Naibu
waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi
ameviagiza vyombo vya habari nchini kuwa na sera katika vyombo vyao
inayojumuisha uandishi wa habari chanya kwa watu wenye ulemavu.
Akitoa
agizo hilo mbele ya wamiliki wa vyombo vya habari jana Ofisini kwake
Jijini Dar es Salaam Waziri Possi amesema habari nyingi zinazohusu watu
wenye ulemavu ni za kuwanyanyapaa na kuonesha kuwa hawana uwezo wa
kufanya mambo chanya.
“Wekeni
kipengele katika sera zenu kitakachosaidia kuwaelimisha watu kuwa watu
wenye ulemavu ni sehemu ya jumuiya katika maisha ya kila siku ya
wanadamu,” amesema.
Kwa
mujibu wa Waziri Possi, vyombo vya habari vikiwa na sera iliyowazi na
kuitekeleza, watu watabadilika na kupata taarifa nzuri za watu wenye
ulemavu.
Dkt. Possi ameeleza kuwa taarifa za watu wenye ulemavu hazitakiwi kuwa na lugha zenye chembechembe za kunyanyapaa.
Amesema kuwa kila kituo cha televisheni kinatakiwa kuwa na wataalamu wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama.
Naibu
waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi
akizungumza na Wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari jana ofisini
kwake Jijini Dare s salaam.
Amesema,
“Serikali kwa kutumia Sheria ya Watu wenye ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010
inaandaa tangazo kuvikumbusha vyombo vya habari kuwa kuwa na wataalam wa
kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama kwa watu wenye
ulemavu.
”Aidha
Naibu Waziri amewaagiza wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ajira kwa
watu wenye ulemavu kwani Sheria inaagiza lazima chombo chochote chenye
wafanyakazi zaidi ya 20, angalau mfanyakazi mmoja awe mtu mwenye
ulemavu.Kwa upande wao wamiliki wameiomba serikali kutotoza kodi tangazo lolote linalohusu habari chanya za watu wenye ulemavu.
Hata
hivyo wamiliki hao wamemweleza Naibu Waziri kuwa ubadilishaji wa Sera
pamoja na kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa
watu wenye ulemavu ni jambo zuri, lakini wanahitaji kupewa muda wa
maandalizi.
CHANZO: MAJID MJENGWA
0 comments:
Post a Comment