SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 30, 2014

PSPF washiriki katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya duniani kwa wafanyakazi viwanja vya Mnazi Mmoja Dar

IMG_4021 - Copy
Ofisa muendeshaji wa Mfuko wa Pesheni wa Mashirika ya Umma (PSPF),  Bw. Hadji Jamadary (kushoto) akimwelekeza kujaza fomu Shabani Maganga wakati wa maaadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.
pspf 1 - Copy
Ofisa muendeshaji wa PSPF, Hadji Jamadary (kushoto) akiwapatia maelezo ya jinsi ya kujiunga na PSPF wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.
pspf3 - Copy
Afisa Muendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF) Bw.  Lule Kasembwe (kushoto) akitoa maelekezo kwa wazee waliotembelea banda lao kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

HALMASHAURI NA WADAU WA JIJI LA MWANZA WAANZA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ZITAKAZOFANYIKA JUNI 16.

 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi inayoundwa na wadau wa watoto jijini Mwanza Bw. Godfrey Salumu akifafanua utaratibu mzima wa utendaji kazi wa kamati ndogo ndogo zilizoundwa kwa wajumbe (hawapo pichani) ili kuweza kufanikisha maadhimisho hayo.

SAFISHA JIJI YAENDELEA LEO KARIAKOO JIJINI DAR

 Tingatinga la Manispaa ya Ilala likibomoa vibanda vilivyojengwa maeneo yasiyoruhusiwa Kariakoo katika operesheni safisha jiji iliyofanyika Dar es Salaam, mitaa ya Aggrey na Livingstone.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Richard Sezibera akimkaribisha Rais  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo unaofanyika leo.
 Rais  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha(AICC) kwenye mkutano wa 12 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini Arusha.Rais Kenyatta ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya wnanachama watano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijadiliana jambo kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa  wakuu wa nchi za  Jumuiya ya Afrika Masharariki uliofanyika mjini Arusha leo. Picha na Freddy Maro.

DKT SHEIN IKULU AZUNGUMZA NA UONGOZI OFISI YA MAKAMU WA KWANZA NA WA PILI WA RAIS

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja jana asubuhi.
Baadhi ya maafisa wa idara mbali mbali za Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wakiwa katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja jana asubuhi,mwenyekiti wake akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Picha na Ramadhan Othman, IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja jana jioni.

Polisi Mkoani Manyara yakamata misokoto 6,000 ya bangi

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, (SACP) Deusdedit Nsimeki, (kulia) akiwa na polisi wengine wa mjini Babati, wakati akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya misokoto 6,000 ya Bangi waliyoikamata kwenye mabasi mawili hivi karibuni ambayo ilikuwa imewekwa kwenye mikate iliyokuwa imesafirishwa na watu wawili,ambao wamewekwa ndani.

Airtel yatoa msaada wa vifaa vya ofisi kwa shule ya Msingi Chau Chalinze

Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani William Mrocky akikabithi kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau Bwana Elvin Msangi msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu wa shule ya msingi ya chau iliyoko Chalinze Mkoani Pwani.

Rais Dkt Kikwete Akutana na Ujumbe wa Rais wa Burundi, na Viongozi wa Baraza la Uunguzi na Ukunga Mkoba Private Equity Fund.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Sheikh Mohamed Rukara, Mjumbe maalum wa Rais wa Burundi Mhe Pierre Nkurunzinza, alipofika na ujumbe wake kuwasilisha ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam 

Warioba awataja wasaliti wa Nyerere

Na Kelvin Matandiko, Mwananchi
Dar es Salaam. 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wanasiasa wanaomtuhumu kwa kumsaliti Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhusu Muungano, ndiyo wasaliti kwa kuwa waliingiza kwenye Katiba, mambo yanayokinzana na makubaliano ya Muungano huo.

NAFASI MPYA ZA KAZI ACTIONAID TANZANIA MWISHO TAREHE 11/5/2014

Administration and Logistics Coordinator
ActionAid is an international anti-poverty agency working in over 40 countries, taking sides with poor people to end poverty and injustice together.
ActionAid started its operation in Tanzania in 1998. ActionAid Tanzania (AATZ) envisions seeing Tanzania without poverty and injustice in which every person enjoys his/her right to a life of dignity. Currently, AATZ is looking for a qualified, experienced and self-motivated person from its internal staff to fill in the following post:

KIPANYA LEO

BASI LAUA WATU 18 WAKIMSITIRI MAREHEMU

Sumry4_ee1c9.jpg
WATU 18 wamekufa papo hapo wakiwemo askari Polisi wanne katika ajali ya barabarani, wakati basi linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipopamia watu hao wakati wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika.

KUTOKA MAGAZETINI JUMATANO YA LEO

0001_47734.jpg

RONALDO AVUNJA REKODI YA MESSI

Christiano Ronaldo 
Nyota wa Real Madrid ya Uhispania Christiano Ronaldo amevunja rekodi ya Lionel Messi ya ufungaji mabao mengi zaidi katika ligi ya mabingwa barani Uropa alipoifungia timu yake mabao mawili na kuisaidia kuichapa Bayern Munich mabao 4-0 katika nusu fainali jana usiku
Mreno huyo mwenye umri wa miaka , 29,alifunga bao lake la 15 na 16 msimu huu katika uwanja wa Allianz Arena.
Kufuatia ushindi huo Real Madrid ilifuzu kwa fainali ya mchuano huo kwa jumla ya mabao 5-0.
Ronaldo sasa amefunga mabao 16 katika mechi kumi za ligi hiyo ya mabingwa Barani Ulaya mbili zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona .
Rekodi hiyo ya mabao 14 ilikuwa ikishikiliwa kwa pamoja kati ya Messi (2011-12, Barcelona), Ruud van Nistelrooy (2002-03, Manchester United) na Jose Altafini (1962-63, AC Milan).
Kwa jumla Ronaldo amefunga mabao 67 katika ligi hiyo ya mabingwa barani ulaya sawa na Messi na ni mabao manne tu nyuma ya rekodi ya idadio kubwa zaidi ya mabao yaliyofungwa na mchezaji wa zamani wa Real na Schalke Raul.
CHANZO BBC,

Wafanyakazi New Habari (2006) wapinga ubaguzi

Wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari (2006), jana walijumuika na baadhi ya mastaa duniani kula ndizi kama ishara ya kupinga vitendo vya kibaguzi kama alivyofanyiwa mchezaji Daniel Alves wa Barcelona
NA MBEYA YETU

Wanamichezo 45 waagwa rasmi kwa ajili ya kwenda nje kufanya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akizungumza na wanamichezo wanaoenda kuweka kambi katika nchi za New Zealand, Ethiopia, China na Uturuki ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola mapema mwezi julai. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leornard Thadeo.

Tuesday, April 29, 2014

NAFASI MPYA ZA KAZI SUA MWISHO TAREHE 12/5/2014


Assistant Lecturer (Department Of Wildlife Management )
Company:Sokoine University of Agriculture (SUA)
Location:Morogoro
POSITION DESCRIPTION:
The Management of Sokoine University of Agriculture (SUA) invites qualified Tanzanians to apply for positions of Tutorial Assistants (TA's) «35 yrs of age) and Assistant Lecturers «45 years). Applicants are advised to note that the minimum GPA of 3.8 or an average of B for unclassified degrees such as that of Veterinary and Medical graduates at undergraduate level applies for TA's and 3.5 at BSc/BA level or equivalent (i.e. an average of B for Veterinary and Medical graduates) and a good Masters degree is applicable for those with postgraduate qualifications. Only registered Veterinarians will be considered for interviews.

LIGI KUU UINGEREZA, ARSENAL YAIGARAGAZA NEWCASTLE KWA MABAO 3-0

 Timu ya soka ya Arsenal ikicheza nyumbani katika uwanja wake wa Emirates usiku wa kuamkia leo, wameendelea kupigania nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao, hii ni baada ya kuifunga bila huruma Newcastle mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu Uingereza.

Sikiliza na Pakua Wimbo Maalumu wa Miaka 50 ya Muungano wa Hellow Hellow Tanzaniaaa


Tanzania @ 50 Wimbo Maalumu wa Muungano Utanzania Wetu ni Muungano Wetu, Tuulinde, Tuudumishe na Tuuimarishe 

Wimbo: TUULINDE
 Watunzi: LAMECK DITTO, AMINI MWINYIMKUU
 Watayarishaji: EMA THE BOY, TUDDY THOMAS
 Studio: SURROUND SOUND

 Wasifu wa Wimbo: Wimbo huu maalumu wa Muungano umeimbwa na wasanii 50, kutoka katika mahadhi tofauti tofauti ya muziki kama Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop na muziki wa injili. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, wasanii 50 tofauti kuimba wimbo kwa pamoja, na kwa ushirikiano mkubwa, wasanii hawa wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu.

 Baadhi ya Wasanii waliohusika Amini Kadjanito Mwasiti Linah Christina Shusho Khadija Kopa Frola Mbasha Ommy Dimpoz Diamond Josse Mara Kalala Jr Ali Kiba Peter Msechu Mrisho Mpoto Abdul Kiba Mzee Yusuph Angel Mwana Fa Nikki Wa pili G Nako God Zilla Madee Asley Shaa Mandojo Domokaya Shilole

Waraka Wa Uraia Pacha Kutoka California, Marekani

Nyama Choma Live in Washington DC.

Nyama inaendelea Kuchomwa na Sausage.

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA WIKI YA CHANJO DUNIANI MKOANI KILIMANJARO

Mke wa rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.

Breaking News: Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi Askari 6 wa kikosi cha Usalama barabarani


Kamanda wa Polisi  Mkoani Mbeya  Ahmed Msangi

========
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi Askari 6 wa kikosi cha Usalama barabarani  Wilaya za Rungwe na Mbeya kwa tuhuma za kuomba,kushawishi na kupokea rushwa.

Kamanda wa Polisi  Mkoani Mbeya  Ahmed Msangi amewatataja Askari hao kuwa ni pamoja na waliokuwa wakifanya kazi wilaya ya Mbeya barabara ya Mbeya/Tunduma eneo la Songwe ni Copro Jonson,PC Rymond na PC Simon.

Msangi amewataja wengine kuwa ni pamoja Sajini Hezron,PC Shaban na PC Kajolo ambao walikuwa wanafanya kazi barabara ya Mbeya/Rungwe wilaya ya Rungwe.

Askari hao walikuwa wanakabiliwa na makosa hayo na walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi na Hukumu kutolewa Aprili 24 mwaka huu na kupewa adhabu ya kufukuzwa kazi.

Aidha Kamanda Msangi amesema Jeshi lake halitasita kuwafukuza kazi Askari watakaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi na Askari yeyote atakayekwenda kinyume atakumbwa na adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani.

Askari wengine waliofukuzwa kazi hivi karibuni ni pamoja na PC James Kagomba ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha,WP Prisca Kilwai anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mtoto.

Wengine wliohukumiwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ni DC Marcelino Venance mwenye namba 8084,PC Juma Idd mwenye namba 3117 na Askari wa Mgambo MG Jackson Mwakalobo ambao walidaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi Dentho Kajigili aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Ivumwe ya Jijini Mbeya. 

Na Mbeya yetu

KUTOKA MAGAZETINI JUMANNE YA LEO

001_90921.jpg

Monday, April 28, 2014

Kipanya LEO

Wanafunzi wapatiwa mafunzo ya usalama na Afya mahala pa kazi na barabarani

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga ( wa pili kulia) akiwasili katika viwanja vya Oyster Bay kushiriki semina ya mafunzo ya usalama na afya mahala pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Karen Lwakatare.

“TUNALAANI UKATILI MAOVU WANAYOFANYIWA WAANDISHI WA HABARI.” - TIBANYENDERA (MISA-TAN)

DSC_0085
Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera (wa pili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusiana maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yatakayofanyika wiki hii duniani kote. Kushoto ni Meneja wa Maadili na Usuluhishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Allan Lawa, Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama (wa pili kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanja (kulia).(Picha na Zainul Mzige).

CLINIKI YA ARS YA VIJANA 72 KUTOKA NCHI 12 ZA AFRIKA YAFUNGWA RASMI

 Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Levi Nyakundi akiongea na waandishi wa habari wakati wa kufunga kliniki ya kimataifa ya soka ya siku tano ya Airtel Rising Stars kwenye uwanja wa Azam Compex. Kliniki hiyo ilileta pamoja vijana zaidi ya 70 kutoka nchi 12 Barani Afrika.

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA ZILIVYOFANA WASHINGTON DC

Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Watanzania hapa Washington DC kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano.

SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR YAFANA MJINI ROMA

                               Keki yetu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAINGIA RASMI KIJIJI CHA MAISHA PLUS

Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus Jana usiku.

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI, KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo April 28-2014, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na Afya Duniani.

Sunday, April 27, 2014

UKAWA WAMJIBU KIKWETE

ukawa5 eeb08
Na Hudugu Ng'amilo
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) warudi bungeni akidai hawana sababu ya kwenda kushitaki kwa wananchi kwa sababu watawacheka na kuwasikitikia, umoja huo umemjibu wakisema wapo tayari kuchekwa.

KOCHA MHOLANZI AKABIDHIWA MIKOBA YA KUINOA TAIFA STARS

Mart Nooij-Kocha Mkuu Mpya Wa Timu Ya Taifa (Taifa Stars)

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi Mart Nooij kutoka Uholanzi kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars).

Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemtambulisha kocha huyo leo (Aprili 26 mwaka huu) kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akiwa amefuatana na Makamu wake Wallace Karia, amesema anafurahi kumtangaza Nooij na ana matarajio kuwa Tanzania itanufaika na uzoefu wake mkubwa wa ukocha, hasa katika bara la Afrika.

“Nawaahidi Watanzania kuwa sitomuingilia kocha katika kazi yake. Kama mimi sitomuingilia kocha, basi hakuna mtu yeyote atakayemuingilia. Tumemwajiri yeye kwa vile ni mtaalamu, hivyo hakuna sababu ya kumuingilia,” amesema Rais Malinzi.

Naye Nooij ambaye amepewa mkataba wa miaka miwili amesema yeye ni mtu wa maneno mafupi, hawezi kuahidi kitu lakini ana matarajio ya kuifanya Taifa Stars ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali.

Amesema kabla ya kukubalia kufundisha Taifa Stars alikuwa na klabu ya St. Georges ya Ethiopia, lakini vilevile amewahi kufundisha mpira wa miguu barani Afrika katika nchi za Burkina Faso, Mali na Msumbiji.

Wasifu wa Nooij umeambatanishwa hapo chini

MABADILIKO YA MIELEKEO YA BARABARA ZA SAMORA NA SOKOINE JIJINI DAR KUANZA KESHO, APRILI 28, 2014

 Viongozi wakijadiliana wakati wa zoezi la kuweka Alama muhimu za barabarani Katikati ya Jiji tayari kwa mabadikiko ya mielekeo ya barabara za Samora na Sokoine unaoanza Jumatatu 28/04/2014. 
 Vijana wakiweka kibao cha alama barabarani.
Jana Aprili 26, 2014 zoezi la kuweka Alama muhimu Katikati ya Jiji la Dar es Salaam limekamilika tayari kwa mabadikiko ya mielekeo ya barabara za Samora na Sokoine unaoanza Jumatatu 28/04/2014. Kwa daladala itakuwa kama ifuatavyo:

Habari na Picha na Deo Mutta, DART

1. Daladala Zote zinazotokea Barabara ya Ally Hassan Mwinyi zitaingia mjini kupitia Bibi Titi na kukata kushoto kuingia barabara ya Makataba na kuishia Posta Mpya na kutoka kwa kuzunguuka Mnara wa Askari na kushuka na Maktaba na Kupinda kulia kuingia Bibi Titi na baadaye All Hassan Mwinyi.

2. Daladala Zote zinazotokea Barabara ya Morogoro zitapinda kushoto kuingia Bibi Titi na Kupinda kulia kuingia Maktaba hadi Posta Mpya. Zitatoka kwa kuzunguuka Mnara wa Askari na kuingia Samora hadi Clock Tower na kuingia Uhuru na Kupinda kulia kuingia Bibi Titi na Kupinda kushoto kuingia Morogoro.

3. Daladala zinazotokea Barabara ya Uhuru zitakwenda moja kwa moja hadi Clock Tower na kuingia Barabara ya Railway na Kupinda kushoto kuingia Sokoine na kuishia Stesheni. Zitatoka kwa kupitia Samora kutokea station na kuingia Uhuru kupitia mnazi mmoja.

4. Daladala zinazotokea Barabara ya Nyerere zitapita bibi Titi na kukunja kulia kuingia Uhuru hadi Clock Tower na kuingia Railway na kukunja kushoto kuingia Sokoine na kuishia Stesheni. Zitatoka kupitia Samora hadi Clock Tower na kuingia Nkurumah na kuingia Nyerere eneo la Cocabs.

5. Daladala zinazotokea barabara ya Kilwa Zitapitia Sokoine na kuishia Stesheni na kutoka kupitia Railway na kuingia Sokoine kuelekea Water Front.

BALOZI IDDI AISHUKURU SERIKALI YA CHINA KUKUBARI KUJENGA UWANJA WA MAO TSE TUNG

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kupitia Balozi Wake Mdogo aliyepo Zanziobar Bw. Xie Yunliang kwa kukubali wazo la SMZ la kuiomba China  kusaidia ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung  Jina linalotokana na Muasisi wa Taifa hilo la China. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZAFANA UJERUMANI: PROFESA MUHONGO AWA MGENI RASMI

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto) akiingia katika ukumbi wa Deustche Bank uliopo Berlin, Ujerumani kabla ya kuzindua rasmi sherehe za jubilee ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kulia ni balozi wa Tanzania Ujerumani Mhe. Philip Marmo.

VIONGOZI TOKA NCHI MBALIMBALI WATAMBULISHWA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO























ALIYEKUWA RAIS WA KENYA MWAI KIBAKI

NA MICHUZI MATUKIO