Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga
( wa pili kulia) akiwasili katika viwanja vya Oyster Bay kushiriki
semina ya mafunzo ya usalama na afya mahala pa kazi na usalama
barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa wanafunzi wa shule za
msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa
Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Karen Lwakatare.
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga
akizungumza wakati wa semina ya usalama na afya mahala pa kazi na
usalama barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa wanafunzi wa
shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni iliyofanyika mwishoni mwa
wiki katika viwanja vya Oyster Bay jijini Dar es salaam. Kushoto ni
Meneja wa OSHA kanda ya Pwani Jerome Materu na Mkuu wa Idara ya Usalama,
Afya na Mazingira wa Vodacom Karen Lwakatare.
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga
akizungumza wakati wa semina ya mafunzo ya usalama mahala pa kazi na
usalama barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa wanafunzi wa
shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni. Kulia ni Mkuu wa Idara
ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Karen Lwakatare.
Meneja
wa Mamlaka ya Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) kanda ya Pwani
Jerome Materu akizungumza wakati wa semina ya mafunzo ya usalama mahala
pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa
wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni. Kushoto ni
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu kamishna wa Polisi Mohamed
Mpinga na Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Karen
Lwakatare(kushoto).
Mfanyakazi
wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Ammy Mlay akipima uelewa wanafunzi
kuhusu amsula ya uslama na afya mahala pa kazi wakati wa semina ya
mafunzo ya usalama mahala pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na
kampuni ya Vodacom kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani
na Mbuyuni mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Oyster Bay jijini Dra
es salaam. Semina hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usalama na
afya mahala pa kazi duniani.
Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania Happy Paul (kushoto) na Ammy Mlay wakiwaonesha
wanafunzi (hawapo pichani)kanuni ya lazima namba nne na sita ya usalama
kazini kwa wafanyakazi wa Vodacom ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha
wafanyakazi wakati wote wanakuwa salama na wenye afya wanapotimiza
majumu yao.Vodacom kwa ksuhirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni
mwishoni mwa wiki waliendesha semina ya masuala ya afya na usalama
kazini kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Mbuyuni na Msasani.
Meneja
wa Masuala ya Sheria Upendo Haji akimuonesha mmoja wa wanafunzi
aliyehudhuria mafunzo ya usalama na afya kazini iliyoandaliwa na Vodacom
Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Mbuyuni
na Msasani jijini Dar es salaam kaununi ya lazima nambari sita ya
usalama inayotumiwa an Vodacom kuhamasisha usalma wka wafanyakazi wake
wawapo kazini. Vodacom kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa
Kinondoni mwishoni mwa wiki waliendesha semina ya masuala ya afya na
usalama kazini kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Mbuyuni na
Msasani.
Mwanafunzi
wa shule ya msingi Msasani ya jijini Dar es salaam akizima mota kutumia
kifaa wakati wa semina ya uslama na afya kazini iliyoandaliwa na
Vodacom Tanzania kw akushirikiana na jeshi la polisi. Wanaomsimamia
mwanafuzni huyo ni Karen Lwakatare (kushoto) na ofisa kutoka kampuni ya
ulinzi ya Security Group.
Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Kanda ya mkoa wa Kinondoni wamewapatia mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa wanafunzi wa shule za msingi Msasani, Mbuyuni na Oysterbay zote za wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kwa upande wa Vodacom wao wametoa mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa wanafunzi hao wakiamini kuwa wao ndio wafanyakazi wa baadae ambao ndio tegemeo la kukua kwa uchumi wetu.
Akizungumzia juu ya mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama,Karen Lwakatare amebainisha kuwa wao watatoa elimu na mafunzo juu ya usalama mahala pa kazi lengo ikiwa ni kufafanua umuhimu wake.
“Mafunzo haya yanalenga kwanza kabisa kuwafafanulia nini maana ya usalama mahala pa kazi, wakishaelewa hivyo basi zoezi la kutoa elimu kwetu litakuwa ni kazi rahisi. Wanafunzi wanauelewa mkubwa na ni rahisi kushika mambo, mbali na hapo wanaishi katika mazingira ambayo ni lazima wafahamu vitu hivi.” Alisema Lwakatare na kuongezea kuwa, “Kwa mfano wanafunzi ambao tunawapa mafunzo hapa shule zao zipo katikati ya jiji na kuzungukwa na barabara kuu hivyo basi lazima wapewe mafunzo haya.” Lwakatare aliendelea kwa kusema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa wanafunzi wa darasa la tatu, nne na tano kutoka kila shule ambazo zimetajwa hapo awali. Wanafunzi hawa wataelezwa ni kwa nini kuna umuhimu wakuzingatia mafunzo hayo kwani hata wao miaka ya baadae watakuja kuwa wafanyakazi na lazima watakuja kukumbana nazo.
“Tunategemea wanafunzi hawa siku za baadae wamalize masomo yao waje kuwa wafanyakazi na wengine wanaweza kubahatika na kuajiriwa na Vodacom. Mafunzo haya ya mara kwa mara yana faida kubwa na pia nina amini wao ndio watakuwa mabalozi kwa wanafunzi wenzao, marafiki, wazazi na hata ndugu na jamaa huko waendapo.” Alimalizia Lwakatare Kwa upande wa jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni wao watatoa mafunzo kwa wanafunzi hao juu ya kutumia vifaa mbali mbali vya kiusalama na usalama barabarani ili kuwapa uelewa zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kinondoni, Kamanda Mohammed Mpinga amesema kuwa wanafunzi hawa wengi wao wanatumia barabara wakati wa kuja shuleni na kurudi nyumbani.
“Tumeona kuna umuhimu kwa wanafunzi hawa kujua alama mbali mbali za barabarani pamoja na matumizi yake mbali na kuishia kuziona tu kwa macho. Kama suala la usalama barabarani lazima lipewe kipaumbele kwani kama tujuavyo jiji la Dar es Salaam lina changamoto nyingi ukizingatia magari sasa yamekuwa mengi kitu ambacho kunakuwa na mikanganyiko mingi.” Alimalizia Kamanda Mpinga.