Mkurugenzi
wa Mipango wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo na timu
yake wamepata kutembelea Taasisi ya Serikali ya Miradi na Manedeleo ya
Miundombinu UTT-PID, Jijini Dar es Salaam mapema jana na kufanya
mazungumzo na uomgozi huo wa taasisi hiyo.
Afisa
Mtenaji Mkuu wa Taasisi ya Serikali ya Miradi na Manedeleo ya
Miundombinu UTT-PID, Dkt. Gration Kamugisha (kulia), akimkaribisha
Mkurugenzi wa Mipango, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Richard
Mkumbo, wakati mkurugenzi huyo na tmu yake walipotembelea taasisi hiyo
jijini Dar es Salaam jana, kwa lengo la kujua maendeleo ya taasisi na
changamoto wanazokabiliana nazo ili kutafuta ufumbuzi wa kuzishughulikia
changamoto hizo.
Mkurugenzi wa Mipango, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Richard Mkumbo, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Serikali ya Miradi na Manedeleo ya
Miundombinu UTT-PID, Dkt. Gration Kamugisha(aliyesimama kushoto),
akielezea mafanikio ya taasisi hiyo na changamoto inayokabiliana nazo
wakati timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ilipotembelea
taasisi hiyo.
0 comments:
Post a Comment