"Hata shughuli za kilimo zinapaswa kufanyika kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo."Dk Agnes Kijazi.PICHA|MAKTABA.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya
HewaTanzania (TMA), imetabiri kuwa mvua kubwa zitanyesha hasa maeneo ya
ukanda wa pwani huku ikitahadharisha uwezekano mkubwa kusababisha maafa.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes
Kijazi alisema jana kuwa utabiri huo unaonyesha kuwa maeneo mengi zaidi
ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani... "Hata shughuli za
kilimo zinapaswa kufanyika kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa
kilimo."
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari TMA pia imewahadharisha watumiaji wa bahari juu ya mabadiliko ya
tabianchi yanayoweza kusababisha bahari kuchafuka.
Taarifa hiyo imesema kunatarajiwa
kuwapo kwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50, kati ya jana na
kesho ambazo zitanyesha mfululizo na kwamba huenda zikasababisha
madhara katika ukanda wote wa pwani.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa mvua hizo
zinasababishwa na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa Mashariki mwa
Bahari ya Hindi, sanjari na kusogea haraka kwa mvua za masika hivyo
kuongeza kiwango cha unyevunyevu kuelekea ukanda wa pwani.
Mikoa iliyopo katika ukanda huo ambayo
inaweza kuathiriwa na mabadiliko hayo ya hali ya hewa ni Mtwara, Lindi,
Pwani, Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar.
"TMA inazitaka mamlaka zinazohusiana
na majanga kuchukua hadhari zinazostahiki ili kuepuka madhara yanayoweza
kutokea kutokana na mvua hizo," ilisema taarifa hiyo.
Katika taarifa ya tathmini ya mvua za
msimu kuanzia Machi hadi Mei, mwaka huu iliyotolewa mwishoni mwa wiki
iliyopita, Mamlaka hiyo ilizitaka menejimenti za maafa na wadau wa sekta
ya afya, kuchukua hatua za hadhari kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi yanayoweza kutokea kwa kuwa baadhi ya maeneo yanatarajiwa
kupata mvua za juu ya wastani.
Chanzo, mwananchi (
0 comments:
Post a Comment