SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, November 5, 2010

MATOKEOA YA URAIS: JK ATANGAZWA MSHINDI KWA ASILIMIA 61.17

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame amkikabidhi cheti Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumtangaza kushinda katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka huu.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame akimpongeza JK muda mfupi baada ya kumtangaza kushinda katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka huu.


Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha cheti cha ushindi katika mbio za urais mwaka 2010 muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza kuwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar
Mgombea urais kwa tiketi ya CUF Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza Dr.Jakaya Kikwete kuwa mshindi katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010.
Rais wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akimpongeza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kutmangaza Rais Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo mchana. Picha na Freddy Maro.


MATOKEO RASMI YALIYOTANGAZWA LEO
1. KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO: 96, 933 (1.12%)

2. KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM: 5,276,827 (61.17%)

3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA: 2,271,941 (26.34%)

4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF: 695,667 (8.067%)

5. RUNGWE HASHIM SPUNDA/NCCR-MAGEUZI: 26,388 (0.31%)

6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT/TLP:17,482 (0.20%) 
7. DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA/UPDP: 13,176 (0.15%)
----------------------------------------------
WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303
WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)
KULA HALALI ZILIZOPIGWA: 8,398,394
KURA ZILIZOHARIBIKA 227,889 (2.64)

0 comments:

Post a Comment