za vyombo vya habari kama ifuatavyo:
(a)Kwamba nia ya Mheshimiwa Rais Kikwete kwenye hotuba yake ilikuwa kupongeza
jitihada za Klabu ya Azam na Kampuni mama ya klabu hiyo Bakhressa Group kwa kuchukua
njia sahihi na za kisayansi kuendeleza mchezo wa soka nchini.
(b) Kwamba haikuwa nia ya Mheshimiwa Rais kuzikemea ama kuzisema taasisi nyingine za
soka katika Tanzania ambazo nazo kwa namna yake zinachangia maendeleo ya soka katika
nchi yetu.
(c) Kwamba, Mheshimiwa Kikwete, kama mpenzi wa soka na michezo maisha yake
yote anatambua na kuheshimu mchango wa Klabu za Soka za Simba na Yanga na
changamoto ambazo zinazikabili klabu hizo katika kuinua kiwango cha michezo nchini.
Hivyo, ni jambo lisilowezekana kuwa yeye anaweza kuzikejeli kwa namna yoyote hizo klabu
hizo kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimejaribu kuelezea tokea alipozindua
Azam Complex.
Hakuna shaka kuwa Rais Kikwete anajua fika na anaamini kuwa waandishi wa michezo
nchini wanafanya kazi kubwa na nzuri na wakati mwingine katika mazingira magumu ya
kuwahabarisha, kuwaelimisha na kuwaburudisha wananchi kuhusu michezo na maendeleo
yake nchini. Ushauri wake ni kwamba waendelee kufanya jitihada zaidi za kuongozwa na
misingi ya taaluma, weledi na ukweli zaidi katika kuifanya kazi yao.