Patricia Kimelemeta
SERIKALI imepokea kinyago cha kimakonde kilichopotea katika jumba la makumbusho zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Kinyago
hicho, kilihifadhiwa katika jumba hilo kwa ajili ya kufanya maonyesho
kwa wageni waliokuwa wakitembelea maeneo hayo na baadhi ya watu
walikiiba na kukiuza kwenye mnada.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Maliasili na Utalii ,
Shamsa Mwangunga alisema kinyago hicho, kilinunuliwa na raia ya Uswis
ambaye alikihifadhi kwenye makumbusho yao ya Taifa.
“Kinyago
hiki kilipotea muda mrefu, lakini ushirikiano uliopo baina yetu na
Interpol tumeweza kufanikiwa kukipata, kutokana na hali hiyo
tutaendelea kulinda mali zetu ili kuhakikisha haiziibiwi,”alisema
Mwangunga.
Alilisema kutokana na hali hiyo, serikali ya Uswis ilitoa
ushirikiano na kurudisha kinyago hicho baada ya kubaini kuwa ni cha
wizi, jambo ambalo liliwafanya wakitoe kwenye maonyesho yao.
Mwangunga
alisema serikali itaendelea kutafuta mali zilizopotea katika nchi
nyingine ili wazirudishe na kuzihifadhi kwenye makumbusho kwa ajili ya
kuwaonyesha wageni.
Alisema kutokana na hali hiyo, serikali pia itaendelea kulinda mali zilizopo ili kudhibiti wizi wa aina hiyo.
Mwangunga alisema mchakato uliopo ni kuhakikisha mali hizo, zinaingiza pato la Taifa kwa aina moja au nyingine.
Friday, May 14, 2010
Uswisi yarejesha kinyago kilichoibwa Tanzania
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, May 14, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment