SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, July 12, 2010

60 wauawa katika milipuko ya bomu Uganda

Waathiriwa wa mlipuko nchini Uganda
Milipuko imetokea Kampala, mji mkuu wa Uganda, ikilenga mashabiki wa soka waliokuwa wakitazama mechi ya fainali ya Kombe la Dunia katika televisheni.
Idadi kamili ya waliofariki bado haijulikani japo awali miili 23 ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Duru zinaarifu kuwa idadi hiyo inahofiwa kufikia zaidi ya watu 60.
Mkuu wa polisi nchini humo, Kale Kaihura, amesema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa milipuko hiyo iliyotokea katika mikahawa ya vyakula na pombe ilinuiwa kusababisha maafa zaidi.
Shaka kuu imetiliwa kikundi cha wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia ambako Uganda imetuma majeshi yake kusaidia katika shughuli ya amani chini ya muungano wa Afrika.
********************* 
Liwalo na liwe, sitajiuzulu - Naoto Kan

Naoto Kan asema hatajiuzulu
Waziri mkuu wa Japan Naoto Kan amesema kuwa hatajiuzulu licha ya kushindwa kwa serikali yake katika uchaguzi wa bunge la uakilishi.
Matokeo ya awali yameonyesha kuwa serikali hiyo ya mseto imepoteza viti vingi katika uchaguzi huo na hivyo kutoa wasiwasi wa kuhujumiwa na upinzani.
Alilaumu matokeo hayo kwa pendekezo alilotoa awali la kuongeza ushuru wa mauzo nchini humo.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa matokeo hayo yameonyesha changamoto kubwa kwa serikali hiyo iliyochukua madaraka mwaka jana chini ya chama cha Democratic kwa kuahidi mabadiliko ya utawala.
bbc swahili

0 comments:

Post a Comment