SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, May 31, 2010

Ulimwengu walaani shambulio la Israel dhidi ya msafara wa misaada ya Gaza


Sample Image
Ulimwengu umeendelea kusikitishwa na kulaani mashambulizi ya manowari za kivita za utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya msafara wa kimataifa wa meli zilizobeba misaada ya kibinaadamu kwa ajili Wapalestina wa Ukanda wa Gaza. Watu zaidi ya 20 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo ya kinyama ya jeshi la utawala haramu wa Israel unaoungwa mkono kikamilifu na Marekani. Viongozi wa ngazi za juu wa Iran wameungana na wapenda haki ulimwenguni kote kulani mashambulizi hayo, ambapo nchini Uturuki mamia ya wananchi wa nchi hiyo wameandamana kwenye miji ya Istanbul, Ankara na mkabala na ubalozi wa Israel kulaani tukio hilo huku wakipiga nara za kupinga Israel. Nchi za Lebanon, Iraq, Jordan, Belgium, Pakistan, Ujerumani, Misri, Ufaransa, Qatar na nyinginezo duniani zimelaani vikali mashambulizi hayo. Amru Mussa Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu amelaani mashambulizi hayo yaliyofanyika leo na kusema kuwa, kushambulia msafara wa misaada ya kibinaadamu ni jinai kubwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa nchini Uganda amesema kwamba, ameshangazwa na mashambulizi hayo na kuhukumu hatua hiyo ya kinyama.

0 comments:

Post a Comment