Waziri wa ulinzi Hishammuddin Hussein (katikati) akikanusha madai ya ndege kukaa masaa manne hewani kabla ya kupotea.
...Askari
maji wa singapore wakiendelea kutafuta ndege hiyo wakiwa umbali wa
kilometa 700 kazikazini mwa Singapore na kusini mwa china.
Maafisa wa Serikali ya Malaysia waliokuwa wanadadisi picha
zilizopigwa na mtambo wa Satelite wa China ikionyesha kinachodhaniwa
kuwa mabaki ya ndege iliyotoweka, Jumamosi, wamesema kuwa mabaki hayo
yalitoweka na huenda sio mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka siku ya
jumamosi.
Waziri wa Ulinzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein, pia amekanusha madai ya Marekani kwamba ndege hiyo ilipaa kwa masaa mengi kabla ya kutoweka na kupoteza mawasiliano
Waziri wa Ulinzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein, pia amekanusha madai ya Marekani kwamba ndege hiyo ilipaa kwa masaa mengi kabla ya kutoweka na kupoteza mawasiliano
Amewaambia waandishi wa habari mjini Kuala Lumpar kuwa picha hizo
zilizopigwa siku ya Jumapili,saa ishirini na nne baada ya ndege ya
abiria ya Malaysia kutoweka na abiria 239 zinadaiwa zilitolewa kimakosa
na maafisa wa China.
Aidha tetesi kuwa kifaa cha kupeperusha matangazo cha ndege hiyo kimekuwa kikituma taarifa imesemekana kuwa si ukweli .
Waziri huyo amesema kuwa kupotea kwa ndege hiyo sio kitu kilichotararajiwa.
Picha hizo zilitolewa na idara ya serikali ya China ya sayansi na teknolojia siku ya Jumatano.
Bwana Hussein kadhalika amekanusha ripoti ya jarida la Wall Street kwambandege hiyo ilituma data ya Engine yake kwa karibu saa 4 kabla ya kupoteza mawasiliano na kituo cha trafiki ya ndege.
Amesema kuwa juhudi za kuisaka ndege ghiyo zingalizinaendelea

NA GPL