SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, July 12, 2010



Hongera kwa Wagombea
Mama Salma Kikwete akimpongeza mai hazbendi wake Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kwa zaidi ya asilimia 99 kuwa mgombea pekee wa Urais kwa tiketi ya CCM usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Kizota mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein(kushoto) na mgombea mwenza bara Dr.Mohamed Gharib Bilal kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pampja na Rais wa Zanzibar Amani Abedi Karume(kulia) pamoja na Makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein(wapili kushoto), pampja na mgombea mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal mwishoni mwa mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Picha na Freddy Maro
****************************  
Dakta Gharib Bilal ateuliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais Jakaya Kikwete JK AKIMPONGEZA DK. GHALIB BILAL
DK. GHALIB BILALI AKIPONGEZWA NA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU. KATI NI MH. FREDERICK SUMAYE
Dokta Gharib Bilal aliyekuwa mgombea wa kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya CCM katika uchaguzi wa urais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi mstaafu, ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu ujao. Kwa utaratibu huo Dakta Bilal atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo CCM itaibuka na ushindi katika uchaguzi ujao wa Oktoba 31. Kabla ya kutamkwa kwa jina la Dk. Bilal jana saa tatu usiku, kura za ndiyo zilipigwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, uliokuwa ukifanyika mjini Dodoma kumthibitisha Kikwete kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Akitangaza matokeo ya kura hizo jana jioni, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume, alisema asilimia 99.16 ya wajumbe walipiga kura za Ndiyo kumthibitisha Rais Kikwete kuwa mgombea wa urais wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

0 comments:

Post a Comment