SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 30, 2010

Swizz Beatz
Swizz Beatz Owes $650,000 In Unpaid Taxes
Swizz Beatz's financial woes are spiraling - the music producer has been hit with a demand for allegedly unpaid taxes amounting to more than $650,000.
A $652,727 lien for delinquent taxes in 2008 was filed against the star in New York on June 3rd. Swiss Beatz, real name Kasseem Dean, has previously seen a string of liens filed against him and his ex-wife, Mashonda, in New York, Georgia and California - and their debts are said to stand at around $2.2 million.
However, he is determined to clear the debt and is negotiating a financial plan with officials to pay back the money. A lawyer for the rapper tells New York Post gossip column Page Six, "We have been discussing the issue with the government for years and are currently negotiating an amicable resolution of the dispute."
The filing of the most recent legal papers came just days after Swizz Beatz, who is expecting a baby with fiancée Alicia Keys later this year, settled a dispute with Mashonda over missing child support payments. He paid out $334,000 in back alimony and child support responsibilities for the former couple's three-year-old son, Kasseem Jr., in May.
Larry King Announces The End Of 'Larry King Live'
 Veteran TV newsman Larry King has confirmed reports he's ending his 25-year run as the host of CNN talk show "Larry King Live."
King took to Twitter on Tuesday to tell fans the news, explaining he had asked the cable network's executives if he could close his popular show later this year, and they agreed.
In the statement, he said, "25 years ago, I sat across this table from New York Governor Mario Cuomo for the first broadcast of 'Larry King Live.' Now, decades later, I talked to the guys here at CNN and I told them I would like to end 'Larry King Live,' the nightly show, this fall and CNN has graciously accepted, giving me more time for my wife and I to get to the kids' little league games."
King and his wife Shawn are currently trying to save their marriage after both filed for divorce earlier this year.
The newsman insists he's not retiring completely, adding, "I'll still be a part of the CNN family, hosting several Larry King specials on major national and international subjects. I'm incredibly proud that we recently made the Guinness Book of World Records for having the longest running show with the same host in the same time slot. With this chapter closing I'm looking forward to the future and what my next chapter will bring, but for now it's time to hang up my nightly suspenders."
British journalist-turned-TV personality Piers Morgan has been hotly tipped to take over King's nightly time spot on CNN in America.
Kiongozi wa FNL Agathon Rwasa mafichoni
Kiongozi wa chama cha FNL Agathon Rwasa

             Kiongozi wa chama cha FNL Agathon Rwasa
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi ambaye zamani alikuwa kiongozi wa kundi la waasi Agathon Rwasa ,amethibitisha kuwa yuko mafichoni.
Kwenye ujumbe uliorekodiwa na kutumwa kwa radio moja nchini humo, Bw Rwasa amesema amejificha kwa kuhofia usalama wake.
Aliondoka nyumbani kwake wiki moja iliyopita kabla ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatatu huku mgombea pekee akiwa Rais wa sasa Pierre Nkurunziza .
Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza kufanyika nchini humo,tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 12.
Wanadiplomasia wameonya kuwa huenda nchi hiyo ikarejea katika hali ya mzozo wa kivita.
Waandishi wa habari wanasema idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo wa urais, ilikuwa ndogo ikilinganishwa na uchaguzi wa mikoa uliofanyika mwezi uliopita.
"Wananitafuta kwasababu nilisema ukweli,nilisema wazi kuwa sitakubali matokeo ya uchaguzi wa mikoa, walitaka kunikamata na nilipopata fununu nikaamua kukimbia"
Kiongozi wa chama cha FNL Agathon Rwasa
Vyama vitano vya upinzani vilidai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi wa kura, na vikajiondoa katika uchaguzi wa urais.
Bw Rwasa, ambaye alitia saini mkataba wa amani mwaka jana, hakusema yuko wapi lakini inaripotiwa kuwa yuko katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wakati alipotoweka kwa mara ya kwanza ,chama chake kilisema alikuwa ''likizoni''.
Bw Rwasa na Rais Nkurunziza ,waliongoza makundi ya waasi wa Kihutu kupigana na jeshi ambalo lilikuwa likiongozwa na Watutsi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Bw Rwasa, alikataa kuhusika katika mpango wa kumaliza mapigano baada ya makundi yaliyokuwa yakizozana kuamua kuunda serikali ya muungano na baadaye uchaguzi ukafuata mwaka 2005.
Aliongoza kundi la National Liberation Forces (FNL) kusalimisha silaha mwezi Aprili mwaka 2009, na anaaminika kuwa mshindani mkubwa wa Rais Nkurunziza.
Watu wapatao 300,000 walikufa wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
MAMA SALMA AZINDUA UPANUZI WA UKARABATI WA SEKONDARI YA TABORA WASICHANA


Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiwahutubia mamia ya wanafunzi wa shule za Sekondari za Mko wa Tabora wavulana na wasichana na Mirambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi na ukarabati wa shule ya sekondari Tabora wasichana uliofanyika jana mkoani humo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi awamu ya kwanza ya ukarabati na upanuzi  wa shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora unaofanywa kwa hisani ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa(UNHCR) uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.7. Kushoto Mkuu wa Shule hiyo Ms Agness Mlelwa (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mama Salma Kikwete akitembelea moja ya bweni lililokarabatiwa katika shule ya wasichana ya Tabora baada ya kuzindua mradi wa ukarabati na upanuzi wa shule hiyo.
 
 
 
 
 
  
  
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono kuwaaga wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora (wavulana na wasichana) na Milambo walihudhuria sherehe za upanuzi na ukarabati wa shule ya sekondari ya wasichana Tabora jana.
Saba Saba Bongo

Lango kuu
Wadada wa tigo huduma kwa wateja wakishoo love leo katika banda lao lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya biashara vya Mwalimu J.K. Nyerere,kilwa rodi jijini Dar.
Wadau wa tigo,toka shoto ni Noel Nchimbi,Claudia Samuel,Doreen Muganga na Fransisca African wakiwakilisha ndani ya viwanja vya saba saba leo.
Pendo na Pauline
Mwanalibeneke Muhidin Sufiani akipiga stori mbili tatu na vimwana wa Sasatel
Banda la TTCL likimaliziwa kupigwa kufanyiwa marekebisho.Banda la NSSF.
Banda la Benki Kuu na TBC.
Banda la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Askari wa kikosi cha Farasi akipiga misele ndani ya viwanja vya saba saba
Banda la Home Shopping Centre.
Vijana wa Scout nao pia hawako nyuma. Mama Lishe wakiendeleza libeneke kwa kuuza vyakula uwanjani hapo.
Israel kuongeza uchunguzi juu ya shambulio la meli za misaada.
  Waziri mkuu wa Usrael Benjamin Netanyahu anaweza pia kuitwa na jopo
 kutoa ushahidi wake juu ya shambulio dhidi ya meli za misaada 
zilizokuwa zikielekea Gaza.
Waziri mkuu wa Usrael Benjamin Netanyahu anaweza pia kuitwa na jopo kutoa ushahidi wake juu ya shambulio dhidi ya meli za misaada zilizokuwa zikielekea Gaza.
Israel inaweza kuongeza jukumu la uchunguzi wake juu ya shambulio lililofanywa dhidi ya meli zilizokuwa zikipeleka misaada katika ukanda wa Gaza, kwa kuruhusu jopo lililoundwa kuchunguza kisa hicho kuwahoji mashahidi.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Israel, imesema kiongozi wa jopo hilo la uchunguzi Jaji Jacob Turkel amewasilisha ombi kupanuliwa kwa uchunguzi huo kwa kuwawezesha mashahidi kutoa ushahidi wao baada ya kula kiapo.
Jopo hilo linaloongozwa na Jacob Turkel, Jaji mstaafu wa mahakama kuu ya Israel, lilianza uchunguzi wake siku ya Jumatatu na kwamba Waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu  na waziri wake wa ulinzi wanaweza pia kuitwa kutoa ushahidi wao kuhusiana na tukio hilo lililotokea Mei 31, ambapo raia tisa wa Uturuki waliuawa.
Kiongozi huyo wa jopo, amesema juukumu lao ni kuchunguza kama kuzingira kulikofanywa na jeshi la majini la Israel na msafara wa meli za misaada uliendana na sheria za kimataifa na pia uchunguzi ya kitendo cha waratibu wa msafara wa meli na washiriki wake.
Miongomi mwa wanaounda jopo hilo ni pamoja na mtaalamu wa Israel wa masuala ya sheria za kimataifa, mkuu wa zamani wa jeshi, pamoja na waangalizi wawili wa kigeni, ambao ni mshindi wa tuzo ya Nobel na mwanasheria wa Canada Ken Watkin, pamoja na David Trimble, mwanasiasa kutoka Ireland ya kaskazini, ambaye alisema kuwa wote wamejidhatiti kuona uchunguzi unakuwa wa kuwajibika na kutumai kuwa utaweza hatimaye kutoa mchango wa maana kwa amani.
Tukio hilo lilitia doa uhusiano kati ya Israel na Uturuki iliyo nchi ya kiislamu ambayo ni mshirika wake muhimu, ambapo toka kutokea kwa shambulio hilo ili muita nyumbani balozi wake pamoja na kufuta mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyokuwa yakifanywa na taifa hilo la kiyahudi.
Israel iliamua kufanya uchunguzi huo baada ya nchi na jumuia mbalimbali duniani kulishutumu shambulio hilo, kwa kufikiria kwamba itapinga pendekezo la Umoja wa Mataifa la kufanyika kwa uchunguzi wa kimataifa.
Shambulio hilo lililofanya na makomando wa Israel, matokeo yake liliangazia vizuizi vilivyowekwa na Israel katika ukanda wa Gaza ambao unadhibitiwa na chama cha Hamas, hali ambayo pia ilisababisha kulegezwa kwa vizuizi hivyo.
Ikijitetea Israel ilisema kuwa makomando wake ambao walivamia moja ya meli zilizofadhiliwa na Uturuki kupeleka misaada Gaza, walikuwa wakitekeleza vizuizi vilivyowekwa kwa ajili ya kuzuia silaha zisiwafikie wapiganaji wakiislamu walioko katika eneo hilo na kwamba walifyatua risasi ili kujihami baada ya wanaharakati waliokuwa ndani ya meli hiyo kuwashambulia visu na marungu.
Mwandishi: Halima Nyanza(Reuters)
Libeneke la JK la Uchaguzi 2010


Kikosi kazi cha kampeni za JK kugombea Urais kimeanzisha libeneke la tweeter na blogger kwa ajili ya mawasiliano ya kisasa kwa wadau. Hebu tembelea libeneke hizo:
Mkulo katika mkutano wa ECOSOC NewYork leo
WAZIRI WA FEDHA AKICHANGIA MJADALA KISERA KUHUSU WAJIBIKAJI NA UWAZI KATIKA USHIRIKIANO WA MAENDELEO; NAMNA YA KUJENGA USHIRIKIANO ULIO SAWA MIONGONI MWA WADAU MBALIMBALI. MJADALA HUO UMEFANYIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI, DK. SERVACIUS LIKWELILE AKIFUATILIA MAJADILIANO

 WAZIRI MKULO AKIBADILISHANA MAWAZO NA WAJUMBE MBALIMBALI WA KIKAO CHA KILELE CHA KAMATI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII YA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA( ECOSOC). Kwa habari zaidi bofya: http://issamichuzi.blogspot.com/
Wanajeshi wawili wapoteza maisha katika ajali ya ndege

sehemu ya ndege iliyopata ajali baada ya kutua barabarani kwa dharura na kugonga basi la watalii ambalo linaonekana juu kushoto likiwa limeanguka
askari wa jeshi la ulinzi na polisi wakiwa eneo la tukio
msururu wa magari yaliyokuwa barabarani
Askari wawili ambao ni marubani wa Jeshi la Wananchi Tanzania wa Kambi ya Ngerengere ya Morogoro, wamekufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kutua barabarani kwa dharura na kugonga gari la watalii na kupinduka jana katika eneo lijulikanalo kama Zimbabwe katika kijiji cha Manga wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga.
Katika basi la watalii inasemekana kulikuwa na watu 24 ambao 19 kati yao ni raia kutoka Uholanzi, wanne kutoka Kenya na mmoja Mtanzania. Wote walinusurika kufa.
Inasemekana kuwa marubani hao walikuwa katika mazoezi ya kawaida katika anga ya eneo hilo, na kwamba wakati ikiwa angani ndege ilipata hitilafu ndipo rubani akaamua atue barabarani ili kuokoa maisha yao, kabla gari hiyo ikiwa kwenye mwendo mkali iliigonga.
Ndege hiyo ndogo ya JWTZ yenye namba F59119 ilikuwa inatumika katika mafunzo ya kijeshi. Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga, Afande Jafari Mohammedi, aliwataja waliokufa kuwa ni rubani wa ndege hiyo Meja Kathbet Leguna (41) na mwanafunzi wake Luteni Andrew Yohana Kijangwa (31).
Taarifa zinasema Meja Leguna alikuwa ni mwalimu wa mafunzo ya ndege za kivita katika kikosi hicho cha Ngerengere na alikuwa anamfundisha urubani Luteni Kijanga. 
issamichuzi blog
Lil Wayne Writes Personal Thank You Notes To Fans
Wayne also heaped praise on his artists Drake and Nicki Minaj, who he proclaims "made me proud" at Sunday night's BET Awards, with the stars claiming the Best Male Hip-Hop Artist and Best Female Hip-Hop Artist titles, respectively. The post follows Wayne's Mother's Day tribute, posted on his official blog last month, and an introductory note in April, when he first launched the site from behind bars to communicate with fans.
Lil Wayne
                              ****************************
Enrique Iglesias Blames Album For Missing World Cup
Soccer-loving Enrique Iglesias is devastated his new album release was scheduled at the same time as the World Cup - because the singer's busy promotion schedule means he is missing all of the crucial games.
The Latino star's ninth studio record, Euphoria, hits stores next week and he has been working hard giving interviews and making TV appearances to plug his new music.
However, Iglesias is not happy about the timing of the release - as he has been struggling to follow his beloved sport as the international tournament takes place in South Africa.
He says, "It is the only thing I dislike about this album. It is taking away from the football. It's not like I can record the games either. The World Cup is just the one event you have got to watch live."
Enrique Iglesias
Ujerumani leo kumpata rais mpya
Mgombea urais wa Ujerumani kwa tiketi ya CDU/FDP Christian Wulff
Mgombea urais wa Ujerumani kwa tiketi ya CDU/FDP Christian Wulff
Rais mpya wa Ujerumani anachaguliwa , leo na baraza maalumu la shirikisho lenye wajumbe 1244.
Atakaechaguliwa  leo atachukua nafasi ya rais wa hapo awali, Horst Köhler,   aliejiuzulu mwezi uliopita.
Wanagombea wadhifa  huo ni  waziri mkuu wa sasa  wa  jimbo la  Lower Saxony,  Chrsitian Wullf, na aliekuwa   anasimamia  idara kuu  ya nyaraka za  siri za  idara ya ujasusi  wa ndani  ya Ujerumani Masharrikiya hapo  awali, Bwana Joachim Gauck,  mwenye umri wa miaka 70.
Waziri Mkuu Christiana  Wullf  ni mjumbe wa vyama vya   serikali  ya mseto  na  CDU   na chama  cha Waliberali, FDP. Vyama hivyo  kwa pamoja na chama ndugu  cha CSU vitawapeleka wajaumbe    644 yaani  21  zaidi  ya  wingi unaohitajika ili  mjumbe  wao ashinde .
Mgombea mwingine, Joachim Gauck,  ni mgombea   anaeungwa mkono  na vyama vya upinzani-SDP na  chama cha  kijani. Kwa pamoja vyama  hivyo  vitawapeleka  wajumbe 462.
Lakini  Gauck mwenyewe  hayumo katika chama chochote .
Kwa hiyo, hesabu zinaonyesha kwamba mgombea  wa  vyama  vya serikali  anatarajiwa kupita katika  kinyang'anyiro cha leo.
Wagombe  hao ni  watu  wanaotofautiana kwa namna nyingi .
Kwanza  kabisa mgombea   wa  vyama vinavyoongoza  serikali, Christian  Wullf, amekulia katika upande wa Magharibi wa Ujerumani. Mgombea  wa  vyama vya upinzani, Joachim  Gauck, alikuwa  mwanaharakati  wa kupigania   uhuru  katika  sehemu ambayo  hapo zamani  ilikuwa inaitwa   Ujerumani  ya mashariki.
Juu  ya  hayo   mgombea   huyo  amesema:
 Joachim 
Gauck,
  Joachim Gauck,
 "Tulikuwa  Mashariki  kwa  sababu  tulilazimishwa .Lakini katika  fikira  zetu tulikuwa na wazo la uhuru ambao   haukuwapo  katika  upande   wa Mashariki, lakini ulistawi katika Magharibi."
Joachim   Gauck,  asiyekuwa  na  chama chochote,  hana matatizo na  wahafidhina na Waliberali.  Kwani  angeliweza  kuwa  mgombea wa  vyama   vya serikali na vyama vya   upinzani kadhalika.
Vyama  vya upinzani vilimpendekeza  Gauck. Kansela wa  Ujerumani alipewa  taarifa  lakini alilikataa  pendekezo   hilo japo   anamthamini sana  Bwana  Gauck.
Mgombe  mwingine Christian   Wullf aliependekezwa na  vyama vinavyoingoza serikali .  Christian  Wullf alianza  kuvuta  pumzi ya  uhuru  tokea siku  ya  kwanza  alipozaliwa katika Ujerumani magharibi.
Wullf  mwenyewe  anasema.
´´Muhimu ni  kwamba natoka katika nasaba   ya kati   na nadhamiria  kubakia  katika nasaba  hiyo. Kwangu  ni jambo la  kuvutia ikiwa  rais atakaefuatia atakuwa  mtu  anaetoka  katika rika la kati. Mtu mwenye uzoefu wa kuleta pamoja kazi na majukumu  ya familia´´.
Christiana  Wullf  ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa  leo  kuwa  rais mpya  wa  shirikisho la jamhuri  ya  Ujerumani.
Amesema akichaguliwa   ataendeleza   sera  za Horst  Köhler, rais  wa  hapo awali  alieliweka bara  la  afrika  moyoni.
Köhler alizetembelea  nchi  kadhaa  za Afrika kuhudhuria vikao   na  ushiriki  katika utekelezaji wa miradi  ya  maendeleo.
Mwanasiasaa huyo amesema  kwake  ni wazi kabisa kwamba Ujerumani   inapaswa kuuendeleza   uhusiano na   Afrika ulioanzishwa na rais   wa hapo awali-
Mwandishi/ Martin Beutler/ZAR/
Paraguay yaishinda Japan kwa penalti
Paraguay dhidi ya Japan
Paraguay iliishinda Japan kwa penalti tano kwa tatu
Paraguay imeshinda pambano la kwanza kwa mikwaju ya penalti katika michuano ya Kombe la Dunia ya 2010 na kufaulu kuingia robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake ambapo watacheza na mshindi kati ya Hispania na Ureno.
Paraguay ilifunga mikwaju yake yote mitano baada ya pambano lake na Japan kumalizika bila ya kufungana mwishoni mwa muda wa ziada.
Pambano hilo lilikosa msisimko wakati kila upande ukijidhatiti kulinda lango lao.
Matumaini ya Japan yalitoweka baada ya Yuichi Komano kugonga mwamba.
Paraguay iliibuka na ushindi wa penalti tano kwa tatu.
Kushindwa kwa Japan kulimaanisha bara la Asia halitakuwa na mwakilishi katika duru ya robo fainali.
*********************************
Uhispania yaingia robofainali
 
David Villa akishangilia bao aliloifungia Uhispania dhidi ya Ureno David Villa akishangilia bao aliloifungia Uhispania dhidi ya Ureno
Mabingwa Ulaya Uhispania imekuwa nchi ya mwisho kufuzu kwa robofainali ya michuano hiyo ya kombe la dunia baada ya kuichapa Ureno bao 1-0 katika mechi iliyokuwa kali na ngumu.
Alikuwa ni mshambuliaji hatari wa timu hiyo David Villa aliyewarejesha nyumbani Ronaldo na wenzake, kwa bao la dakika ya 63 na kufufua matumaini kwa Uhispania kuweza kutwaa ubingwa huo.Uhispania ni miongoni mwa timu ambazo zinapigiwa sana upatu kushinda taji hilo, hata mfalme wa kandanda duniani Pele ni miongoni mwa wale wanapiga upatu huo.
Timu nyingine zilizofuzu kwa robofainali ni pamoja na  Paraguay, Ujerumani, Ghana, Brazil, Argentina, Uholanzi na Uruguay.
Paruguay ilifanikiwa kuingia hatua hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya kabumbu la nchi hiyo baada ya kuitoa Japan kwa changamoto ya mikwaju ya penalti, kufuatia kila mtu kutoweza kuufumania mlango wa mwenzie hata pale mpambano uliporefushwa muda.
Mshambuliaji nyota wa timu hiyo Santa Cruz alisema kuwa kufuzu kwa hatua hiyo, ni ndoto aliyokuwa akiiota na kwamba sasa imekuwa kweli.Amesema kwa kipindi cha miaka minne iliyopita wamekuwa wakiota fainali za mwaka huu kufanya vyema.
Mechi mbili za kwanza za  robofainali zitakuwa Ijumaa ijayo kwa pambano kati ya Brazil na Uholanzi na baadaye Ghana na Uruguay. Jumamosi itakuwa zamu ya Ujerumani kuumana na Argentina na hatimaye Uhispania kucheza na Paraguay.
Oprah Winfrey, atisha kwa utajiri
Oprah Winfrey
Oprah Winfrey
Mtangazaji wa televisheni Marekani Oprah Winfrey ametajwa kuwa mtu mwenye mvuto na utajiri mkubwa duniani kupitia jarida la Forbes.
Winfrey amempiku muigizaji wa filamu Angelina Jolie kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya watu 100 mashuhuri kwa mwaka katika jarida la Forbes.
Nafasi hizo hupangwa kutokana na mapato ya mtu na kiwango anachoonekana kwenye vyombo vya habari.
Muimbaji Beyonce, amechukua nafasi ya pili, huku mkurugenzi wa filamu James Cameron akiingia tena kwenye chati na kuchukua nafasi ya tatu kufuatia mafanikio yake ya filamu ya Avatar.
Lady Gaga amepanda katika nafasi mpya ya orodha hizo akiwa nafasi ya nne.
Kama ilivyo kwa Beyonce, mapato yake na taarifa za maisha yake kwa ufupi zimeongezeka katika miaka 12 iliyopita kutokana na ziara zake duniani na mikataba mbalimbali.
Jolie, wakati huo huo, ameteleza kutoka nafasi ya juu hadi kufikia nafasi ya 18.
Nyota wa gofu aliyezingirwa na matatizo mengi Tiger Woods ni nyota pekee wa michezo kuwa katika 10 bora.
 Simon Cowell
Simon Cowell










Britney Spears amekuwa wa sita, ikufuatiwa na U2 kwenye nafasi ya saba, wakiwa wamerudi katika 100 bora.
Sandra Bullock, aliyeshinda tuzo ya Oscar mwaka huu ya muigizaji bora wa kike, amepanda chati kwa kasi kutoka nafasi ya 92 hadi kufikia ya nane.
Johnny Depp naye amerudi kwenye chati katika nafasi ya tisa.
Kigogo wa muziki Simon Cowell ameongoza kwa upande wa Uingereza, kwa kupanda nafasi 14 hadi kufikia nambari 11.
Lakini Clodplay imeshuka kwa nafasi 20 na kuwa ya 35 katika mwaka ambao bendi hiyo imepumzika kufanya ziara na kuamua kurejea studio.
Nyota wa Harry Potter Daniel Radcliffe ameshika nafasi ya 82.
Umaarufu wa mfululizo wa Twilight ulionekana kwa kuwepo muigizaji wa kike Kirsten Stewart akiwa nafasi ya 66 na Robert Pattinson nafasi ya 50, wote wakiwa kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza.
Mwaka huu, Forbes iliongeza kigezo cha mtu maarufu kuwepo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook au Twitter, pamoja na mapato na kiwango cha kuonekana kupitia vyombo vya habari.
bbc swahili
'Waliompiga risasi' Nyamwasa, mahakamani
Luteni Jenerali Kayumba Nyamwasa
Luteni Jenerali Kayumba Nyamwasa
Watu wanne wamefikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini wakishtakiwa kwa njama ya kumuua aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini Rwanda Luteni General Kayumba Nyamwasa.
Inafahamika kuwa washukiwa hao wanne waliofikishwa mahakamani ni kutoka Tanzania, Somalia na Msumbiji.
Wote wanakabiliwa na mashataka ya kupanga njama ya mauaji na watafikishwa tena mahakamani Julai 14.
Watu wengine wawili waliokamatwa wakati wa msako mkuu wa polisi waliachiliwa baada ya mashtaka dhidi yao kufutwa.
Luteni Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa ambae alikuwa mwandani mkubwa wa Rais Paul Kagame sasa amegeuka kuwa mkosoaji wake mkubwa na alikwenda kuishi uhamishoni nchini Afrika Kusini mapema mwaka huu.
Serikali ya Rwanda inataka arejeshwe nchini humo kwasababu wanaamini amehusika na mashambulio kadhaa ya maguruneti mjini Kigali mwanzoni mwa mwaka huu.
Jenerali Nyamwasa anaamini serikali ya Rwanda ndiyo iliyohusika na jaribio la kumuua kwa risasi alipokuwa anaelekea nyumbani kwake mjini Johannesburg.
Serikali ya Rwanda inakanusha madai hayo kwa kusema hakuna sababu yoyote ya kumuua.
***************************** 
Waziri Mkuu wa Kenya afanyiwa upasuaji

Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga
Daktari wa Waziri Mkuu Raila Odinga, Oluoch Olunya, amethibitisha kuwa Odinga amefanyiwa upasuaji katika ubongo wake baada ya kubainika kuwa kulikuwepo na shinikizo kubwa katika kichwa chake.
Daktari Olunya aliyekuwa akihutubia waandishi wa habari kuhusiana na kulazwa kwa Waziri Mkuu katika hospitali ya Nairobi, amesema kwamba Waziri Mkuu aliwaambia kuwa aligonga kichwa chake kwenye gari lake majuma matatu yaliyopita.
Mtaalamu huyo wa upasuaji wa ubongo amesema kuwa Odinga anaendelea kupata nafuu na kwamba ameweza kukaa kwa urahisi katika chumba chake hospitalini.
Muuguzi huyo pia amesema Raila ana uchovu mwingi mwilini na anahitaji kulazwa kwa siku tano zijazo.
Awali taarifa kutoka kwa ofisi yake ilidai kwamba alikuwa na uchovu tu.
Bwana Odinga alipelekwa hospitalini Jumatatu mchana baada ya kushiriki mkutano wa kisiasa na madaktari wake waliamuru apumzike hospitalini.
Hadi sasa Raila Odinga mwenye umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mkakamavu.
Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya kiafya.
Taarifa ya kupasualiwa kwake imewashangaza wengi.
Hadi sasa , maswali mengi kuhusu afya ya kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa rais Mwai kibaki.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi. Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya.
bbc swahili

Tuesday, June 29, 2010

Jermaine Jackson Asks Fans To Forgive Chris Brown

 

 Jermaine Jackson was left stunned by Chris Brown's emotional tribute to his brother Michael at the BET Awards on Sunday night, and he's now calling on the R&B star's critics to forgive him for beating up Rihanna.
Brown's career has been in freefall ever since he pleaded guilty to lashing out at Rihanna during a fight last year - radio stations have refused to play his records and the media has slammed his attempts at a comeback - even after countless public apologies online and on TV.
The singer broke down during a rendition of Jackson's "Man in the Mirror" at the BET Awards and the touching cover prompted Jermaine Jackson to stand up for the young star backstage.
Speaking to TV news show "Extra," Jackson said, "He's a human being like all others, we all make mistakes. What he did was wrong. I love Rihanna...I'm one of his biggest fans...We can't condemn him because of what happened. We hope he learns from this."
And Jackson admits he was greatly moved by Brown's tribute to his late sibling: "It was very emotional for me... It was just a spectacular moment. He (Brown) deserves to perform because it's healing for him. How can he learn from his mistakes if you don't give him the chance? He needs that. I support him a thousand percent; I'm not supporting what he did because it was wrong, but, at the same time, we have to give him a chance."

kidemokrasi ya Kongo Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo

Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo
Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo
Wakongomani wajkiandaa kuadhimisha miaka 50 tangu walipojipatia uhuru wao kutoka Ubeligiji
Mfalme Albert II wa Ubeligiji na viongozi wengine wa kimataifa wataadhimisha hapo kesho miaka 50 tangu Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ilipojikomboa toka enzi za ukoloni, ingawa nchi hiyo tajiri kwa maadini ya kila aina imekabwa tangu wakati huo na miongo ya vita, rushwa na umaskini.
Wimbo wa taifa la Kongo ulioimbwa kwa mara ya kwanza June 30 mwaka 1960 unawahimiza wananchi "wanyanyuke na kuijenga nchi kwa amani ili izidi kupendeza kuliko zamani." Matumaini hayo lakini, yametoweka vibaya sana.
Utawala wa miaka 32 wa Mobutu Sese Seko, aliyeingia madarakani mwaka 1965, uliikamua sana Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Ingawa ina akiba kubwa ya madini ya dhahabu, shaba, kobalt na alamasi, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ni moja wapo ya nchi maskini kabisa za dunia, nchi iliyoathirika na vita vya miaka minane vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2003 na kugharimu maisha ya watu wasiopungua milioni tatu.
Miaka minne baada ya Joseph Kabila kuchaguliwa kuwa rais, imesaidia kuleta utulivu kidogo. Hata hivyo, thuluthi mbili ya wakongomani milioni 60 bado wanalazimika kuishi kwa dala moja na senti 25 kwa siku.
Maaskofu wa Kongo wameandika katika risala yao ya pamoja kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kwamba "Ndoto ya Congo inayopendeza imevurugwa".
"Kwa maoni yetu, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imerejea nyuma badala ya kusonga mbele," wamesema wachamungu hao.
Ziara ya mfalme Albert wa Pili ni  ya kwanza kuwahi kufanywa na mfalme wa Ubeligiji katika koloni lake hilo la zamani tangu miaka 25 iliyopita. Atajiunga na katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-Moon,  na rais Jacob Zuma wa Afrika kusini  katika maadhimisho ya uhuru hapo kesho mjini Kinshasa.
Afrika kusini imezitaja sherehe hizo kuwa ni "tukio muhimu kwa bara lote la Afrika. Hata hivyo, viongozi wa Afrika kusini wameelezea wasi wasi wao kwa kushindwa rais Kabila kurejesha utulivu katika eneo la mashariki la nchi hiyo.
Wakinamama 
walioyapa kisogo maskani yao wamewekwa katika kambi ya Kibati  
Wakinamama walioyapa kisogo maskani yao wamewekwa katika kambi ya Kibati
Ziara ya mfalme Albert II na waziri mkuu aliyejiuzulu, Yves Leterme, inabainisha uhusiano ulioanza upya kuwa mzuri kati Ubeligiji na koloni lake hilo la zamani. Uhusiano huo ulipooza kufuatia lawama za rushwa zilizotolewa na waziri mmoja wa Ubeligiji dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Mfalme Albert wa pili na Vyes Leterne hawapangi kusema chochote hadharani wakati wa ziara hiyo ya siku nne iliyoanza jana usiku mjini Kinshasa. Hata katika karamu ya chakula cha usiku hii leo, mfalme Albert II hajapangiwa kuwahutubia viongozi wa mataifa ya kigeni watakaohudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Na hata katika gwaride la kijeshji la kesho, mfalme Albert II anatazamiwa kuvaa suti tuu badala ya sare ya kijeshi, ingawa yeye binafsi ana cheo cha luteni jenerali na naibu amiri jeshi nchini mwake.
Mfalme Albert wa pili atatumia ziara yake hiyo ya siku nne, miongoni mwa mengineyo, kuitembelea hospitali ya mfalme Baudoin pamoja na shule mjini Kinshasa.
 Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Afp,Reuters
Jina la msichana wa miaka 6 wa Kimarekani limo katika orodha ya magaidi
Sample Image   Familia moja ya Ohio nchini Marekani imepigwa na mshangao mkubwa wakati iliposikia kuwa binti mdogo wa miaka 6 wa familia hiyo yumo katika orodha ya magaidi ya Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani.
Hayo yalitokea hivi karibuni wakati familia hiyo ya Dkt. Santhosh Thomas ilipokuwa imepanga kusafiri kwa ndege kutoka Cleveland hadi Minneapolis.
Baada ya kuambiwa kuwa binti yake Alyssa Thomas hawezi kusafiri kwa ndege kwa sababu jina lake limo katika orodha ya magaidi, Dkt. Thomas alisema kwa istihzai kwamba:
"Wamesema, ‘Naam, yumo katika orodha.' Tumeshasikia, sawa, sasa uzito uko wapi? Twambieni tufanye nini ili tumtoe katika orodha hiyo, orodha hiyo siyo kabisa tunayotaka tuwemo ndani yake."
"Hivi hamumuoni hiki ni kibinti cha miaka 6 tu, hakitishii chochote," aliendelea kusema.
Ameongeza kuwa, "Pengine amewahi kumtishia mdogo wake wa kike, lakini sidhani kuwa hilo ni tishio linaloweza kuwashughulisha maafisa wa Wizara ya Usalama wa Ndani."
Hatimaye familia hiyo iliruhusiwa kusafiri kwa ndege kwa sharti kwamba baba wa familia hiyo aende akaripoti kwa Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani.
Baada ya kutokea mashambulizi ya Septemba 11, 2001, George W. Bush Rais wa wakati huo wa Marekani alibuni wizara mpya ya usalama wa ndani na hivyo kuzifanya wizara za nchi hiyo kuwa 14.
http://kiswahili.irib.ir/
  Waziri Mkuu wa Kenya alazwa hospitalini

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga
Hadi sasa Raila Odinga mwenye umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mwenye nguvu.
Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya kimwili.
Kwa hiyo taarifa iliyotolewa hii leo na msemaji wake imewashangaza wengi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo madaktari wameamuru Odinga alazwe hospitalini kwa muda wakisema tu kwamba ana uchovu. Cha kukanganya ni kwamba taarifa hiyo iliwanukuu madaktari hao pia wakisema Odinga ana uwezo wa kufanya kazi kama kawaida ikiwa atajisikia kufanya hivyo. Japo hawatamruhusu kufanya hivyo.
Hadi sasa, maswali mengi kuhusu afya ya kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa Rais Mwai kibaki ambaye baada ya uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi.
Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya.
******************************
Luanda, Angola mji ghali zaidi duniani
Jiji kuu la Angola Luanda


 Utafiti wa kimataifa umebaini kuwa Luanda,mji mkuu wa Aangola ndiyo mji wenye gharama ya juu kwa wataalamu wanaotoka nje na kwenda kufanya kazi huko.
Ripoti iliyonadiwa na kampuni ya masuala ya kifedha ya - Mecer imesema gharama za kupanga nyumba mjini Luanda ni mara dufu ikilinganishwa na jiji la London.
Mji wa Luanda umetajwa kuwa ghali zaidi, ukifuatwa na Tokyo, Ndjamena na Moscow. Bara Afrika lina miji mitatu miongoni mwa miji kumi ambayo ni ghali duniani.
Jiji la Libreville, Gabon likishikilia nafasi ya saba. Uchunguzi ulifanyiwa katika miji 214 katika mabaraza yote matano. Mambo yaliyoangaziwa ni pamoja na gharama za maisha ikiwemo usafiri, chakula, mavazi na starehe.
Tiketi moja ya kutazama filamu mjini Luanda inauzwa dola 13.
Licha ya raia wengi wa Angola na Gabon kuishi katika lindi la umasikini, hali ni tofauti kwa wageni ambapo gharama za maisha miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni za mafuta zinaambatana na usalama wao pamoja na ada ya kuagiza bidhaa kutoka nchi zao.
Gharama za juu zimawalazimu wenyeji wengi kuondoka mijini kwani hawawezi kukimu maisha.
  Milipuko Burundi wakati wa kuhesabiwa kura za urais
Agathon Rwasa, kiongozi wa FNL
Hali ya wasiwasi imetanda mjini Bujumbura,Burundi baada ya mabomu ya guruneti kulipuka katika eneo moja lenye watu wengi jana usiku.
Hakuna aliyekufa kwenye tukio hilo lililotokea wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais inaendelea katika sehemu zengine nchini humo.
Kumekuwa na matukio ya mashambulio ya maguruneti katika siku za hivi karibuni.
Wakati huo huo vyama vya upinzani nchini Burundi vimesema kwamba havitatambua matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu wa jana ambapo rais Pierre Nkurunziza alikuwa mgombea wa pekee.
Wapinzani wa rais Nkurunziza walijiondoa mchuano wa urais wakidai udanganyifu kwenye uchaguzi wa mabaraza.
Muungano wa vyama 12 vya upinzani umesema ni asili mia 30 pekee ya wapiga kura waliojitokeza kwenye zoezi la jana na kuapongeza raia waliosusia uchaguzi huo.
Uchaguzi wa jana ndiyo wa kwanza tangu kundi la mwisho la waasi kujiunga na mpango wa amani na kuitikia kushiriki katika mchakato wa kisiasa.       
                    ******************

Watu 10 Wakamatwa Marekani kwa kuipelelezea Urusi
Washukiwa kadhaa wamefikishwa mahakamani
Watu kumi wamekamatwa nchini Marekani kwa kushukiwa kuwa majasusi wa Urusi.Watu hao walikamatwa kwenye msako uliofanyika katika miji ya NewYork, Boston, New Jersey na Virginia. Mshukiwa mwingine angali anasakwa.
Idara ya Sheria ya Marekani imetoa stakabadhi kudhibitisha kuwa watu iliowazuilia wamekuwa wakikusanya habari za kijasusi a kuzipokeza kwa serikali ya Urusi.
Idara hiyo inasema baada ya uchunguzi wa muda mrefu imewanasa watu hao wakiwemo wanaume wanne na wake zao ambao wamekuwa wakifanya kazi kichichini ili kupata habari muhimu kutoka kwa ofisi za serikali na idara zingine muhimu.
Maafisa hao wa marekani pia wanasema washukiwa hao wamekuwa wakiwasajili watu wengine kwa kazi hiyo ya kijasusi. Mmoja wao anadai kuwa alikuwa ametumwa kuchunguza hasa jinsi serikali ya Rais Obama inavyoiona Urusi kabla ya rais huyo wa Marekani kuzuru urusi.
Habari hizi zimeitia serikali ya Marekani wasiwasi hasa kwa sababu rais Obama amekuwa akijaribu kuoberesha uhusiano wa serikali hiyo na Urusi.
Matukio haya yanarudisha kumbukumbu ya vita baridi kati ya mataifa hayo ambavyo vilidumu kwa zaidi ya miongo mitatu.
Katika miaka ya 60 hadi ile ya 80 karibu ulimwengu mzima ulijipata umenaswa katika vita hivyo baridi na matai. Mataifa hayo mawili yalikuwa yanang'aninia kuwa na ushawishi na hata udhibiti wa karibu mataifa yote duniani.
Na ili kufanikisha kampeni zao serikali ya Marekani na ile ya muungano wa Usovieti ziliwaweka majasusi karibu kote duniani. Na sasa takriban miaka 20 tangu vita hivyo kukoma mbinu hizo hizo bado zinaendelea kutumiwa.
Robo fainali ya kukata na shoka
Brazil imewafunga Chile mabao 3-1
Robo fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini itakutanisha mabingwa mara tano Brazil na Uholanzi siku ya Ijumaa mjini Port Elizabeth, baada ya timu hizo kufuzu kufuatia ushindi wa Jumatatu.
Brazil iliendelea kudhihirisha azma yake ya kulitwaa kombe hilo kwa mara ya sita ilipowafunga Chile mabao 3-0 katika uwanja wa Ellis Park mjini Johannesburg.
Awali katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, Arjen Robben na Wesley Sneider walifunga mabao yaliyoiwezesha Uholanzi kuishinda Slovakia 2-1 na hivyo kujiandikishia nafasi miongoni mwa nane bora.
Mabao ya Brazil dhidi ya Chile yalipatikana kupitia mlinzi Juan aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 38, kabla ya Luis Fabiano kuongeza la pili dakika 4 baadaye.
Robinho alifunga bao la tatu na la ushindi kwa Brazil katika dakika ya 59 kufuatia pasi kutoka Ramires.
Wesley Sneijder
Wesley Sneijder
Uholanzi walionekana kuelekea kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Slovakia hadi muda wa ziada, wakati mlinda mlango Maarten Stekelenburg alipomwangusha Martin Jakubo kwenye eneo la hatari, na hivyo Slovakia wakapata penalti iliyofungwa na Robert Vittek.
Uholanzi haijapata kushinda Kombe la Dunia na imeshafikia hatua ya fainali mwaka 74 na 78, na wakati huu wanajitahidi kutimiza hamu ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.
Robo fainali nyingine siku ya Ijumaa itakuwa kati ya Ghana na Uruguay katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg, hii ikiwa ni mara ya tatu katika historia ya Kombe la Dunia kwa timu kutoka Afrika kufikia hatua ya nane bora.
Siku ya Jumamosi itafanyika robo fainali ya tatu kati ya Ujerumani na Argentina katika uwanja wa Green Point mjini Cape Town.
Timu zitakazochuana kwenye robo fainali ya mwisho zitafahamika Jumanne, baada ya mechi za mwisho za raundi ya pili, Paraguay ikicheza dhidi ya Japan mjini Pretoria huku Uhispania na Ureno zikipambana mjini Cape Town.
**************************** 
Blatter aomba radhi kwa makosa ya waamuzi
Sepp Blatter
Rais wa Fifa, Sepp Blatter
Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter ameomba msamaha kwa ajili ya makosa yaliyofanywa na waamuzi kwenye Kombe la Dunia, ambapo bao llilofungwa na Frank Lampard wa England dhidi ya Ujerumani lilikataliwa, na pia kukubaliwa kwa bao la kuotea lililofungwa na Carloz Tevez wa Argentina dhidi ya Mexico.
Bwana Blatter amesema mdahalo kuhusu haja ya kutumia teknolojia kubaini iwapo mpira umevuka mstari wa goli au la utaanzishwa upya kwenye mkutano wa bodi ya kimataifa ya vyama vya soka utakaofanyika mwezi Julai.
Mkutano wa bodi hiyo uliofanyika mwezi Machi uliamua kukataa kutumika kwa teknolojia hiyo kwenye Kombe la Dunia, kwa tetesi kwamba kusimamisha mechi kwa ajili kuthibitisha kwenye video ikiwa mpira umevuka mstari au la kutaathiri mtiririko wa mchezo na pia kuzinyima timu fursa ya kufunga.
Mjadala kuhusu haja ya kutumika kwa teknolojia hiyo uliibuka tena siku ya Jumapili wakati Ujerumani ilipoifunga England mabao 4-1 mjini Bloemfontein na kuiondoa kwenye mashindano.
Kwenye mechi hiyo, mwamuzi kutoka Uruguay Jorge Larriando na msaidizi wake walikataa kutambua kwamba mpira uliopigwa na Frank Lampard katika dakika ya 38 ulivuka mstari wa lango la Ujerumani na kuingia kabla ya mlinda mlango kuuondosha.
Bao hilo lingeiwezesha England kusawazisha kabla ya mapumziko.
Baadaye siku hiyo katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg kulitokea utata mwingine kwenye mechi kati ya Argentina na Mexico.
Mwamuzi aliruhusu bao la kwanza la Argentina lililofungwa na Carlos Tevez akionekana kuwa ameotea.
Kulitokea mabishano makali uwanjani wakati wa mapumziko baada ya tukio hilo kuonyeshwa tena kwenye skrini kubwa ndani ya uwanja.
Blatter amesema amezungumza na vyama vya soka vya England na Mexico na kuomba msamaha.