Wakfu wa kimataifa wa waandishi wa habari wa wanawake imempa tuzo ya ujasiri ya uandishi wa habari kwa uchunguzi wake.
"Sikutarajia lakini si kwamba nina furaha" Bi Ntetema ameiambia BBC, akisema kwamba mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne aliuliwa hivi karibuni.
Takriban maalbino 53 wameuawa Tanzania katika miaka ya hivi karibuni, pamoja na wengine wengi katika nchi jirani ya Burundi.
Bi Ntetema amelazimika kukimbia nchini mwake mara mbili kutokana na ripoti hizo.
Amesema, "Siwezi kuwa na furaha wakati kumetokea mashambulio saba tangu tarehe 8 Februari baada ya kuwepo na utulivu tangu Oktoba mwaka jana."
Amesema pia kwamba maalbino ndio mashujaa halisi, hasa wale waliokatwa viungo vyao au wanawake waliokimbiwa na waume zao kutokana na kuzaa maalbino.
Bi Ntetema, mwenye umri wa miaka 51, ambaye kwa sasa anafanya kazi kwenye shirika la kutetea haki za binadamu, Under The Same Sun amesema, "Hao ndio mashujaa wa kweli."
Takriban maalbino 17,000 wanaishi kwa hofu nchini Tanzania, hasa vijijini kaskazini magharibi mwa nchi hiyo penye kufanyika mauaji mengi ya albino.
0 comments:
Post a Comment