SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, May 25, 2014

MARAIS WAONDOKA BAADA YA KUSHUHUDIA KUAPA KWA RAIS ZUMA LEO

  Ndege za kijeshi zikiunda umbo la "20" kuashiria miaka ishirini ya uhuru kamili wa Afrika Kusini  katika sherehe za kuapa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini, leo Mei 24, 2014.
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiondoka Union Buildings baada ya kushuhudia Rais Jacob Zuma akiapa kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini, leo Mei 24, 2014.
 Rais Jacob Zuma akila kiapo katika Nelson Mandela Amphitheate katika jengo la Union Buildings mjini pretoria wakati wa sherehe za kuapishwa kwake leo mei 24,2014
Marais na viongozi toka nchi mbalimbali wakiondoka Union Buildings baada ya kushuhudia Rais Jacob Zuma akiapa kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini, leo Mei 24, 2014. PICHA NA IKULU