Mmoja
wa wafanyakazi wa TMT, Happy (mwenye fulana iliyoandikwa crew) akitoa
maelekezo kwa vijana ambao wamejitokeza kwa mara ya kwanza katika usaili
wa Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika katika
Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaama ambalo lilisimama
kutokana na mmoja wa Majaji wetu, Bi Yvonne Cherry kufiwa na Mzazi
Mwenzake ambae pia alikua ni Muongozaji na Mtayarishaji mahiri wa filamu
na vipindi vya runinga Marehemu George Tyson ambae amezikwa hapo jana
kijijini Kwao huko Kenya.
Baadhi
ya washiriki waliojitokeza katika Shindano la Tanzania Movie Talents
wakiwa kwenye mstari kwaajili ya kupewa namba ya ushiriki.
Baadhi ya washiriki wa TMT wakipewa namba ya ushiriki na maelekezo.
Baadhi ya washiriki wakisubiria Kuingia ndani Kwa majaji kwaajili ya kuanza kuonyesha Uwezo wao wa kuigiza.
Washiriki wakisubiri zamu zao kwaajili ya kuonyesha uwezo wao wa kuigiza.
Hatimaye
shindano la Tanzania Movie Talents limeendelea tena leo mara baada ya
kumalizika kwa Msiba wa aliyekuwa Mzazi Mwenza wa jaji Yvonne Cherry au
Monalisa, Marehemu George Tyson. Marehemu George Tyson ambaye
alikuwa ni mmoja wa Waongozaji filamu mahiri hapa nchini
Tanzania,alifariki kwa ajali ya gari wakati akitokea mkoani Dodoma
kikazi akirejea jijini Dar.
Ikumbukwe
kuwa Shindano hili lilianza kufanyika Siku ya Ijumaa tarehe 30 Mei 2014
katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam. Mara
baada ya kumaliza kwa Shindano hilo kwa siku hiyo ya Ijumaa ndipo
tulipopata Taarifa za Msiba wa Marehemu George Tyson na ndipo tulipoamua
Kusitisha Shindano hilo hadi pale msiba utakapomalizika kwa maana
Ulikua ni Msiba mkubwa sana katika Tasnia ya Filamu nchini lakini
vilevile Msiba huo ulitugusa moja kwa moja kutokana na Marehemu George
Tyson alikuwa mzazi Mwenza wa Mmoja wa Majaji wetu ambae ni Vyonne
Cherry au Monalisa.
Kutokana
na Msiba huo Timu ya TMT ilibidi kusitisha na kuungana na Jaji wetu
Monalisa katika kipindi hiki kigumu cha Msiba wa kuondokewa na mzazi
mwenzake hadi pale walipomaliza kuzika Hapo jana.
Shindano
hili litaendelea kwa Siku tatu zilizobaki kwaajili ya Kupata washindi
watano watakaoiwakilisha kanda ya Pwani ambapo kila Mmoja ataondoka na
kitita cha Shilingi laki tano kila Mmoja na baadae kuungana na washindi
wengine kutoka kanda 5 katika safari ya kuwania zawadi kubwa kabisa ya
Milioni 50 za Kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni
mwa Mwezi wa nane na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.
NA LUKAZA BLOG.