Wajumbe
wa Bunge la Katiba, wakimwondoa mwenzao baada ya kutokea vurugu bungeni
jana wakati Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba akijiandaa
kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba. Picha na Emmanuel Herman
Mwenyekiti
wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana alipata jaribio la kwanza
baada ya baadhi ya wajumbe kupinga kuruhusiwa kwa Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuwasilisha Rasimu ya Katiba
kwa madai ya ukiukwaji wa kanuni za Bunge.
Wajumbe
hao chini ya Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa), walitangaza mapema
jana kwamba wangepinga ratiba nzima kuendelea hadi madai yao ya kumtaka
Rais Jakaya Kikwete afungue Bunge kwanza kabla ya rasimu kuwasilishwa
yasikilizwe.
Madai ya Ukawa
Viongozi
wa Ukawa waliitisha mkutano wa wanahabari na kutangaza kususia kuendelea
na ratiba wakipinga uvunjwaji wa kanuni unaodaiwa kufanywa na Sitta.
Katika
uamuzi huo uliofikiwa jana mchana, mmoja wa viongozi wa Ukawa, Profesa
Ibrahimu Lipumba alisema: "Kwa sababu za ukiukwaji wa kanuni, tunapenda
kueleza kwamba hatupo tayari kuunga mkono, tutapinga kwa kadri ya uwezo
wetu, mambo makubwa manne kufanyika bungeni."
Alisema
mambo ambayo wanapinga ni uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba uliopangwa
kufanyika jana kabla ya ufunguzi wa Bunge maalumu unaotarajiwa kufanywa
na Rais Jakaya Kikwete.
Profesa
Lipumba pia alisema wangepinga kufanyika kwa semina ambayo ilipangwa
kuongozwa na wataalamu wa ndani au nje ya nchi leo kuhusu uzoefu katika
masuala ya Bunge la Katiba.
"Pia
tutapinga hotuba ya Rais endapo itatolewa baada ya uwasilishaji wa
Rasimu ya Katiba na pia jambo jingine lolote linalokiuka Kanuni za Bunge
Maalumu," alisema Profesa Lipumba aliyeambatana na wajumbe wenzake,
James Mbatia na Tundu Lissu.
Kanuni zinazolalamikiwa
Profesa
Lipumba alisema mara baada ya kuchaguliwa, Sitta amevunja Kanuni ya 7
(1) (g) na (h) ambazo zimeweka mpangilio wa shughuli zote za Bunge
Maalumu.
"Hotuba
ya ufunguzi ambayo itatolewa na Rais, ilielezwa wazi kwenye kanuni kuwa
itatangulia na kufuatiwa na uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba. Hivyo kwa
kutangaza kuanza kuwasilisha rasimu ni kuvunja kanuni," alisema.
CHANZO: MJENGWA BLOG
CHANZO: MJENGWA BLOG