SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, July 12, 2010

Uhispania Mabingwa wa Kombe La Dunia 2010

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini pamoja na Rais wa Fifa,Sepp Blatta wakiwa na mabingwa wapya wa Dunia mara baada ya kuwakabidhi kikombe chao cha ubingwa walioupata kwa kuitungua timu ya Taifa ya Uholanzi bao 1-0 lililofungwa na mchezaji Andres Iniesta dakika nne tu kabla ya mechi         kumalizika.Torres na wenzake wakifurahia ubingwa huo.

Uhispania, washindi wa Kombe la Dunia 2010
Mfungaji wa goli pekee lililoipa ubingwa timu ya Taifa ya Hispania,Andres Iniesta akishangilia goli lake muhimu lililoipatia ubingwa timu ya Taifa ya Hispania.
 Andres Iniesta alifunga goli dakika nne kabla ya muda ulioongezwa kumalizika na kusababisha Uhispania kupata ushindi wao kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia kwa bao 1-0 dhidi ya Uholanzi.
Kombe hili pia limekuwa na maajabu ya "Pweza" jina lake "PAUL"ambaye ametabiri kwa usahihi matokeo ya mechi zaidi ya nane za kombe la dunia ikiwa ni pamoja na mechi ya jana, ambayo alitabiri kuwa Hispania itashinda.

0 comments:

Post a Comment