Helkopta iliyokuja na Rais Kikwete ikitua eneo la daraja la Dumila mkoani Morogoro leo.
Rais akielekea sehemu ya ujenzi wa daraja pamoja na makazi ya watu waliopatwa na mkasa wa mafuriko.
.
.
Rais JK akielekea kukagua daraja la Dumila lililokatika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo.
Rais Kikwete akikagua daraja hilo.
Rais
Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Magole mkoani Morogoro
waliokumbwa na mafuriko ambao kwa sasa wanaishi katika mahema yaliyopo
Shule ya Sekondari Magole.
Rais Kikwete akisalimiana na bibi mmoja wa kijiji cha Magole.
Rais Kikwete akiingia katika mojawapo ya hema.
Wananchi wa Magole waliokumbwa na mafuriko.
Rais Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi.
Rais Kikwete akiongea na wakazi wa Magole leo.
Wananchi wa Magole wakiwa nje ya mahema yao.
RAIS
Dk. Jakaya Kikwete leo ametua kwa helikopta kijijini Magole, Dumila ili
kukagua daraja lililoharibiwa na mvua pamoja na kuongea na wananchi wa
eneo hilo waliokumbwa na mafuriko yaliyotokea Januari 22, mwaka huu
wilayani Mvomero, Morogoro.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL)
0 comments:
Post a Comment