MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
"TUNAOMBA SANA MSAADA WENU MTOTO ATIBIWE KWANI ANATESEKA SANA MTOTO HUYU."
Afisa
ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya Thobias Mwalyego baada ya kupokea taarifa
kutoka kwa waandishi wa Habari alilazimika kwenda hadi mtaa wa
Maendeleo Iyunga ili kupata maelezo ya kina kutokana na ofisi yake
kutokuwa na taarifa zozote juu ya mtoto huyo.Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike amesema wakati wa tukio yeye alikuwa hayupo nyumbaniMama mzazi wa Adorotea Milika Kibelege.Hatimaye
Wazazi wa mtoto Adorotea Njavike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne
wamewasili Jijini Mbeya kutoka Mkoani Njombe baada ya kutafutwa kwa muda mrefu
kutolea maelezo ya ajali ya mtoto aliyeungua moto miezi saba iliyopita.
Ajali hiyo
imepelekea ulemavu mkubwa kwa mtoto huyo ambapo ngozi ya kidevu imeungana na
kifua na kumsababishia ulemavu unaomfanya kushindwa kula vizuri na macho
kushindwa kufumba.
Baba wa
mtoto huyo Joseph Njavike amesema wakati wa tukio yeye alikuwa hayupo nyumbani
kwani mtoto alibaki na mama yake mzazi aitwaye Milika Kibelege.
Milika
amesema kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa mbili usiku alipokuwa anapika
na yeye kupigwa na kitu kichwani kisha mtoto kudondokea motoni nay eye kuzirai
kabla ya mtoto kuokolewa na majirani baada ya kusikia kilio kikali kutoka kwa
mtoto.
Milika amesema kuwa baada ya tukio mtoto
alikuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji cha Wanzali na kwamba yeye
alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo hali iliyomlazimu Dada yake kumchukua mwanae hadi
Mbeya ili aweze kupatiwa matibabu zaidi.
Kutokana
na
uduni wa maisha wameshindwa kufika Mbeya kumjulia hali mtoto wao hadi
walipofuatwa na Dada yake Machi 8 mwaka huu kuwa wanahitajika Mbeya ili
kibali kitolewe mtoto asafirishwe kwenda Hospitali ya Mhimbili kwa
matibabu zaidi.
Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye
alitoweka na mtoto huyo amesema anaomba radhi kwa kuondoka bila kuaga
na mtoto huyo kwani alichanganyikiwa alipoambiwa mtoto itabidi
asafirishwe kwenda India na matibabu yake yatachukua miezi sita hivyo
akaona ni bora awafuate wazazi wa mtoto huko njombe wakajadiliane
Afisa ustawi
wa Jamii Mkoa wa Mbeya Thobias Mwalyego baada ya kupokea taarifa kutoka kwa
waandishi wa Habari alilazimika kwenda hadi mtaa wa Maendeleo Iyunga ili kupata
maelezo ya kina kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa zozote juu ya mtoto
huyo.
Mwalyego
amesema kuwa kuanzia sasa ataendelea kufuatilia maendeleo ya mtoto huyo
kuhakikisha anapatiwa huduma zinzostahili ukiwemo msamaha wa matibabu kutoka
Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kwa upande
wa wazazi wamewashukuru wasamaria wema waliojitokeza kuchangia matibabu ya
mtoto wao na madaktari wanaofanya juhudi za kuhakikisha mtoto huyo anapatiwa
upasuaji wa haraka.
Aidha
amekubali kuandamana na mwanae katika matibabu endapo ataruhusiwa kwenda kokote
na Afisa Ustawi wa Jamii alishauri pia Mama mkubwa kuongozana na Familia hiyo
kutokana na udhaifu wa mama Adorotea
Na Mbeya Yetu Blog
0 comments:
Post a Comment