SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 31, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA MAPAMBANO YA NGUMI YALIYOCHEZWA IDDI PILI MANZESE

Bondia Sadick Nuru (kushoto) akioneshana umwamba na Baraka Mchonge wakati wa pambano lao lililofanyika Siku ya Iddi Pili kwenye Ukumbi wa Manyara Park Manzese jijini Dar es Salaam.Katika pambano hilo Sadick, alishinda kwa pointi.
Bondia Steven Kobelo (kushoto) akipambana na Karim Ramadhani. Katika pambano hilo hakupatikana mbabe. 

Mabondia Joseph Gili(kushoto)akioneshana umwamba wa na Ibrahimu Tamba Katika pambano hilo Tamba alishinda kwa K/O raundi ya nne. 
Bondia Julius Kisalawe (kushoto) na Ramadhani Kumbele wakichapana wakati wa pambano lao la kuwania ubingwa wa 
 TPBC uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam Kumbele alishinda kwa point na kufanikiwa kuchukua ubingwa huo. Picha na Super D
Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kulia akimvisha mkanda wa ubingwa bondia Ramadhani Kumbele baada ya kumdunda Julius Kisalawe kwa point kushoto ni Mwamuzi Ally Bakari.

0 comments:

Post a Comment