SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, July 11, 2010

 JK apiga kura Kizota leo

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume wakitoka nje wa ukumbi wa mkutano wa Kizota wakati wa mapumziko mafupi ili kutoa nafasi ya kura kuhesabiwa.
Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura ya kumthibitisha kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi wakati wa mkutano mkuu unaofanyika katika ukumbi wa Kizota mjini Dodoma leo asubuhi.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Bi.Ashura Abeid Faraji kutoka Zanzibar akimsalimia mwenyekiti wa CCM , Rais Jakaya Mrisho Kikwete nje ya ukumbi wa mikutano wa Kizota wakati wa mkutano mkuu wa CCM unaofanyika mjini Dodoma.
Wahudumu wakibeba visanduku vya kura tayari kwenda kuhesabiwa baada ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kupiga kura leo mchana
(picha na Freddy Maro)

0 comments:

Post a Comment