Dar es Salaam, Februari 16 2016 -
Watumiaji wa simu za mkononi wameonywa dhidi ya matumizi ya simu bandia
na zisisokidhi viwango vya ubora ambazo tayari zimetangwa kupigwa
marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia mwezi Juni
mwaka huu.
Kutokana
na sababu hiyo, Tigo, ambayo ni kampuni ya kidijitali, imeanza
kuendesha kampeni ya kuhamasisisha wateja wake na umma kwa jumla kupitia
vyombo vya Habari inayolenga kuwaepusha na athari za matumizi ya simu
bandia.
``Kwa
mujibu wa maelekezo ya TCRA matumizi ya simu za mkononi ambazo namba
zake za utambulisho wa kimataifa (IMEI) ni bandia yatapigwa marufuku
kutumika kwa mitandao yote ya simu nchini Tanzania kuanzia Juni 16 mwaka
huu. Ili kujiepusha na usumbufu wowote utakaotokana na hatua hii
tunawashauri wateja wetu kujipatia simu halisi na bora kutoka maduka ya
Tigo yaliyo karibu nao,`` alisema Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya
Mawasiliano wa Tigo, David Zakaria.
Ripoti ya utafiti ulichapishwa katika tovuti ya GSMA ("http://www.gsma.com" www.gsma.com )
inasema kwamba tofauti na ilivyo kwa simu halali ambazo hupitia mamia
ya hatua mbalimbali za kuhakiki ubora wake kabla ya kupelekwa sokoni,
simu bandia hazifanyiwi majarbio ya ubora na kuna taarifa za kitafiti
zinazoonyesha kuwa baadhi ya simu bandia zina kiwango kikubwa cha madini
ya risasi na vitu vingine ambavyo ni hatari kwa mazingira na afya ya
binadamu.
Ripoti
hiyo inaendelea kusema kuwa simu feki zinatengenezwa na malighafi
dhaifu zisizokidhi viwango na zimeshaonesha kuwa kiwango cha hatari cha
vyuma na kemikali kama risasi hadi kufikia kiwango cha mara 40 zaidi
kuliko kiwango kilichoidhinishwa na sekta ya mawasiliano duniani kwa
mujibu wa na Jukwaa la Watengenezaji wa Simu za Mkononi (MMF).
Akizungumza
kuhusu hatua ya Tigo kutoa tahadhari kwa wateja wake Zakaria alisema,
``Wanunuzi wanatakiwa kuwa waangalifu wakati wanaponunua simu mpya au
vifaa vya mawasiliano madukani au katika intaneti kwa sababu bidhaa
nyingi feki zinatengenezwa kwa kuigaa muundo na nembo za kibiashara za
bidhaa halisi kwa makusudi ili kuwalaghai wateja.
``Ili
kuweza kuelewa iwapo simu yako ni feki au ni halisi unatakiwa kupiga
namba namba *#06# ambapo atapokea namba ya IMEI ya simu hiyo na kisha
kutima kwa njia ya jumbe mfupi kwenda namba 15090 ambapo utapata jibu
iwapo simu hiyo ya mkononi ni halisi au ni bandia,” alisema Zacharia.
0 comments:
Post a Comment