SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 5, 2011

MWANAMUZIKI MARTELLY ASHINDA URAISI WA HAITI

Bw.Michel Martelly.
Mwanamuziki wa zamani wa Haiti, Michel Martelly, ameshinda uraisi wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali, Martelly amepata asilimia 67 ya kura na hivyo kumshinda mpinzani wake, mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Mirlande Manigat.
Matokeo haya yanaimaliza ndoto ya Manigat ya kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais kwenye taifa hilo la Caribbean.
Sasa Martelly, mwenye miaka 50, anakabiliwa na changamoto la kuijenga upya Haiti, ambayo hata kabla ya tetemeko la ardhi la Januari 2010, ilikuwa tayari ni miongoni mwa mataifa masikini kabisa duniani. Tetemeko hilo la ardhi liliuharibu kabisa mji mkuu wa Port-au-Prince huku likiuwa watu 225,000.
Matokeo rasmi yanatarajiwa hapo tarehe 16 Aprili, lakini kwa tafauti hii ya kura tayari ushindi huu unampa nafasi ya uhakika Martelly.

Na MO BLOG TEAM.

0 comments:

Post a Comment