi ya furaha yakimtoka.
Furaha ya ushindi wa ndugu yetu.
Miss Dar Indian Ocean 2010 Alice Lushiku katika pozi akisubiri kukabidhi taji hilo kwa Stella Mbuge.
Miss Dar Indian Ocean Alice Lushiku 2011 akikabidhi taji kwa Miss Vodacom Dar Indian Ocean 2011.
Miss Dar Indian Ocean 2010 Alice Lushiku akipata picha ya kumbukumbu na Miss Vodacom Dar Indian Ocean 2011 Stella Mbuge.
Miss Vodacom Dar Indian Ocean 2011 Stella Mbuge (katikati) mshindi wa pili Hamisa Masano (kulia) na mshindi wa tatu Renalda Apolei wakitoa tabasamu bashasha katika picha ya pamoja.
Wadau wakitazama shindano hilo.
Mshindi wa pili  Miss Dar Indian Ocean Hamisa Masano akiwa ndugu, jamaa na marafiki waliokuja kumpa support. 
Credit kwa Mo Blog

BARCELONA 3 MAN UNITED 1!!

Barcelona’s players celebrate with the trophy at the end of the UEFA Champions League final football match FC Barcelona vs. Manchester United, on May 28, 2011 at Wembley stadium in London.Barcelona won 3 to 1.
Prince Filipe of Spain applauds as Eric Abidal (R) of FC Barcelona lifts the trophy and celebrates with teammates Victor Valdes (2L) and Xavi (2R) after victory in the UEFA Champions League final between FC Barcelona and Manchester United FC at Wembley Stadium on May 28, 2011 in London, England.
Manchester United’s Dutch goalkeeper Edwin van der Sar fails to save a goal scored by Barcelona’s Spanish forward David Villa (not pictured) during the UEFA Champions League final football match FC Barcelona vs. Manchester United, on May 28, 2011 at Wembley stadium in London.
Barcelona’s Spanish forward David Villa (hidden) is congratulated by teammates after scoring a goal during the UEFA Champions League final football match FC Barcelona vs. Manchester United, on May 28, 2011 at Wembley stadium in London.
Wayne Rooney of Manchester United (C) shows his dejection as the Barcelona players celebrate victory after the UEFA Champions League final between FC Barcelona and Manchester United FC at Wembley Stadium on May 28, 2011 in London, England.
Sir Alex Ferguson manager of Manchester United (C) shows his dejection after the UEFA Champions League final between FC Barcelona and Manchester United FC at Wembley Stadium on May 28, 2011 in London, England.
Barcelona’s French defender Eric Abidal (r) celebrates with the trophy at the end of the UEFA Champions League final football match FC Barcelona vs. Manchester United, on May 28, 2011 at Wembley stadium in London.Barcelona won 3 to 1.
(Photo by Laurence Griffiths).

Saturday, May 28, 2011

WIKIENDI NJEMA ENJOY!!

POET, MUSICIAN GIL SCOTT-HERON DIES

Gil Scott-Heron was known for his poetry and soul works in the late 1960s and early 1970s.
Gil Scott-Heron, dubbed the "godfather of rap" for his mix of poetry and music, died Friday in New York, his publicist at XL Recordings said. He was 62.
It was not immediately known what killed Scott-Heron, who was best known for the 1970 song "The Revolution Will Not Be Televised," a politically and socially charged song that examined the African American condition in America at the time. The song was banned by some radio stations.
Scott-Heron died at 4 p.m. at a New York hospital, said Lisa Gottheil, his publicist at XL Recordings.
Scott-Heron defined the genre, long-time friend and former bandmate Charlie Saunders told CNN. Saunders worked on Scott-Heron's 1970 debut album "Small Talk At 125th & Lenox."
Saunders, a percussionist, said the last time he saw Scott-Heron was about two years ago when he needed a place to stay.
"He came by our house to get himself together. He spent 4 to 5 days and then moved on," Saunders said.
Much of Scott-Heron's poetry and music reflected his struggles with drugs and alcohol.
Born in 1949, Scott-Heron first gained fame for his poetry and spoken word performances in the late 1960s. By the mid-1970s, he had published two books of poetry and recorded four albums, including "Small Talk At 125th & Lenox."
His early albums, "Pieces of a Man" and "Winter in America," have been credited with influencing other musical genres, such as hip hop. But it was the song "The Revolution Will Not Be Televised" that put Scott-Heron on the musical map.
His music has been sampled by everyone from Kanye West, who sampled "Comment #1" for his 2010 song "Who Will Save America," to Common's sample of "No Knock" on his 2008 hit "Universal Mind Control."
After a 13-year hiatus from making music, Scott-Heron put out a new album last year called "I'm New Here."
In a 2008 interview with New York magazine, Scott-Heron revealed he had contracted HIV, the virus that causes AIDS, after years of battling drug and alcohol addictions. In 2001 and 2007, he was jailed on drug charges.

FAINALI LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA LEO NANI KUIBUKA MSHINDI??

BARCELONA Vs MANCHESTER UNITED.........
Klabu ya Barcelona ya Hispania leo inashuka dimbani kupambana na timu ya Manchester United ya Uingereza katika kuwania ubingwa wa michuano hiyo katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu itakayopigwa katika uwanja wa Wembley.
Timu ya Barcelona ikiwa chini ya kocha wake Pep Guardiola na Manchester United ikiwa chini ya Sir Alex Fegurson, zote zinatamani kutwaa taji hilo ili kukamilisha furaha za ushindi, baada ya timu hizo kuibuka videdea wa ligi katika nchi zao.

MTANANGE LEO SIMBA YA TANZANIA V/S WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO.

Kikosi cha Simba. 
Kikosi cha Wydad Casablanca  cha Morocco.
Klabu ya Simba ya Tanzania leo inatarajiwa kuunguruma wakati itakapovaana na Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco katika mechi ya raundi ya tatu ya Ligi ya klabu Bingwa Afrika itakayochezwa katika uwanja wa Metrospot jijini Cairo nchini Misri.
Simba na Wydad zilipzta nafasi ya kucheza raundi ya tatu na mshindi kufuzu robo fainali ya ligi ya klabu bingwa kwenye uwanja huru baada ya Simba kushinda rufaa yao dhidi ya mchezaji Janvier Besala Bokungu wa TP Mazembe aliyechezeshwa na mabingwa hao wa zamani kinyume cha utaratibu.
Timu itakayofungwa leo itashiriki michuano mingine ya Kombe la Shirikisho.
Naitakia Simba kila la kheri iweze kushinda mechi ya leo na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo na kuiletea sifa Tanzania kwa ujumla.
Mungu Ibariki Simba Sports Club.
Mungu ibariki Tanzania.

MKE WA WAZIRI MKUU WA INDIA MAMA GURSHARAN KAUR AISAIDIA WAMA MILIONI 15!!

Mke wa waziri Mkuu wa India Mama Gursharan Kaur(Kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi  milioni 15 mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) fedha ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali za kuwasaidia watanzania zinazofanywa na taasisi hiyo. Msaada huo umetolewa leo katika ofisi za WAMA zilizopo jijini 
Dar es Salaam.
 
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.
Na Anna Nkinda – Maelezo
Mke wa waziri Mkuu wa India Mama Gursharan Kaur ametoa msaada wa shilingi  milioni 15 kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleoo (WAMA) fedha ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali za kuwasaidia watanzania zinazofanywa na taasisi hiyo.
Msaada huo umetolewa leo katika ofisi za WAMA zilizopo jijini Dar es Salaam wakati mama Kaur alipoitembelea taasisi hiyo inayoongozwa na  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kufahamu  shughuli zinazofanywa na WAMA.
Akikabidhi  msaada huo Mama Kaur alisema kuwa ameguswa na kazi zinazofanywa na WAMA za kuisaidia jamii ya kitanzania, hivyo msaada huo utasaidia kutekeleza majukumu mbalimbali wanayoyafanya.
Kwa upande wake Mama Kikwete alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo yanayoikabili jamii ya kitanzania.
Alisema kuwa taasisi ya WAMA imekuwa ikipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa maendeleo wa ndani na wa nje ya nchi hivyo aliwaomba wananchi wenye moyo wa kusaidia wasisite kufanya hivyo bila ya kuangalia kama msaada watakaoutoa ni mdogo au mkubwa.
Mama Kikwete alisema kuwa Taasisi ya WAMA imekuwa ikifanya kazi mbalimbali za kuhakikisha kuwa inawasaidia wanawake kuinua maisha yao, kuisaidia jamii ya watanzania kuwa na afya bora, kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa vijana na kada tofauti, kushughulikia uzazi salama  na kuwawezesha watoto wa kike ambao ni yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu.
Mama Kaur ameambatana na mumewe waziri Mkuu wa India Dr. Manmohan Singh aliyeko nchini katika ziara ya kikazi ya siku tatu.

NELLY KAMWERA NDIE MISS UNIVERSE 2011

Miss Universe 2011,Nelly Kamwera akiwani mwenye furaha mara baada ya kushinda usiku huu katika mashindano yaliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar.
Miss Universe 2011,Nelly Kamwera (kati) akiwa na mshindi wa pili,Neema Kilango (kulia) na Mshindi wa tatu,Yaceba Asenga mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Miss Universe 2011 yalifofanyika katika hoteli ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar usiku huu.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania,George Rwehumbiza (kulia) na Meneja wa Mambo ya Nje wa Vodacom,Nector Foya wakiwa katika picha ya pamoja na Miss Universe usiku huu.
Mwanzilishi wa Mtandao wa Jamii Forums,Maxence Melo (kulia) na Mmoja wa wasaidizi wake,Bahati Chande wakiwa pamoja na top 3 ya Miss Universe usiku huu.
Miss Universe 2010 aliemaliza muda wake usiku wa leo,Hellen Dausen akimvisha Crown Miss Universe 2011,Nelly Kamwera ikiwa ni ishara na kukabidhima rasmi majukumu hayo ya ulimbwende.
Top 5 (anayeonekana katikati yao wa tatu toka kulia ni MC ABBY)
Mratibu wa shindano la Miss Universe,Maria Sarungi akitangaza washindi katika kinyang'anyiro hicho.
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation ambaye pia alikuwa ni mmoja wa majaji wa mashindano hayo,Mwamvita Makamba akiuliza swali kwa mmoja wa washiriki wa Miss Universe wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Washiriki woote stejini.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini waliofanikisha shughuli nzima ya Miss Universe usiku huu.
Majaji wakifuatilia mashindano.
AY na Miss Universe 2011.
Click