SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 29, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA WIKI YA CHANJO DUNIANI MKOANI KILIMANJARO

Mke wa rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.

Baadhi ya taasisi a NGO'S mbalimbali zilihudhuria uzinduzi huo.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi wakisikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa.
Makundi mbalimbali ya watu yalishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani iliyozinduliwa mjini Moshi.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi wakisikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani.
Mwakilishi  mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Rufaro Chatora akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi huo kutoka Asasi mbalimbali mkoani Kilimanjaro.
Mwakilishi wa UNICEF,Sudha Sharma akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Naibu waziri wa Afya,Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika katika sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo duniani uliofanyika katika viwanja vya mandela mjini Moshi.
Mkurugenzi
huduma za Afya toka wizara ya Afya,Dk Neema Rusibamayile akitoa neno la shukrani mara baada ya Mke wa rais,Mama Salma Kikwete kutoa hotuba yake.
Mke wa rais ,Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo duniani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa chanjo ya matone kwa mtoto Ahmad Saleh kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo duniani.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.