SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, January 28, 2014

MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA NA MZEE DUDE WA FUTUHI AFARIKI DUNIA !

 
Sudi Mohamed, 'MCD' (pichani, juu na chini) ambaye ni mpinga tumba maarufu nchini Tanzania amefariki dunia usiku huu akiwa Moshi ambako alikwenda kwa ajili ya matiabu zaidi yapata miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Meneja Hassani, MCD alipelekewa nauli ya kurudi jijini Dar esalaam leo ili arejee kesho lakini mauti yakamfika usiku mida ya saa tano na nusu. MCD amewahi kupiga katika bendi kadhaa za muziki wa dansi ikiwemo Mashujaa Band na African Stars ambako alirejea tena. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - ameen!
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa  kiongozi wa Twanga Luiza Mbutu mazishi ya MCD ilikuwa yafanyike leo saa 10 jioni, lakini familia imekubali kusogeza mbele ili wafanyakazi wenzake pamoja na marafiki wa marehemu waweze kuwahi mazishi hayo ya aliyekua mpiga tumba wa Twanga pepeta Mcd.
Msafara wa waimbaji wa Twanga pepeta,wawakilishi wa bendi zingine,wadau na marafiki, unaondoka Dar es Salaam leo saa 4 asubuhi kuelekea Moshi.
Taarifa inasema MCD alifariki sekunde chache baada ya kufikishwa  hospitali ya KCMC na atazikwa Kiislam dini ambayo ameitumikia mpaka kifo chake mbali na kuwa alishabadili dini mara kadhaa.
Usiku wa kuamkia leo,viongozi wa Twanga Pepeta,wadau na wasanii wa bendi mbali mbali walikutana na kuchagua kamati itakayoratibu safari ya kuelekea Moshi pamoja na mambo mengine ya kusaidia taratibu za mazishi.
Kamati hiyo ilikaa na kuwateua wafuatao kuwa wajumbe wa kamati hiyo amabao ni  Omary Baraka (Mkurugenzi Msaidizi ASET), Hassan Rehani (Meneja ASET), Abdallah Dossi(Mwenyekiti Macamp ya ASET), Martin Sospeter (Meneja Mashujaa Musica), Tarsis Masela (Kiongozi Akudo Impact).
Wengine ni Deo Mutta (Katibu wa Macamp ya ASET), Rehema Kiluvia (Mdau Twanga Pepeta) na Super Nyamwela (Kiongozi Mkuu Shoo Extra Bongo) na Luizer Mbutu (Kiongozi Mkuu Twanga Pepeta) ambaye ndiye mweka hazina wa kamati hiyo.
Kwa wote watakaotaka kuchangia msiba huo kwa njia ya simu za mkononi basi wanaombwa kutuma pesa zao kupitia simu zifuatazo  0653 797976,  0762 46 00 90,  0787 090 090,namba zote zinamilikiwa na Luizer Mbutu:
Source:Saluti5

 
 Mzee Dude enzi za uhai wake.
MSANII wa kundi maarufu la vichekesho na uigizaji la Futuhi, Mzee Dude amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza leo jioni!
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!

0 comments:

Post a Comment