Timu ya soka ya Arsenal ikicheza nyumbani katika uwanja wake wa Emirates usiku wa kuamkia leo, wameendelea kupigania nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao, hii ni baada ya kuifunga bila huruma Newcastle mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu Uingereza.
Arsenal ambao waliianza vyema ligi kuu hadi kutishia kuutwaa ubingwa msimu huu kabla ya kupotea njia, jana walijikuta wakiizamisha kabisa Newcastle kwa mabao yaliyowekwa kimiani na wachezaji Koscienly katika dakika ya 26, bao la pili likifungwa na Ozli dakika ya 42 kabla ya Giroud kufunga bao la tatu dakika ya 66 ya mchezo.
Kwa matokea hayo, Arsenal imeendelea kubaki nafasi ya nne ikiwa na pointi 73 hivyo kurejesha matumaini kwa mashabiki wake kuwa, walau itakata tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.