SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 8, 2010

Mkutano wa ECOWAS kuhusu usalama na usuluhishi wa mgogoro wafanyika nchini Nigeria

Abuja
Mkutano wa 27 wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kuhusu usalama na usuluhishi wa mgogoro unaendelea huko Abuja, Nigeria.
Kwenye mkutano huo wa siku 2 mwenyekiti wa kamati ya ECOWAS Bw. James Victor Gbeho amesema, eneo la Afrika magharibi liko kwenye kipindi muhimu cha mabadiliko ya mamlaka, ambapo hali ya usalama wa eneo hilo inakabiliwa na changamoto nyingi, kwa hiyo mkutano huo utazihimiza Niger, Guinea, Guinea Bissau na Togo zitulize migogoro yao, na kuihimiza Cote d'Ivoire ifanye uchaguzi mkuu, ambao umeahirishwa mara nyingi.
Kwenye mkutano huo mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Afria magharibi Bw. Said Djinnit amesema, Umoja wa Mataifa utaimarisha ushirikiano kati yake na ECOWAS, na kuhimiza amani ya kudumu na maendeleo katika eneo la Afrika magharibi.

Hali ya kuenea kwa sumu ya risasi nchini Nigeria yadhibitiwa Zamfara
Naibu waziri mkuu wa afya wa Nigeria Bw. Suleiman Bello tarehe 7 alisema, hali ya kuenea kwa sumu ya risasi nchini humo hivi sasa imeshadhibitiwa.
Bw. Bello alisema, watu waliopatwa sumu hiyo wanapewa matibabu, na kazi za kuondoa sumu hiyo kwenye sehemu zilizochafuliwa zinaendelea, alitaka wananchi wa nchi hiyo wasiwe na wasiwasi.
Tangu mwezi Januari mwaka huu, hali ya kuenea kwa sumu ya risasi ilitokea kwenye jimbo la Zamfara lililoko kaskazini mwa Nigeria, na mpaka sasa watu 355 waliripotiwa kupatwa na sumu hiyo, na watu 163 kati yao walikufa, wakiwemo watoto 111. watoto wengine zaidi ya mia moja bado wanapewa matibabu.
china radio international

0 comments:

Post a Comment