Mkurugenzi
wa Masoko, Utafitti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully
Mwambapa akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe
za miaka 20 ya benki ya utendaji wa benki hiyo uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa
uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20 ya benki hiyo
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa beki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa beki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Dk. Charles Kimei (kushoto).
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakishuhudia uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 ya benki ya CRDB katika hoteli ya Ramada leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charls Kimei (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja,
Saugata Bandyopadhyay (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Esther
Kitoka.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya Pamoja.
Wakurugenzi wakiwa wamepozi kwa picha.
Wakurugenzi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mameneja wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Akizungumza
na baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa benki hiyo wakati wa uzinduzi
wa kampeni ya miaka 20 ya utendaji wa benki hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa
CRDB Charles Kimei alisema wamefanikiwa kuifanya taasisi hiyo kuwa
kinara wa kutoa huduma bora.
Alisema
amana za wateja wa benki hiyo zimeongezeka zaidi ya mara 100 kutoka sh.
bilioni 40 walizoanza nazo mwaka 1996 hadi sh. trilioni 4.2 iliyokuwepo
Desemba 31 mwaka jana.“Safari ya miaka 20 ilikuwa na misukosuko ikiwemo
kupata hasara y ash. bilioni 1.8 mwaka 1997 lakini tunajivunia kusema
tumepita salama na sasa tumekuwa taasisi bora ya fedha hapa Tanzania.
“Idadi
ya bidhaa zetu, wateja na hata thamani ya benki pia imeongezeka… tunao
waajiriwa 2,682 wenye nidhamu,” alisema Dk. Kimei huku akibainisha
kwamba katika kampeni hizo watawekeza zaidi kwenye elimu.Alisema
maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka 20 ya CRDB yatakayohitimishwa
Juni mwaka huu yamepewa kauli mbiu ya ‘Benki inayokua na kuboresha
maisha ya watu.
0 comments:
Post a Comment