SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 8, 2014

"NILISHAWAHI KUWA NA MIL 600, SASA HIVI SINA HATA SENTI TANO" -MR NICE

Hivi karibuni baada ya kuchezea kichapo kisa kikidaiwa kuwa mke wa mtu nahapo alipigwa chupa ya bia iliyomchana chana uso mzima na kumuacha na kilema cha makovu.



Hapa Mr Nice Shavu dodo msafara wake ulikuwa zaidi ya gari nane hadi kumi huku zikiwa zimejaa wapambe na wachumba wa ukweli.




Mmoja wa wacheza shoo wa Mr Nice aliyekuwa kivutia kwa mashabiki alifahamika kwa jina la Wabogojo
 
 
Hapa ndiyo kwanza anaanza kuimba muziki kitambi hicho
 
 
Msimu wa Majanga huku tayari akiwa amefirisika kabisa

 
Hapa Mr Nice kipindi akiwa safi pesa karatasi watoto wazuri full kumshobokea kama ilivyo kwa Diamond kwa sasa.
 

Mawazo juu ya mawazo, washikaji wote aliokuwa anakula nao bata wamekula kona yani shida tupu.
 
 
Hapa Mr Nice akiwa hoi chini baada ya kupigwa ngumi zaidi ya 20 za chembe na Dudu Baya kwenye ukumbi wa Diamond miaka kadhaa iliyopita




Hapa Dudu Baya akipambana na Mabaunsa kwa kumzuia asiendelee kumsurubu Mr Nice siku alipompa kipigo cha mbwa mwizi. Kulia mwenye shati jeupe ni Mkurugenzi wa Clouds Media Lugemalila Mutahaba

Katika hali isiiyokuwa ya kawaida mwanamuziki Lucas Mkenda maarufu kwa jina la Mr Nice ameibuka na kueleza sababu zilizomfanya kufirisika licha ya kuwahi kumiliki zaidi ya bilioni moja na nusu kwenye akaunti zake tofauti.
 mwanamuziki huyo ambae kwa sasa yupo nchini kwa muda mfupi kabla ya kurudi tena nchini Kenya alikohamishia makazi na kufanyia shughuri zake za kimuziki huko.

Akizungumza na mwandishi wetu kwenye ukumbi wa mpya wa burudani wa Full Stop uliopo Mwanamboka Kwa Manyanya Kinondoni Jijini Dar ambapo alisema kuwa dunia imemfanyia kitu kibaya na hafahamu nini kimetoka katika maisha yake.

Mr Nice alisema kuwa anashindwa kuelewa kwa nini maisha yamempiga kiasi hicho kwani pesa yote aliyokuwa anaipata alikuwa anaipata kwa jasho lake" Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu kwani sikuwahi kumdhurumu mtu wala kuiba cha mtu pesa yote nilikuwa naipata kwa hali naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu" Alisema mwanamuziki huyo

Aidha mwanamuziki huyo anasema" Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini pesa hizo zilitokana kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, Afrika Kusini na kwingineko na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana" Alisema
Hata hivyo Mr Nice nasema kuwa hizo ni nchi za mbali lakini bado shoo za alizokuwa anazifanya nchi za Kongo, Zambia, Uganda, Rwanda, Kenya na moja ya shoo ambayo akiikumbuka huwa inamtoa machozi ni ile ya nchini Rwanda ambayo siku anashuka Airport alikuta kitu cha kushangaza sana.

Anasema alikuta umati mkubwa wa watu ukimsubiri pamoja na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo pamoja maofisa wa ngazi za juu wa Polisi na Jeshi huku kukiwa na Red Capet kisha akapigiwa saluti huku akisindikizwa na mizinga ishirini na moja.Hata hivyo mwanamuziki huyo anasema alifikia uamuzi wa kujiita the milonea Mr Nice baada ya kuingia mkataba na kampuni ya TBL kupitia bia yake ya Safari alifanya shoo mikoa yote ishirini n tano kwa pesa ndefu na kufanya kuwa mwanamuziki mwenye pesa nyingi Afrika Masharki kuliko mwanamuziki yeyote.

Mambo mengine ya kushangaza aliyokuwa nayo mwanamuziki huyo kipindi akiwa na pesa ni juu ya msafara wake uliokuwa umejaa wapambe wengi na kulazimika kutumia magari zaid ya nane kwenye mizunguko yake huku yakiwa hayazimwi Ac masaa ishirini na nne hata kama hayana watu ndani.
Aidha Mr Nice alimaliza kusema kuwa anawashauri wanamuziki wa sasa kujifunza kwa waliopita ili nao yasijekuwakuta kama yaliyowakuta wao
Chanzo: Sophie Mbeyu Blog