SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, August 30, 2010

Sarrazin akosolewa vikali

Mwanachama wa Bodi ya Benki Kuu ya Ujerumani, Thilo Sarrazin.

Thilo Sarrazin,mwanachama wa Bodi ya Benki Kuu ya Ujerumani, amekosolewa vikali na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle na Baraza Kuu la Wayahudi kuwa anachochea ubaguzi na chuki dhidi ya Uyahudi.

 Chama cha SPD hakimtaki tena kama mwanachama na viongozi wa SPD wametoa mwito kwa Sarrazin kuondoka chamani. Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema haiwezekani kabisa kuyakubali matamshi ya Sarrazin.

Kufuatia matamshi ya utata ya Thilo Sarrazin kuhusu wahamiaji wa Kiislamu nchini Ujerumani yaliyokosolewa vikali, sasa mwanachama huyo wa Bodi ya Benki Kuu ya Ujerumani "Bundesbank" na chama cha SPD, amekosolewa upya kwa maoni yake kuwa Wayahudi wana jeni ya aina moja.Vile vile amesema, wahamiaji wa Kiislamu barani Ulaya hawataki au hawawezi kujijumuisha katika jamii za nchi za magharibi.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hayo ni matamshi yasiokubalika hata kidogo. Matamshi hayo yanavuka mpaka na yanaonyesha chuki dhidi ya makundi fulani katika jamii. Ubaya zaidi, Sarrazin anadai kuwa anashughulikia mada hiyo, lakini matamshi yake hayasaidii hata kidogo. Amesema:"Suala la kuwajumuisha wahamiaji ni mada iliyo muhimu sana katika jamii yetu. Nimewaalika ofisini kwangu wajumbe wanaoshughulikia mada hiyo na tumefanya kazi kubwa - na bado kuna kazi nyingi za kufanywa. Lakini vile anavyozungumza, atasababisha mgawanyiko katika jamii na hiyo itakwamisha majadiliano."Wakati huo huo, Naibu Kansela na Waziri wa Mambo ya Nje,Guido Westerwelle, amesema matamshi ya kuchochea ubaguzi au chuki dhidi ya Uyahudi hayana nafasi yo yote ile katika majadiliano ya kisiasa. Nae waziri wa ulinzi, Karl-Theodor zu Guttenberg, ameuliza iwapo Sarrazin anafaa kubakia katika Bodi ya Benki Kuu. Amesema, hata uchokozi una mipaka na ni dhahiri kabisa kuwa Sarrazin ameivuka mipaka hiyo kwa matamshi yake yasiofaa.Kilichozusha hasira ni matamshi mapya ya Sarrazin kuwa watu wenye asili mbali mbali wana jeni tofauti. Akawataja Wayahudi na Wabasque. Baraza Kuu la Wayahudi limesema, matamashi hayo ni chuki ya kibaguzi. Sasa hata katika chama cha SPD, sauti zinazidi kupazwa kupinga uanachama wa Sarrazin. Kiongozi wa SPD katika jimbo la Berlin, Michael Müller amesema, chama hakiwezi tena kumvumilia mwanachama anaekwenda kinyume na maadili ya chama chake. Viongozi wa ngazi za juu katika chama cha SPD wamemshauri Sarrazin kuondoka kwa hiyari, lakini mwanachama huyo amepinga pendekezo hilo.Mwandishi: Müller,Andrea/ZPR/P.Martin/RTRE

Mwaka wa tano baada ya kimbunga cha Katrina.


Rais Obama ameahidi kwamba utawala wake utawasaidia waathirika wa Katrina.
Rais Obama ameahidi kwamba utawala wake utwasaidia waathirika wa Katrina
Zaidi ya watu 1,500 waliuawa,wakaazi waliilaumu serikali kwa uzembe.
Rais wa Marekani, Barack Obama akihudhuria kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu kutokea kwa kimbunga cha Katrina katika eneo la New Orleans, aliwasifu wakaazi wa mji huo kwa ujasiri wao na kuahidi kusaidia katika ujenzi mpya na ukarabati wa mji huo hadi ‘kazi yote imekamilika’.
Zaidi ya watu 1,500 walikufa katika kimbunga hicho kilichoiharibu kabisa sura halisi  katika mji huo ulioko katika jimbo la Louisiana.
Rais Obama alikiri kwamba mji huo unaosifika kwa muziki wa aina ya Jazz, bado unahitaji msaada lakini jitihada za wakaazi zimehakikisha mji wenyewe unashamiri tena.
Tarehe 29 Agosti 2005. Maji yenye kasi yalivunja kingo za maji.
Bw Obama alisema kwamba kimbunga hicho kilichosababisha maji kuvuka kingo zamjini huo, kiliwasomba wakaazi na makaazi na lilikuwa janga baya ambalo pia lilikuwa kosa la kibinaadamu lililoonyesha aibu kutokana na uzembe wa serikali. Hata hivyo rais Obama aliahidi kwamba eneo hilo ambalo linapambana na athari ya muda mrefu ya baada ya kimbunga hicho, mzozo wa kiuchumi na pigo la hivi maajuzi la kuvuja kwa mafuta katika ghuba ya Mexico, linaweza kuutegemea utawala wake kwa msaada. Aliuambia umati wa watu kwamba utawala wake utasimama bega kwa bega hadi kazi imekamilishwa.
Tarehe 29 mwezi Agosti mwaka wa 2005, mji huo unaosifika sana kwa muziki na mandhari ya kuvutia, ulivurugika wakati maji yenye kasi yalipozivunja kingo  za maji.
Zaidi ya watu milioni 1.4 wakiwemo wakaazi na watalii waliamrishwa kuhama lakini maji yalipofika wengi walikuwa bado hawajaondoka.
Waathirika wengi waliukimbilia uwanja ambao watu 10,000 waliopoteza makaazi walikopiga kambi. Kimbunga hicho kilisababisha hasara  hadi katika  majimbo ya Mississippi na Alabama na kukata umeme, mawasiliano  pamoja na kuyachafua maji ya kunywa.
Utawala wa rais Obama ulisema umetoa msaada wa kuimarisha miundo mbinu pamoja na idara za sheria na afya  na pia kufadhili mipango ya kujenga vizuizi vya takriban kilomita 350 vya kiwango cha juu kuliko vile vya awali.
Siku  ya kumbukumbu ya miaka mitano tangu kutokea kwa kimbunga cha Katrina,  ilikamilika kwa misa iliyofanywa katika jumba la Armstrong mjini humo. Meya wa mji huo, Mitch Landrieu akizungumza katika misa hiyo alisema, lazima wakabiliane na ukweli kwamba katika mwaka wa tano katika karne hii ya 21,siku nne za mihangaiko, ziliandamwa pia vurugu katika barabara za Marekani. Alisema Vizuizi vya kuzuwia maji viliporomoka na serikali ikashindwa kufanya kazi na kwamba ni siku ambayo hawataisahau yakiwa ni matukio yasiyofaa kutokea tena.  
Meya huyo alisema janga hili liliwafunza wakaazi wake umuhimu wa ujirani wema na ushirikiano baina ya watu wa asili tofauti.        
Mwandishi, Peter Moss /AFP

Sunday, August 29, 2010

JK Aiteka Mpanda Na Sumbawanga

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akimnadi kwa wananchi mgombea Ubunge wa jimbo la Sumbawanja mjini kupitia chama hicho,Bw.Khalfan Hayeshi pindi alipokuwa katika mkoa wa Rukwa jana.
Rais Jakaya Kikwete akigombewa kusalimiwa na wananchi wa Sumbawanga alipokuwa akiwasili katika uwanja wa Mandela.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi pindi alipowasili mjini Mpanda na kufanya mkutano wa kampeni.
Rais Jakaya Kikwete akishuka kwenye Helkopta mara baada ya kuwasili Sumbawanga mjini tayari kwa mkutano uliofanyika jana kwenye uwanja wa Mandela.
kwa picha zaidi
TANZANIA YAICHAPA ERITREA GOLI 1 KWA 0
****RAMADHAN TORNAMENT****
Kikosi  Kazi cha Tanzania. 
Jana ilikuwa ni patashika nguo kuchanika  katika Uwanja wa MASAB TANK HYDERABAD INDIA mtanange wa kukata na shoka kati ya Timu yaTanzania na Eritrea katika kinyanganyiro kinachoitwa RAMADHAN TORNAMENT jana ilikuwa fainali.
Baada ya mechi hii kuahirishwa kwa siku kadhaa kutokana na mvua kubwa kunyesha mjini hapa na maji kujaa uwanjani hapo, Hatimaye siku ya jana hali ya hewa  iliweza kuwa na vijana machachari wa timu  ya Tanzania na kufanikiwa kuwatoa katika kinyanganyiro hicho baada ya kuwachapa Eritrea bao 1 kwa  0.Kwa upande wa Tanzania msakata kabumbu machachari  kijana mdogo mkubwa wa mambo Said Omar Mihala aka Young Halla aliweza kuipatia timu yake bao moja katika kipindi cha pili na Eritrea wakitoka uwanjani na huzuni.
Said Omar Mihala aka Young Halla akishikilia kikombe huku akitabasamu.
Mapungufu yaliyojitokeza ni kuwa ilioneka kuna wachezaji katika timu ya Eritrea wakiichezea timu hiyo wengi wao kutoka somalia na Sudan na Eritrea wenyewe si wengi na wanafahamika, swali linakuja je kamati ya maandalizi ya mashindano hayo inalijua hili au ndio........................?
Hadi mwisho wa mechi hiyo Tanzania walitoka kifua mbele  kwa kuifunga Eritrea  1 kwa 0.
Timu ya Tanzania  jana imeweza kupata nafasi ya kuibuka washindi  katika mashindano hayo.
 
Said Omar Mihala akivishwa medali ya mchezaji bora katika mashindano hayo.
Hizi ni vikombe na medani vikiwa vimepangwa kwa ustadi wa aina yake.
Meza hii ndio waliokaa wageni rasmi kama uionavyo pichani.
Huu ndio uzi mpya waliokabidhiwa timu ya Tanzania.
Wachezaji katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa kikombe na medani zao.
Foba akipongezwa na mgeni rasmi
Shah akipongezwa na mgeni rasmi
Enock akipongezwa na mgeni rasmi
Hapa watanzania wakisubiri kupewa kikombe chao cha ushindi 2010
Jana sio siri shangwe la vijana wa JK lilianza kuonekana mapema kutoka kwa wachezaji na pia washangiliaji kwa kuishangilia timu yetu kwa nguvu zote hatimaye ushindi ukapatikana kama ilivyo ada.
Hivyo basi uongozi wa TSAH unawashukuru wanajumuiya wote kujitokeza kwa wingi bila kukosa kuishangilia timu yenu . 
 Mungu ibariki Tanzania,Watanzania TSAH,na Watu wake,Amin.
Imeandikwa na ALLY S. MGIDOS.

Chelsea yazidi kuongoza England

Didier Drogba

Didier Drogba
Chelsea vinara wa Ligi Kuu ya England wameendeleza rekodi ya ushindi kwa msimu huu baada ya kuwalaza Stoke City mabao 2-0. Pamoja na ushindi huo Chelsea walikosa kufunga mkwaju wa penalti baada ya Frank Lampard aliyecheza chini ya kiwango kupiga shuti hafifu lililodakwa na mlinda mlango Thomas Sorensen wa Stoke City. Mabao ya Chelsea yalifungwa na Florent Malouda kipindi cha kwanza na bao la pili lilipachikwa na Didier Drogba kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili. Kwa matokeo hayo Chelsea wamefikisha pointi tisa kwa michezo mitatu na wanaongoza ligi hiyo. Katika pambano lililochezwa mchana, Arsenal nao waliweza kujiongezea pointi tatu baada ya kuwafunga Blackburn Rovers nyumbani kwao mabao 2-1 na kufikisha ponti saba. Matokeo mengine kwa michezo ya leo ya Ligi Kuu ya England, Blackpool walitoka sare.

Thursday, August 26, 2010


Balozi Peter Kallaghe Awasili Nchini Uingereza
Balozi mpya wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe akisaini kwenye kitabu cha ubalozini hapo tayari kwa kuanza kazi rasmii.Balozi mpya wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu ambaye yupo nchini Uingereza kwa shughuli za kikazi.Balozi mpya wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe akipokelewa na wafanyakazi wa ubalozini hapo.akisalimiana na baadhi wa wafanyakazi wa ubalozini hapo pindi alipokuwa amewasili.

Mubarak: Misri kujenga kituo chake cha kwanza cha nishati ya nyuklia

Sample Image
Rais Hosni Mubarak wa Misri amesema nchi yake inajiandaa kujenga kituo chake cha kwanza cha kuzalisha nishati ya nyuklia. Kupitia Msemaji wake Suleiman Awadh, Rais Mubarak amesema kuwa kituo hicho cha kuzalisha nishati hiyo muhimu kitajengwa mjini El-Dabaa, katika pwani ya magharibi ya badari ya Alexandria. Serikali ya Misri inatarajia kituo hicho kuanza shughuli zake kufikia mwaka wa 2019. Katika safari yake nchini Misri mwezi Juni, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA Yukiya Amano alisema kuwa, wakala huo uko tayari kuisaidia nchi hiyo kunufaika na nishati ya nyuklia. Misri ilitia saini Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia NPT mwaka wa 1981. 

*****************************
I
Sample Image

Iran yasema kuwa Marekani ndio mfadhili 
mkubwa wa uhaini duniani

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa utawala wa kibeberu wa Marekani ndio mfadhili mkubwa wa viongozi wahaini ulimwenguni na wachochezi wa ghasia zilizogubika nchi kadhaa baada ya kufanyika chaguzi katika nchi hizo. Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran ya Kiislamu Heidar Moslehi ameviambia vyombo vya habari kuwa, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na wizara yake, Marekani ilitumia takriban dola bilioni moja kufadhili machafuko yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu hapa nchini mwaka jana. Amesema kuwa, licha ya ufadhili na uchochezi uliofanywa na Marekani baada ya uchaguzi huo, maafisa usalama wa Iran waliweza kukabiliana na njama kubwa zilizokuwa zimepangwa na nchi hiyo. Moslehi ameongeza kuwa, Marekani ndiyo iliyowapa nguvu vibaraka walioongoza machafuko hayo nchini. 

Idadi ya waliofariki katika maporomoko ya udongo China yafikia 38

Sample Image
Polisi ya China imeripoti kuwa idadi ya watu waliofariki dunia kwenye maporomoko ya udongo mkoani Yunnan nchini humo imefikia 38 huku wengine zaidi ya 54 wakitoweka. Shirika la Habari nchini humo la Xinhua limesema kuwa, timu ya waokoaji imeweza kuokoa mwili wa mtu mmoja tu hadi kufikia sasa kwenye vifusi vya majengo yaliyofukiwa na udongo kufuatia maporomoko hayo. Licha ya serikali ya China kujaribu kutengeneza daraja linalounganisha eneo la janga na eneo ambalo halijaathirika, vijiji vilivyoko katika mkoa huo wa Yunnan vimeendelea kuathirika pakubwa na mafuriko pamoja na maporomoko. Janga hilo la kimaumbile la mvua kubwa limeikumba China tangu mwishoni mwa mwezi Mei na kusababisha mafuriko na maporomoko ambayo yamepelekea mamia ya watu kupoteza maisha yao. 

Afrika Kusini yataka kuungana na kundi la Mataifa ya BRIC

Sample Image
Afrika Kusini imesema kuwa inataka kuorodheshwa kwa njia isiyo rasmi katika kundi la BRIC linalozijumuisha nchi za Brazil, Russia, India na China. Lengo kuu la kundi la BRIC ambalo linaongoza mataifa yanayokuwa kiuchumi, ni kuhakikisha mataifa yanayokuwa kiuchumi yanashirikishwa katika masuala ya uchumi wa ulimwengu na kupata sauti kwenye mashirika ya kimataifa kama lile la Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF. Zuma ambaye yuko ziarani nchini Uchina tayari ameshazuru nchi za Brazil, Russia na India katika jitihada za kutafuta uanachama katika kundi la BRIC. Rais huyo amesema kuwa, juhudi zake za kutafuta uanachama huo zinatokana na ukweli kwamba hakuna hata nchi moja ya Afrika ambayo ni mwanachama wa kundi hilo. Baadhi ya wadadisi wa masuala ya kiuchumi wanaona kuwa, uchumi wa wanachama wa BRIC unakuwa kwa kasi na unatazamiwa kuupiku ule wa mataifa 8 yaliyostawi kiuchumi ya G8.

Redknapp asema haogopi timu yoyote

Redknapp asema haogopi timu yoyote

Harry Redknapp



Tottenham wajigamba
Meneja wa Tottenham Harry Redknapp amesema wapo tayari kukabiliana na timu yoyote katika hatua ya makundi kuwania Ubingwa wa Ulaya.
Spurs iliilaza Young Boys mabao 4-0 pambano lililochezwa uwanja wa White Hart Lane na kufanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 1961-62.
Kuna kila dalili Tottenham wakapangwa kundi moja na mabingwa watetezi Inter Milan ama Barcelona, lakini Redknapp amejigamba hawahofii timu yoyote.
Amesema"Tupo tayari kukabiliana na yeyote, tumekwishafuzu hatua ya makundi tutapambana na yeyote bila kuogopa".
Mabao matatu yaliyofungwa Peter Crouch na moja la Jermain Defoe, yaliiwezesha Tottenham kulipa deni la kufungwa mabao 3-2 ugenini katika mechi ya awali na hivyo kuingia hatua hiyo kwa jumla ya mabao 6-3 dhidi ya timu ya Bern kutoka Switzerland.

Arsenal yamsajili Squillaci


Sebastian Squillaci
Klabu ya Arsenal imekamilisha taratibu za kumsajili mlinzi wa kimataifa wa Ufaransa Sebastian Squillaci kutoka klabu ya Sevilla.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 30 mwishoni mwa wiki iliyopita aliwasili London ambako alipimwa afya yake siku ya Jumatatu katika uwanja wa Emirates.
Mlinzi huyo wa kati wa zamani wa klabu ya Lyon ya Ufaransa hatacheza mchezo wa Jumamosi wa ligi dhidi ya Blackburn, lakini anaruhusiwa kucheza michezo ya ligi kuwania ubingwa wa vilabu vya Ulaya.
Squillaci anaonekana ataisaidia ngome ya Arsenal wakati huu walinzi wakongwe Sol Campbell, William Gallas na Mikael Silvestre wakiwa wameondoka katika klabu hiyo.
Imelezwa Arsenal imempatia mkataba wa miaka mitatu, licha ya kawaida ya Wenger kuwapatia mkataba wa muda mfupi wachezaji waliovuka umri wa miaka 30.
Mlinzi huyo alijiunga na Sevilla akitokea klabu ya Les Gones miaka miwili iliyopita na aliomba asichezeshwe katika mchezo wa marudio kutafuta nafasi ya kushiriki hatua ya makundi wiki iliyopita kati ya Sevilla na Braga ili asikose aweze kuichezea Arsenal katika mashindano hayo.
Wakati huu mlinzi mwengine wa Arsenal Philippe Senderos akiwa amehamia Evarton, Wenger alimsajili mlinzi wa kati Laurent Koscienly, ambapo kwa sasa klabu hiyo itakuwa na hazina kubwa ya walinzi wa kati baada ya Djourou naye kupona kabisa.
Squillaci alikuwemo katika kikosi cha ajabu ajabu cha Ufaransa kilichoshiriki Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na alicheza walipofungwa na wenyeji Bafana Bafana, hali iliyosababisha wamalize wa mwisho katika kundi lao.
Wakati alipokuwa majeruhi, aliweza kuanza kucheza mechi 14 za ligi kwa timu yake ya Sevilla msimu uliopita.

STARS YAANZA MAZOEZI YA KUIVAA ALGERIA


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Paulsen (kulia), akiwapa somo wachezaji wake.
TIMU ya taifa, Taifa Stars, leo imeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ikijiandaa na mpambano wake na timu ya taifa ya Algeria kwa ajili ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika unaotarajiwa kufanyika Septemba 3 mwaka huu nchini Algeria.

John Boko ‘Adebayor’ akiachia shuti kali lililomshinda kipa wa timu hiyo, Jackson Chove (hayupo pichani), na kuingia wavuni.

Daktari wa Stars, Mwanandi Mwankyema (kushoto) akikimbia sambamba na kipa, Juma Kaseja, aliyeumia mkono akiwa kwenye majukumu ya timu hiyo na kufungwa P.O.P.

Jan Paulsen akisisitiza jambo kwenye mazoezi hayo, kushoto ni mchezaji wa timu hiyo Abdulhalim Humud.
Paulsen akiwapa somo Humud (kushoto) na Nizar Khalfan. PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS 

ATISHIWA KUUAWA KWA KUMTUPA PAKA KWENYE PIPA LA TAKA

Polisi wakimsindikiza Mary Bale wakati akiondoka nyumbani kwake.
MARY BALE, mwanamke mfanyakazi katika benki ambaye alinaswa na kamera za CCTV akimtupa paka aitwaye Lola katika pipa la taka, jana alisema anasikitika sana kwa kitendo chake hicho alichokifanya bila kufikiri.
Mwanamke huyo ambaye amepata vitisho vingi kupitia mtandao wa Facebook, aliongeza: “Siwezi kuelezea kwa nini nilifanya hivi, nilipitiwa na pepo mbaya na sikutaka kumpa mateso Lola.”
Polisi wanafuatilia kwa karibu vitisho vilivyowekwa katika mtandao huo dhidi ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 kutoka Conventry.
Wamiliki wa Lola, Stephanie na Darryl Mann, walitoa wito wa jumuia “kutojichukulia maamuzi mikononi mwao” kuhusu suala hilo.
Hivi ndivyo Mary Bale alivyomtupa paka aitwaye Lola katika pipa la taka.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUMWAKILISHA RAIS KIKWETE KUAPISHWA KWA RAIS WA BURUNDI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watanzania waishio Burundi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura Augost 25 jana Waziri mkuu leo atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kuapishwa kwa rais wa chi hiyo, Pierre Nkurunzinza.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiongozwa na Spika wa Bunge la Burundi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndegewa Bujumbura Augosti 25 ambako leo atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumwapisha Rais wa Nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Burundi waliofika kwenye uwanja wa ndege BujumburaAugosti 25, 2010 jana ambako leo atamwakilisha Rais Jaky Kikwete katika sherehe za kumwapisha Rais wa Burundi, Pierre Nkurnzinza. Kulia ni Spika wa Bunge la Nchi hiyoPie Ntavyohanyuma na wapili kushoto ni mkewe Tunu.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Kipindupindu yasababisha maafa Nigeria


Mafuriko nchini Nigeria
Wizara ya afya nchini Nigeria, imeonya kutokea mlipuko wa kipindupindu huku watu 150 wakifariki dunia kutokana na maradhi hayo.
visa vya kipindupindu vimeripotiwa katika majimbo kumi na mbili kati ya majimbo thelathini na sita nchini humo.
Wizara ya afya imesema maradhi hayo yamesababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha na ukosefu wa maji safi ya kunya na vyoo.


'Hawakusema wanabakwa' yasema UN

Mjumbe mmoja wa Umoja wa mataifa amesema majeshi ya Umoja wa Mataifa yasingeweza kuzuia ubakwaji wa zaidi ya wanawake 150 na wavulana, uliofanywa na waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,- DRC kwa sababu majeshi hayo hayakuwa yakifahamu kinachoendelea.
Mwanamke aliyebakwa


Zaidi ya wanawake 3,500 wamebakwa tangu kuanza kwa mwaka huu kwa mujibu wa UN
Majeshi hayo ya kulinda amani yalipita katika eneo la tukio mara mbili, lakini waliambiwa waasi walikuwa wakiweka vizuizi vya barabarani tu na sio zaidi, amesema mjumbe huyo.mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki Moon amesema 'alikasirishwa' na kitendo hicho na ametuma wajumbe wawili kwenda kuchunguza.
Wanawake 200Umoja wa Mataifa (UN) umeitisha kikao cha dharura cha Baraza la usalama, kujadili jinsi ya kukabiliana na suala hilo. Ubakaji huo ulitokea katika mji wa Luvungi na vijiji vya karibu, ikiwa ni umbali mdogo tu kutoka ilipo kambi ya jeshi la kulinda usalama la Umoja wa Mataifa, amesema mfanyakazi mmoja wa utoaji misaada na daktari raia wa nchi hiyo.Baadhi ya taarifa zinasema waasi waliteka eneo moja na kubaka wanawake 200 na baadhi ya wavulana wadogo katika kipindi cha siku nne.
Ubakaji DRC
Wakinamama DRC wakijiandaa na chakula cha usiku Goma mwaka 2009
Kundi la pamoja la haki za binaadam la Umoja wa Mataifa limethibitisha tuhuma hizo za ubakaji kwa wanawake wasiopungua 154, uliofanywa na waasi wa kundi la FDLR wa Rwanda na Mai-Mai wa Kongo Kinshasa katika kijiji cha Bunangiri.
Siku 10
Hata hivyo Roger Meece, afisa wa UN mashariki mwa Kongo, amesema wakazi wa huko waliwaambia wanajeshi wa Umoja wa mataifa waliokuwa wakifanya doria kuhusu vizuizi vya barabarani, lakini hawakusema lolote kuhusu vitendo vya ubakaji. Umoja wa Mataifa uliambiwa kuhusu jambo hilo na shirika la misaada siku 10 baadaye.
Akizungumza na waandishi wa habari kutoka Goma, Bw. Meece amesema wanavijiji huenda waliogopa kusema jambo hilo kwa kuhofia waasi hao, au kutokana na kuona aibu kutokana na unyanyapaa wa kubakwa uliopo nchini humo.

Ubakaji DRC


'Watoto wa vita' Yatima na watoto waliopotea katika makao Goma.
Bw. Meece amesema Umoja wa Mataifa sasa unafanya uchunguzi wa jinsi ya kurekebisha uhusiano na wakazi wa huko.
Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, bado linakabiliwa na ghasia zinazofanywa na waasi, licha ya kumalizika kwa vita vilivyodumu kwa miaka mitano, mwaka 2003.Majeshi ya kulinda usalama ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakisaidia jitihada za kutokomeza kundi la waasi la FDLR, ambalo viongozi wake wanahusishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. Waasi hao wanafanya harakati zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Muambukiza UKIMWI aepuka jela Ujerumani

Nadja Benaissa
Nadja Benaissa
Mwanamziki wa miondoko ya Pop wa Ujerumani anayeishi na virusi vya Ukimwi anayetuhumiwa kumwambukiza mpenzi wake virusi vya ugonjwa huo amepewa kifungo cha nje cha miaka miwili.
Nadja Benaissa, mwenye umri wa miaka 28, alikiri kufanya mapenzi bila kujikinga na kuficha hali yake ya kiafya, lakini amekana kumwambukiza mwenzake kwa makusudi.
Mwimbaji huyo wa kundi la No Angels alikutwa na kosa la kusababisha madhara kwa mtu mmoja, na makosa mawili ya kujaribu kumdhuru mtu.
Katika kesi hiyo alisema, " anaomba radhi kwa moyo wake wote."
'Uwoga'
Bi Benaissa alifanya mapenzi na watu watatu bila ya kuwaambia kuwa ameathirika. Mmoja wao alithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.
Bi Benaissa aliiambia mahakama kwamba hakumwambia mtu yeyote kuhusu maradhi yake kwasababu alikuwa na wasiwasi wa matokeo hasa ya kazi yake, ambapo alisema lilikuwa ni "suala la uwoga."
Alidai aliambiwa na madaktari kuwa hatari ya kumwambukiza mtu virusi ni "sawa na kuwa haiwezekani."
Bi Benaissa alikamatwa mjini Frankfurt mwaka jana, muda mfupi kabla ya kushiriki kwenye tamasha, na kuwekwa kizuizini kwa siku 10.
Kundi la No Angels liliundwa mwaka 2000 katika kipindi cha kimataifa cha televisheni cha Popstars, kabla ya kurekodi mfululizo wa nyimbo maarufu na kuibuka kundi lenye mafanikio makubwa Ujerumani.
Mwaka 2007 waliibuka upya na kushindana katika mashindano ya Eurovision mwaka 2008, na kuchukua nafasi ya 23.

Wednesday, August 25, 2010

SIJAFUNGA MIMI KAFUNGA MSHAMBULIAJI!!!


Beki wa klabu ya Man City Micah Lincoln Richards amemaliza mzizi wa fitna miongoni mwa waandishi wa habari za michezo toka nchini Uingereza kufuatia bao la pili la klabu hiyo katika mchezo wa jana dhidi ya Liverpool.
Micah Lincoln Richards amemaliza mzizi huo wa fitna kufuatua utata kuzuka miongoni mwa waandihi hao ambao walikua wakijiuliza ni nani mfungaji wa bao hilo, ambapo miongoni mwao walisikika wakisema mpira wa kichwa uliopigwa na beki huyo haukuguswa na Carlos Teves kabla haujaingia ndani ya kimia.
Alipohijiwa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 alisema bao la pili limefungwa na Carlos Teves huku akitoa sababu kwamba mchezaji huyo ni mshambuliaji hivyo kazi yake ni kufunga mabao.
Micah Lincoln Richards pia ameonyesha kufurahishwa na usajili uliofanywa klabuni hapo kwa kusema wachezaji waliosajiliwa wameonyesha uwezo mkubwa wa kukisaidia kikosi cha Man City kupata ushindi wao wa kwanza wa ligi msimu huu mbele ya Liverpool.
Katika mchezo huo wa jana Man City walifanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri yaliyofungwa na Gareth Barry 13 pamoja na Carlos Tévez 52 na 67.